2018-04-12 16:30:00

Ujumbe wa Mei Mosi wa Baraza la Maaskofu Italia kuhusu hadhi ya Mtu!


Hadhi ya mtu haina maana ya kuwa umehukumiwa kuwa kitu cha kubadilishwa kama fedha, badala yake ni kujumuishwa katika ule mzunguko wa umoja ili kuwa na kitu cha kuweza kupata na kutoa kwa upande wa haki na uwezo, ambao ni suala nyeti la kila jamii ya kibinadamu. Ni uthibitisho kutoka katika Ujumbe wa Tume ya Maaskofu Katoliki wa  Italia kwa ajili ya matatizo ya kijamii, kazi, haki na amani, ulioandikwa kwa mtazamo wa Siku ya Wafanyakazi duniani itakayo adhimishwa tarehe 1 Mei 2018.

Maaskofu katoliki Italia, wakikumbuka juu ya mchakato wao tangu hatua ya Mkutano wa  Wiki ya Kijamii, iliyofanyika huko Cagliari nchini Italia, wanasisitiza jinsi gani  walivyoweza kutembea katika barabara za nchi ili kuingia katika  maeneo yote  na kugundua ubora wa matendo ya dhati na matatizo mengi yaliyopo nchini mwao. Na katika Wiki hiyo ya kijamii waliweza kuona dharura tatu msingi za kujikita kwa pamoja katika safari yao nchini huo. Kwanza ikiwa ni hatua ya kuondoa vile vizingiti kwa yule anayejitahidi kuunda kazi, kwa mijibu wa maelekezo ya hotuba ya Papa Francisko aliyo huubia huko Padova Italia.

Kuunda nafasi ya kazi iliyo njema,ikiwa ni  (kazi huru , ya ubunifu,ya kushirikishana na kuunganisha) ,askofu wanathibitisha kwamba: leo hii ni moja ya aina msingi wa upendo, kwa sababu inaunda msimamo halisi ili kuweza kuondokana na  mahitaji hasa yale yanayohusu umaskini. Dharura ya pili ilikuwa inahusiana na taasisi mbalimbali za mafunzo, ikiwa ni pamoja na mashule, vyuo vikuu, taasisi za vyuo vya ufundi wa hali ya juu ili kuweza kukabiliana na changamoto za sasa. Kwa maana hiyo maaskofu wanasisitiza  hawali ya yote  kuwa hii ni kuchangamotisha vijana waweze kua na na shauku, upendo, mawazo na  wito, kiasi  kwamba bila motisha au nguvu zozote hizo, siyo rahisi kujikita katika mashindano msingi ya kupanda katika ngazi ya talanta zao.

Kwa maana hiyo Maaskofu katika ujumbe huo wanathibitisha kuwa, wanayo ndoto ambayo kwa upande wa vijana hawataweza tena kuuliza ni jinsi gani ya kuweza kupata kazi, badala yake  wao watasema tufanye kazi kwa shauku na ari njema ili kuweza kufikia malengo yao, hasa ya kuunda kazi yao mpya na thamani endelevu kwa ajili ya wema wa pamoja wa nchi  ambao kwa dhati unaundwa na jamii nzima mahali wanapoishi.

Dharura ya tatu ni ile inayohusu mtandao wa ulinzi kwa ajili ya wote walio wadhaifu:  hiki ni chombo madhubuti wanasisitiza maaskofu na ili  kijikita  ndani yake na kukarabati na kurudisha hadhi iliyopotea kwa wale wote walio baguliwa na jamii , ambao wanatamani kurudi kwa upya katika mzunguko wa kijamii waweze  kuwajibika nao ndani ya jamii. Kwa upande wa suala hili , maskofu wanaongeza kwa nguvu kusisitiza na kuomba sera za kisiasa, kuachana na mivutano yao ya kisiasa ili kuweza kuunda kile kiitwacho mtandao wa ulinzi wa pamoja ulio imara kwa ajili ya jamii na nchi kwa ujumla. Ujumbe wao unamalizika ukisema kuwa, kazi iliyo bora, ndiyo ukuu msingi wa kujikita katika nafasi yao na kubuni  mbinu mpya ambayo ni msingi  wa kila fursa ya kazi kwa maana ya utajiri uweze  kuchanua katika maisha ya kibinadamu.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!
All the contents on this site are copyrighted ©.