2018-04-12 16:01:00

Rais mpya wa Siera Leone Bw.J.Maada Bio kuanza na nguvu kazi katika nchi!


Baada ya habari za ushindi wa Bio, wachama cha watu cha upinzani, ambacho kwa miaka 10 kinaendesha upinzani walitelemka barabara za mji Mkuu Freetown. Kulikuwa na mivutano mikubwa kati ya wagombe wawili. Hata hivyo rais mpya wa Sierre Leone Bwana Maada Bio, ameunda Tume mpya ya uchunguzi kuhusiana na  ghasia zilizojitokeza kati washabiki wa chama cha upinzani kwa  aliyeshindwa urais  Bwana Samura Kamara.
 
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari  mahalia, wiki iliyopita Bwana Bio alitangazwa kuwa mshindi wa urais na kwa asilimia  51,81% dhidi ya asilimia 48,19 % ya mpinzani wake,  Bwana Kamara, ambapo lakini Kamara ametangaza kuomba rufaa ya dhidi ya matokeo pili ya uchaguzi wa urais iliyofanyika, tarehe 31 Machi 2018.

Bwana Julius Bio ambaye ni rais mpya, alikuwa tayari ameshika madaraka ya urais mara baada ya mapinduzi ya kijeshi, yaliyotokea mnamo mwaka 1986 akiwa Mkuu wa majeshi. Wakati huo huo mara baada ya uchaguzi, rais mpya wa Sirra Leone ameanza kujikita katika matendo hai ya kitaifa, kwa tangazo juu ya  Siku ya kitaifa kwa ajili ya usafi wa kila Jumamosi ya kwanza ya mwezi na kuhamasisha juu ya kupambana na uvivu nchini mwake. 

Rais Mpya Julius Maada Bio, ametangaza ya kwamba, kila Jumamosi ya kwanza ya  mwezi itakuwa ni  Siku ya Kitaifa kwa ajili ya usafi, ikiwa ni moja ya kutimiza sehemu ya ahadi kati ya majukumu ya Kampeni yake ya uchaguzi.
 
Siku ya usafi wa miji itakayo kuwa inafanyika kila Jumamosi ya mwezi itakuwa inaanza saa moja asubuhi, hadi saa sita mchana kwa mujibu wa maelezo ya Rais Bio. Na siku ya Kitaifa ya usafi, imepangwa na Wizara ya Afya kufanyika kila tarehe 5 Mei ya kila mwaka. Rais mpya Bio, aidha amesema kwamba, wafanyakazi wote wa umma na mawaziri wote wanatakiwa wawe  kila siku kazini kuanzia saa 2:30 asubuhi, hadi saa 10.45 za jioni. Yeye binafsi na makamu wake wameamua kuwa, watatafanya ukaguzi huo ofisini bila kutoa taharifa na ikitokea kuchelewa kazini, kutakuwa na uwajibishwaji au hatari ya kuachishwa kazi mara moja.
 
Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!
All the contents on this site are copyrighted ©.