2018-04-12 15:39:00

Askofu Mkuu Gallagher: Watawa wako mtari wa mbele na mashujaa wa Kanisa!


Semina ya watawa wanaohudumia katika maeneo yenye migogoro na dhidi ya mapambano ya biashara ya watu, imeandaliwa na Umoja wa Wakuu wa Mashirika ya kitawa (Uisg) kwa ushirikiano wa Ubalozi wa Marekani mjini Vatican, kwa  kusikiliza ushuhuda nyingi za watawa kwa namna ya pekee ushuhuda wa Sr Berini mwenye tuzo ya ujasiri wa wanawake 2018 kutoka kwa Melania Trump.

Mkutano uliofanyika asubuhi ya tarehe 11 Aprili 2018 Roma, uliweza kusikika sauti mbalimbali kutoka mabara mengine ambao wametoa ushuhuda wao na  msingi wa utume ambapo mara nyingi wanakumbana na hatari kwa mashirika mengi ya kitawa yanayojikita kutoa huduma hata katika kanda zenye vita na kupambana dhidi ya biashara ya binadamu. 

Huduma hiyo iko mstari wa mbele na kushuhudiwa na wengi, ikiwa pia hata Papa Francisko kuwatia moyo na msaada wa maneno yake, katika hotuba nyingi na ambazo mara nyingi anawatia moyo, kuwaalika na kutoa wito hasa kwa kushutumu vikali juu biashara haramu ya binadamu,kupinga kila aina nyingi za  utumwa mpya mamboleo, vita, uwenda wazimu na ukatili katika dunia hii.  Kutoka Sudan hadi Ufilippini, kutoka Marekani ya kusini hadi Siria, kutoka Cambodia hadi Nigeria, bila kusahau nchi za Ulaya ambamo pia yapo matukio ya kujuhusisha na ununuzi na biashara ya watu utafikiri ni bidhaa.

Kati ya matatizo yaliyo mengi sana, juhudi za watawa kwa waathirika  hao ni nyenzo hai, ambayo haikosekani kamwe kila mahali na hadi wengine kufikia kupoteza maisha kwa ajili ya ndugu. Hata hivyo katika mkutano huo hata  Balozi Marekani mjini Vatican kutoka  Bi Callista L. Gingrich ameweza kumsifu wakati wa  hotuba yake kwa namna ya pekee Sr  Maria Elena Berini,Mtawa wa  Shirika la Mtakatifu Yohana Antida  wa Thouret, ambaye pia alishiriki katika mkutano huo, kwa maana  siku chache zilizopita, amepata  tuzo ya  Kimataifa kwa ajili ya wanawake  jasiri 2018 (Women of Courage Award 2018 ), inayotolewa na Melania Trump, ikiwa ni kupongezwa ujasiri wa wanawake kwa ngazi ya kujikia katika maisha ya kijamii.

Sr  Berini, alizaliwa mwaka 1944 huko  Sondrio nchini Italia na baada ya kujiunga na utawa, alianza utume wa kimisionari na ambapo baada ya kupitia miaka kadhaa nchini Chad tangu 1972-2007, kwa sasa anaishi nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, akiendelea na huduma yake ya kuchungaji  mpakani mwa nchi ya  Chad na Kameruni.

Naye Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican, wakati wa  hotuba yake, iliyofunga kazi ya semina hiyo, aliweza kukumbuka kwa hali halisi ya  hatua za uzoefu wake wa kichungaji katika huduma ya kidiplomasia kama mwakilishi wa  Vatican wa nchi kadhaa, kwa maana yeye binafsi amesimulia uzoefu wa  Libia, Burundi, Guatemala na Australia na kuthibitisha kuwa, inahitaji ujasiri mkubwa kama ulivyo wa watawa wengi katoliki katika huduma ya watu.
 
Aidha amekuwa na utambuzi msingi wa huduma ya watawa wanayo itoa na hata wengine kupoteza maisha yao, akikumbuka mfano nchini, BURUNDI walipo uwawa watawa watatu kwa namna ya kiajabu, GUATEMALA, mahali ambapo watawa wameokoa maefu ya wasichana waathirika wa biashara ya binadamu, hata AUSTRALIA, mahali ambapo watawa wamekuwa wakisaidia jamii ya watu asili.

Askofu Mkuu Gallagher amesisitisha kwamba,  watawa katika dunia wanafanaya kazi yenye thamani kubwa na hajabu. Halikadhalika akihojiana na Vatican News, amethibitisha hayo hayo kwa moyo wa huruma na upendo mkuu, juu uwajibikaji wa wata jasiri.  Askofu Mkuu Gallagher anasema: watawa wanaonesha sura ya Kanisa, ambayo ni sura ya fumbo la Kristo kwa watu wake, kwani  watu hao ndiyo muhimu katika maisha ya Kanisa. Watawa wanao ujasiri wa kwenda katika maeneo ambayo kwa upande wa wanaume, labda wana hofu ya kwenda, ili kupeleka huruma ya Yesu kwa watu wenye dhiki na tahabu na kwa maana hiyo hawana budi kupongezwa na kutiwa moyo ili waendelee hivyo hivyo bila kukata tamaa” amethibitisha Askofu Mkuu Gallagher.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!
All the contents on this site are copyrighted ©.