2018-04-11 12:23:00

Mkuu wa Shirika la Don Bosco, Padre Fernandes kutembelea Damasko!


Mkuu wa shirika la Don Bosco, Padre Angel Fernandes Artime amefanya ziara yake mji wa kale, Damasko kwa ajili ya kuwatia moyo, furaha na matumaini watu walio jeruhiwa zaidi ya miaka 7 ya vita. Gazeti la Wasalesian wanaandika kuwa, Mkuu wa shirika hilo alifika tangu tarehe 5 Aprili 2018  nchini humo akiwa amesindikizwa  na baadhi ya vijana wa Mtakatifu Bosco  ambapo waliweza kutembea  na roho ya hija kupitia katika barabara aliyopitia Mtume Paulo Mtume wa watu na kuingia katika Kanisa la Mtakatifu Anania.

Katika Kanisa hilo, walisikiliza historia juu ya safari ya uongofu wa Mtakatifu Paulo na mwisho Padre Artime alitoa kutafakari ndogo kuhusu  umuhimu wa ushuhuda huo, na  jinsi gani unavyotakiwa hata leo hii kwa wote, ili kuweza  kubadili mtazamo wa maisha na kuyaelekeza kwa  Mungu. Siku ilimazikia katika eneo la Tabbala huko huko Damasco.

Tarehe 6 Aprili Padre Angel Fernandes, aliungana na wanajumuiya wanaoishi na kujikitia kutoa huduma  katika maeneo hayo ili kusikiliza matatizo na changamoto wanazokabiliana nazo, pia yeye  kuwaonesha ukaribu wake. Mchana  aliweza kukutana na watoto, vijana wanaohudumiwa na shirika lake katika eneo hilo, ambapo ni karibia vijana na watoto  1,000.  Vijana hao  waliweza kutumbuiza nyimbo za  burudani na ngoma kumkaribisha mkuu wa shirika hilo na hata yeye katika kushiriki furaha hiyo aliweza kushika gita ana kuimba nao!

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!
All the contents on this site are copyrighted ©.