2018-04-11 13:29:00

Kongamano la 62 kitaifa la Waseminari kuanzia 12-15 Aprili huko Padua!


Kongamano la 62 Kitaifa la Kimisionari  kwa ajili ya Waseminari nchini Italia litafanyika tarehe12-15 Aprili 2018. Kongamano hilo litaongozwa na kauli mbiu “Mavuno ni mengi na yatoa kilio”. Tukio hili limeaandaliwa na Baraza la Kipapa la umoja wa Kimisionari (Pum), Missio ni chombo cha kichungaji cha Baraza la Maaskofu wa Italia . Ni mpango ambao upo  kwa ajili ya seminari zote za  kiaskofu, mahali ambapo wataudhuria waseminari 150, kutoka katika majimbo yote ya Italia, kwa maana hiyo kuanzia kaskazini hadi kusini, kwa mujibu wa maelezo ya Padre  Ciro Biondi, Katibu wa Tume ya  Baraza la Kipapa la Umoja wa Kimisionari (PUM).

Akiendelea kueleza juu ya Kongamano hilo, Padre Biondi anasema, Kauli mbiu ya Kongamano iliyochaguliwa inajaribu kuchukua na kuendeleza ile ya Siku ya Kimisionari Duniani isemayo “ Mavuno ni mengi” lakini wao wameongeza  neno juu kilio  kwa maana ya kwamba  mavuno ni mengine lakini yaliyotawanyika na  ambayo Yesu mwenyewe alipata huruma. Anaongeza kusema kuwa, leo hii katika ulimwengu, wengi bado wanadharau ujumbe wa Kristo  na wanaishi katika mipasuko mingi, migogoro, ghasia na pembezoni. Waseminari wanapaswa kusikiliza kilio hicho na kelele za watu ili kuweza kuweka moto hai wa kupeleka mwanga wa Injili.

Katika Kongamano hilo, atahutubia Askofu Mkuu Pierbattista Pizzaballa, Msimamizi wa kitume nchi Takatifu Yerusalemu, Ijumaa tarehe 13 Aprili 2018 asubuhi masaa ya Ulaya, wakati huo huo mchana Monsinyo Francesco Innone ambaye ni Profesa wa Taalimungu ya Utatu, na Kanisa pia  mjumbe wa  Sekretarieti ya Mafunzo ya Kudumu ya Usimamizi ya Nchi Takatifu Yerusalemu atasimumulia  juu ya Mateso ya Yesu kwa ajili ya wafuasi kama vijana wa Uinjilishaji.  Madai hiyo itafafanuliwa zaidi kwa mantiki tano ambazo zitaelezwa zaidi katika  siku itakayofuata. Jumamosi 14 Aprili, Askofu Giuseppe Pellegrini wa Jimbo la Pordenone Italia, ataadhimisha Ekaristi Takatifu, mchana wanatarajia kufanya ziara mbalimbali kutembelea  hali halisi ya huduma za kimisionari Jimboni Padova. Na hatimaye, Jumapili 15 Aprili, wanatamalizia na uwakilisho wa waraka wa mwisho pia  maadhimisho ya Ekaristi Takatifu yatakayoongozwa na Askofu Claudio Cipolla wa Jimbo la Padova.

Chama cha Umisionari wameandaa Kongamano la Umisionari kwa vijana zaidi 400 kuanzia tarehe 28 Aprili hadi Mei Mosi

 “Lakini kwakuwa umesema nitatupa ndoto zangu” ndiyo kauli mbiu ya kongamano la umisionari wa vijana, lililoandaliwa na Chama cha Missio, litakalo fanyika kuanzia tarehe 28 Aprili hadi Mei Mosi 2018, huko Sacrofano Roma. Kongamano hili linawaalika vijana wote chini ya umri wa miaka 30. Atakayefungua kazi hiyo ni Askofu Franceso Beschi  wa Jimbo la Bergamo Italia na Mwenyekiti wa Missio  na Mjumbe wa Tume ya Baraza la Maaskofu kwa ajili ya Uinjilishjai wa watu na ushirikiano kati ya Makanisa na kufunga wakati wa mkesha na tafakari ya mwisho ili kutoa uamsho mpya na  shauku ya kimisionari kwa vijana chini ya miaka 30.

Ni siku tatu za mkutano wa kina ambazo zitajikita katika tafakari, shughuli ya pamoja na kufanyia  kazi ya ndoto za pamoja chini ya  mbingu iliyowazi kwa mujibu wa walio andaa tukio la Kongamano  la Missio ya Vijana. Zaidi ya vijana 400 wamealikwa  wote kutoka majimbo yote na ili wapate kusikiliza na kushiriki kwa ari moja ya kutaka kujenga mawazo ya umisionari endelevu wa Kanisa. Padre Giulio Albanese Mmsionari wa Kikomboni na mwandishi, atazugumza na vijana tarehe 30 Aprili kwa mada ya “kushuhudia ndoto” yaani ile ya umisionari wa pembezoni mwa dunia.

Wakati huo huo Padre Claudio Monge , wa Shirika la Wadomenikani na Profesa wa Taalimungu ya dini, ataongoza masifu ya asubuhi kwa tafakari ya mada kuhusu “mazungumzo ya kidini”. Padre Pietro Pierobon, mmisionari nchini Kameruni atatoa tafakari yake kwa  kutazama sura ya Mtakatifu Yosefu mfanyakazi  na kuzungumza juu ya umisionari na huduma barani Afrika. Aidha  Mwana Biblia Rosalba Manes, Profesa wa Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana atatoa tafakari juu ya safari ndefu ya sura ya Maria.

Giovanni Rocca, Katibu wa Taifa wa Missio Vijana anaeleza kuwa, huo ni mchakato wa aina yake na binafsi, ulioandaliwa kwa lengo maalumu lakini kuanzia na Neno la Yesu. Lengo la Kongamano ni lile la kujenga kwa pamoja njia za kimisionari ambazo zinaacha alama si kwa kwa sababu ya vifaa na  zana, lakini pia kuacha ishala za kiroho, ili vijana waweze kutambua zaidi namna ya kupata mwanga wa njia yao wenyewe ya kuifuata.

Sr Angela Rwezaula

Vatican News
All the contents on this site are copyrighted ©.