2018-04-11 12:51:00

Askofu wa Jimbo la Ziguinchor-Senegal anawataka waamini kuombea amani!


Askofu Paul Abel Mamba, wa jimbo la Ziguinchor, Mji mkuu wa  Casamance Mashariki ya nchi ya Senegal wakati wa mahubiri ya Sikukuu ya Pasaka, ametoa malalamiko juu ya ghasia zilizotokea mwezi Januari mwaka huu na kwamba huo ni mwendelezo wa matokeo ya vita vilivyoibuka vya nguvu uchanguzi mkuu tangu mwaka 1982. Mashambulizi ya Januari yaliwaua vijana 13, tarehe 6 Januari  katika kijiji cha Boffa-Bayottes.

Mashambulizi hayo yametokana na baadhi ya makundi chama  cha viongozi tawala cha nguvu ya Demokrasia ya Casamance (MFDC) lakini  viongozi hao wanakanusha kuhusika na mashambulizi na mauajai hayo. Kwa mujibu wa Askofu Mamba anathibitisha kuwa tangu wakati huo mivutano  katika kanda imezidi kuongezeka.  Na tarehe 29 Machi kulitokea wizi katika barabara ya Ziguinchor-Oussouye ambapo watu wenye silaha,walimuua mtu mwenye umri wa miaka 33 na wengine wawili kujeruhiwa.  Vilevile wiki moja kabla, watu wenye silaha walikuwa wameogopesha watu wa kijiji cha Kaguitte- Ziguinchor na kumteka nyara mwanamke mmoja.

Askofu kwa masikitiko yake amesema utafikiri wanarudi nyuma kwasababu hadi sasa walikuwa tayari wameanza mazungumzo yanayo endelea kuhusu amani , kwa njia hiyo anawaalika makundi hayo kuacha kutumia silaha, kwasababu anaongeza kuthibitisha  nguvu hazisaidii kitu.Majeshi yenye nguvu zaidi ulimwenguni hayakuwahi kujipatia amani kamwe  kwa njia ya nguvu. Ni kwa njia ya mazungumzo tu na kusikilizana mmoja na mwingine, inawezekana kufikia amani ya kweli. Amehitimisha akiwaalika waamnini wote kuomba zawadi ya amani katika kanda hiyo.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!
All the contents on this site are copyrighted ©.