2018-04-10 13:21:00

Papa Francisko amefanya Katekesi 15 juu ya Ibada ya Misa Takatifu


Baba Mtakatifu Francisko hivi karibuni amehitimisha katekesi 15 zilizokuwa zinahusu sehemu za Liturujia ya Misa Takatifu, kuanzia Ishala ya Msalaba hadi  baraka ya mwisho. Turudi katika uwanja wa Mtakatifu Petro ili kuweza kukumbuka kipindi chote  cha katekesi zake 15 alizofanya kwa miezi mitano iliyopita kabla ya utangulizi wa  katekesi nyingine mpya ijayo. Baba Mtakatifu akikumbusha umuhimu wa  Misa Takatifu anasisitiza kuwa:wakati wa misa ni muhimu sana wa kujiunda ndani ya moyo ili kuwaza unachokifanya mbele ya Yesu, hivyo ni muhimu kuwa makini na mambo ambayo yanaweza kukuondolea ule usikivu hasa katika matumizi ya simu za mikononi. Kutokana na hilo alitoa onyo kali kwamba,hakuna kutumia simu za mikono pia kuepuka maeneno wakati wa maadhimisho ya Misa Takatifu kwa maana Misa siyo tamasha, ni Pasaka ya Kikristo!

Akianza na ishara ya msalaba, Baba Mtakatifu alisema kuwa: watoto wengi hawajui kufanya ishala ya msalaba vizuri. Wanatambua kuchora picha ya Msalaba tu, hivyo ni wajibu wa kuwafundisha vema watoto wakiwa wadogo. Hiyo ndiyo  maana ya kuanza misa, maisha na siku. Papa aliyasema hayo bila kuandika katika Katekesi yake ya kwanza kuhusu Misa Takatifu,  tarehe 8 Novemba 2017 na kurudia neno hilo tarehe 20 Desemba 2017, akiwataka wazazi na wazee kuwafundisha watoto tangu mwanzo kufanya ishala hiyo vema ambayo  ni ya  kikristo kwa hakika.

Katika katekesi ya tarehe 15 Novemba 2017; Baba Mtakatifu aligusia juu ya ukimya wakati wa Misa kwamba, Misa ni sala na hawali ya yote sala ni ukimya. Kwa maana hiyo tunakwenda katika misa, siyo katika tamasha. Misa ni makutano na Mungu na Kanisa siyo jumba la makumbusho.
Tarehe 22 Novemba, alielezea juu ya Karvario kwamba: misa ni kama kwenda Karvario  akifafanua maana ya Misa kama kufanya kumbukumbu zaidi ya kukumbuka. Tarehe 13 Desemba 2017, alisema, kwenda si kwendakatika Misa ya Jumapili kwasababu ya sheria ya Kanisa, bali kufanya Domenika ya kikristo. 

Alitoa mfano na kusisitiza kuwa: jamii iliyobobea katika ulimwengu, kama imesahau, ni kwamba bila Kristo ni kama kuhukumuwa  kutawaliwa na uchovu wa kila siku. Kwa maana hiyo ni muhimu kutafuta maana ya pumziko la siku ya  Jumapili iliyoundwa na ukristo. Kwa mwaka mpya Baba Mtakatifu aliufungua na sehemu ya maungamo ya jumla katika Liturujia, mahali ambapo tarehe 3 Januari 2018, alisema: haitoshi kutomtendea vibaya jirani, inatakiwa kuwa na uchaguzi ili kuweza kuepuka  kutotimiza wajibu, ikiwa na maana ya  kuacha kile ambacho ulikuwa unatakiwa kutenda na kwa hofu au kuona aibu unawasingizia wengine.

Baba Mtakatifu alitoa ushauri kuwa, ni lazima  kupima udhaifu  ulio nao kama ule wa udongo wa mfinyanzi ambao kwa  wote tumetokea na kufanya uzoefu ili kuimarishwa. Ni lazima kutafiti dhamiri na kuona udhaifu, ili uweze kufunguka moyo na kuomba huruma ya Mungu ikubadili na kuongoka. Ni tendo ambalo linafanyika katika liturujia ya maungamo ya ujumla mwanzoni mwa kuanza Misa.

Kwa kufafanua ukimya alisema, haina maana ya kukosa maneno ya kuzungumza, katika katekesi ya tarehe 10 Januari 2018. Wakati wa maombi, Padre anaamsha  mikono yake akiiga Yesu aliye na mikono wazi  katika msalaba. Kuna ukimya baada ya mahubiri, kabla ya  maombi ya ulimwengu na  baada ya sala ya Nasadiki. Na kwa upande wa maombi, ni wakati wa kumwomba Bwana mambo ya nguvu wakati wa misa, mambo ambayo tuhahitaji  au kutamani. Ni tafakari ya katekesi yake ya tarehe tarehe 14 Februari 2018. Baba Mtakatifu alitoa onyo kuhusu mantiki za kiulimwengu ambapo nasema , Mungu haweze kusikiliza maombi ya mantiki za kiulimwengu, hivyo alihimiza kuomba jambo ambalo ni la kweli na linastahili mbele ya Mungu.

Vilevile Misa inatakiwa kufanyika moja kwa moja na siyo kusikia wanasema. Ni  kwa mujibu wa katekesi ya tarehe 31 Januari 2018 wakati anafafanua juu ya sehemu ya Neno la Mungu wakati wa Misa Takatifu. Habari ya kweli ma njema ya siku, kwa mkristo siyo ile  inayosomwa katika gazeti, kimyume chake ni Neno la Mungu!. Katika Misa Takatifu tunasoma Injili ili kuwa na dhamiri ya kile ambacho Yesu alifanya na alisema wakati ule! Na wiki iliyofuata akasema: Mahubiri siyo kama hotuba ya sikukuu fulani au  katekesi na mikutano ya uchaguzi.  Mahubiri ni mwendelezo wa tafakari ya mazungumzo yaliyofunguliwa tayari kati ya Bwana na watu wake kupitia Neno la Mungu, ili iweze kufikia utimilifu wake katika maisha ya kila siku. Kwa njia hiyo mahubiri yanatakiwa yawe mafupi na siyo zaidi ya dakika kumi, alisistizia hilo Baba Mtakatifu.

Kiini cha Misa Takatifu ni Kristo.  Altare ni Kristo na altare ya kwanza ni Msalaba. Aliyasema hayo katika katekesi ya tarehe 28 Februari   2018 wakati anafafanua Liturujia ya Ekaristi. Yesu mwenyewe anatoa mwaliko wa kitu kidogo sana, lakini  Yeye anatupatia yaliyo makubwa zaidi  kama vile, utashi mwema, moyo uliofunguka, utashi wa  ubora zaidi na mwema ili kumpokea katika Ekaristi. Katika katekesi ya tarehe 7 Machi, alisema  katika maombi ya Ekaristi, hakuna yoyote anasahulika,iwe kwa ajili ya ndugu zetu wapendwa, waliopo na wale ambao hawapo tena. Lakini  kwa kuwaombea ndugu waliotangulia haijatajwa gharama yoyote kwa maana hiyo, Misa Takatifu hailipiwi ni ya bure kama sadaka ya Kristo! 

Kuwasamehe walio tukosea siyo rahisi, ni neema ambayo tunatakiwa kuomba. Haya ni afakari ya Baba Mtakatifu wakati wa anafafanua  juu ya sala ya “Baba yetu Aliye Mbinguni” tarehe 14 Machi. Yesu anasamehe daima na hachoki kusamehe, bali ni sisi tunachoka kuomba, alirudia maneno hayo hata katika katekesi yake ya tarehe 21 Machi, kwa kuonesha tunu msingi zitokanazo na Komunio maana anasema kuwa, tunageuka kuwa kile tunachokipokea kwasababu kila tunapopokea komunio, tunafanana zaidi na Yesu na kugeuka zaidi katika Yesu. Wakristo hawendi katika Misa ili kufanya mazoezi ya wiki. Ni tafakari ya Katekesi yake ya mwisho kuhusu Liuturujia ya Misa Takatifu iliyofanyika tarehe 4 Aprili 2018. Baba Mtakatifu Francisko anaonesha hatua madhubuti ya kuwajibika hasa katika maadhimisho ya Misa, hasa bada ya Misa kujikita katika matendo ya dhati ya maisha ya kila siku.

Amehimiza kufungua roho katika ukuu wake na siyo kubaki na ufinyo wa mioyo kwa mambo madogo madogo ya ubinafsi. Ni kufungulia roho katika ukuu wa mambo makuu na yenye upeo wa hali ya juu. Matunda ya Misa yanapaswa yakomae katika maisha ya kila siku, kwa sababu misa ni mbegu ndogo ya ngano ambayo inatutengenisha na dhambi, inatuwajibisha kukabiliana na wengine zaidi maskini, kupitia katika mwili wa Kristo kwenda katika mwili wa ndugu ambao wanasubiri weweze kutambuliwa, kuhudumiwa kuheshimiwa na kupendwa. Ekaristi inatengeneza Kanisa ambalo linaunganisha wote.Na maisha yetu daima yaweze kuchanua kama ya Pasaka, kwa maua ya matumaini, imani na matendo mema. Na ili sisi tuweze kupata nguvu daima katika Ekaristi, umoja na Yesu.

Sr Angela Rwezaula 

Vatican News!
All the contents on this site are copyrighted ©.