2018-04-08 13:10:00

Papa:Viongozi na wanajeshi wachague njia ya mazungumzo kuliko mabomu!


"Kabla ya Baraka ya mwisho tusali kwa mama yetu wa Mbinguni, lakini kabla zaidi, ninapenda kuwashuru ninyi nyote ambao mmeshiriki maadhimisho haya, kwa namna ya pekee Wamisionari wa Huruma waliofika kwa ajili ya mkutano wao.Ninawashukuru wa huduma yenu". Ni utangulizi wa maneno ya Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya Misa Takatifu na kabla ya sala ya Malkia wa Mbingu katika viwanja vya Mtakatifu Petro, mjini Vatican tarehe 8 Aprili 2018, Mama Kanisa akiwa anaadhimisha Domenika ya Pili ya Pasaka ambayo inaitwa Domenika ya Huruma ya Mungu.

Baba Mtakatifu anaendelea kusema: "tuwaombee ndugu, kaka na dada wa nchi za Mshariki ambao kwa mujibu wa kalenda ya Juliano wanaadhimisha Sikukuu ya Pasaka", hivyo anawatakia matashi mema na kwamba,  Bwana mfufuka awaangazie kwa  amani, awape nguvu jumuiya wanazoishi katika hali ngumu.  Vile vile  ametoa salamu maalumu kwa Jumuiya ya Waroma na Sinti ambao wameudhuria misa hiyo Takatifu  wakiwa wanaadhimisha Siku yao Kimataifa. 

Anawatakia amani na undugu,wanachama hao na watu wa kale kwa kuwatakia matashi mema ya mkutano wao ili uweze kuwa fursa ya kutambuana  na kuheshimiana.Kwa maana anathibitisha kuwa:  ni kwa njia hiyo inapelekea ushirikishwaji wa kweli. Na anawaombea hao Waroma na Sinti pia kuwaomba wasali kwa pamoja kwa ajili ya ndugu wahamiaji wa nchi ya  Siria. Mwisho amewasalimu hata  mahujaji wote, makundi ya kiparokia, familia, vyama mbalimbali  na wote kwa pamoja amewaweka chini ya ulinzi wa Maria, Mama wa huruma na kusali sala ya Malkia wa Mbingu........

Baada ya Sala ya Malkia wa Mbingu (Regina Coeli)
Mara Baada ya Sala ya Malkia wa Mbingu, Baba Mtakatifu Francisko kwa masikitiko makubwa ,amesema kuwa, zimefika habari mbaya kutoka nchi ya Siria kuhusiana na  mashambulizi ya  mabomu ambayo yamesababisha waathirika wengi, kati yao wanawake na watoto. Habari zinathibitisha kwamba kuna matokeo mabaya ya tindikali iliyochanganywa na mabomu hayo! Papa anasema tuwaombee marehemu wote, watu walio jeruhiwa na  kwa ajili ya familia zao wanaoteseka. 

Anathibitisha kuwa, hakuna vita njema, bali ni ukatili, na  hakuna kinachoweza kuthibitisha juu ya utumiaji wa zana hizo za kuangamiza wimbi la watu wengi hivyo!. Kwa maana hiyo nasema, tuwaombee wahusika wa kisiasa na wanajeshi ili  waweze kuchagua njia nyingine  hasa ile ya mazungumzo ambayo ndiyo njia moja pekee  ya kuweza kuleta amani na siyo ile ya kuleta kifo na uharibifu kwa njia ya mabomu ya maangamizi makubwa.

Na Sr Angela Rwezaula 

Vatican News!
 








All the contents on this site are copyrighted ©.