2018-04-08 12:49:00

Domenika ya Huruma:Ni kwa njia ya Makovu,Mitume walimtambua Yesu mfufuka!


Katika Injili ya siku neno “kuona” limerudiwa mara nyingi: “Basi Mitume wakafurahi mno kumwona Bwana (Yh 20,20);na  baadaye wakamwambia Thoma; Tumemwona Bwana” (Yh 20,25). Lakini Injili haielezei  namna gani ya  kumwona au kuelezea mfufuka, japokuwa wanaeleza jambo moja muhimu kwamba  aliwaonesha mikono yake na ubavu wake, (Yh 20,20). Hii ni kutaka kusisitiza jinsi gani mitume walimtambua Yesu yaani kwa njia ya makovu yake. Tendo hilo pia lilimtokea hata Thoma.  Yeye alikuwa anataka kumwona mikono yake na alama za misumari kwa maana alisema “nisipoona mikononi mwake alama za misumari na kutia kidole changu katika kovu hizo, na kutia mkono wangu ubavuni mwake, sitasadiki”. Lakini baada ya kuona akasadiki. 27).

Huo ni utangulizi wa mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko tarehe 8 Aprili 2018 katika Misa Takatifu ya Domenika ya pili ya Pasaka ambayo ni Sikukuu ya Huruma ya Mungu; ni katika Misa Takatifu iliyoadhimishwa  katika viwanja vya Mtakatifu Petro Mjini Vatican saa 4.30 asubuhi masaa ya Ulaya na kuudhuriwa waamini na mahujaji wengi kutoka pande zote za dunia.

Baba Mtakatifu akiendelea na mahubiri yake anasema, pamoja na kutokuamini, ni lazima kumshukuru Thoma kwasababu hakuridhika tu kusikia kutoka kwa wengine kuwa, Yesu ni mzima,na  hata kwa kumwona mwili na mfupa tu, bali alitaka kumwona ndani, kugusa kwa mkono wake makovu na ishala za upendo wake. Injili inamwita Thoma kuwa ni Pacha (Yh 20,24), Baba Mtakatifu anathibitisha kuwa huyo kweli ni kaka yetu pacha. Hiyo ni kwasababu, hata sisi haitoshi kujua kuwa Mungu yupo: pia haijazilishi  Maisha ya Mungu aliyefufuka na hata kuwa na shauku ya Mungu pamoja na utambuzi kuwa ni mwenye haki na Mtakatifu,badala yake, hata sisi tunayo haja ya kutaka kuona Mungu, kumgusa kwa mikono aliyefufuka kwa ajili yetu. 

Tunawezaje kumwona? Kama mitume, ni kwa njia ya makovu yake. Kwa kuyatazama, walitambua kuwa hakuwapenda kimchezo, aliwasamehe, pamoja na kwamba kati yao wengine walimsaliti na kumkimbia. Kuingia katika makovu yake ni kutafakari upendo upeo ambao unabubujika kutoka ndani ya moyo wake. Ni kuutambua upendo wake unavyodunda kwa ajili yangu, yako na kwa kila mmoja.  Baba Mtakatifu anasisitiza ya kuwa, tunaweza kujifanya tunajua na kuongea thamani nyingi lakini kama mitume, hatuna budi kutazama Yesu na kukuguswa na upendo wake. Ni kwa njia hiyo tu, tunatembea kwa moyo wa imani na kama mitume tunapata amani na furaha ya nguvu zaidi ya hofu (Yh,20 19-20).

Thoma baada ya kuona makovu ya Bwana alisema, “Bwana wangu na Mungu wangu”! (20,28). Kutokana na neno hili, Baba Mtakatifu amependa kusisitiza  juu ya mtazamo wa Thoma anayerudia kusema “wangu”. Anaelezea kuwa Wangu ni  kivumi miliki na iwapo tunatafakari vema , tunaweza kufikiri ni suala mabao liko  nje na Mungu kwa maana inawezekanaje Mungu akawa wangu? Ninawezaje kumfanya Mwenyezi awe wangu? Lakini kwa dhati, Baba Mtakatifu anafafanua ya kuwa,  kusema wangu si kukufuru Mungu, bali maana yake ni kutukuza huruma yake kwasababu ni Yeye aliyejifanya kuwa karibu nasi. Ni kama historia ya upendo kumwambia: umejifanya mtu kwa ajili yangu, umekufa na kufufuka kwa ajili yangu na sasa siyo Mungu tu, bali wewe ni Mungu wangu na ni maisha yangu. Kwako wewe ninapata upendo ambao nilikuwa ninautafuta na zaidi nilivyokuwa sitegemei!

Mungu hachukii, kwa maana hata  mwanzo wa amri kumi za Mungu inasema: mimi ni Bwana na Mungu wako (Kut 20,2), pia mimi ni Bwana na Mungu wako mwenye wivu(Kut 20,5). Ndilo jibu la Mungu mpendwa na  mwenye wivu ambaye anajieleza kama Mungu wako.Na ndiyo  maana katika moyo wa Thoma uliojaa utambuzi huo alijibu, “Bwana wangu na Mungu wangu”. Katika kuingia leo hii kupitia makovu yake katika fumbo la Mungu, tunatambua kuwa huruma ya Mungu ni mapigo ya moyo wake na yenye kuwa na thamani ya hali ya juu, na tunageuka hata sisi kuwa wapendwa wa kweli wa Bwana. 
Ni jinsi gani ya kuonja utamu wa upendo wake, ni jinsi gani ya kugusa leo hii kwa mkono wetu huruma ya Yesu? Baba Mtakatifu anafafanua kuwa, Injili leo hii inatoa jibu, ikiwa  inasititiza jioni ya Pasaka (Yh 20,19), baada ya kufufuka Yesu kwa mara ya kwanza anawavuvia Roho ya kuondolea dhambi. Na ili kufanya uzoefu wa upendo lazima kupitia pale, yaani kuacha usamehewe dhambi, japokuwa Baba ;takatifu anabainisha kwamba  kwenda kuungama wakati mwingine inaonekana kuwa vigumu.

Mbele ya Mungu tunajaribiwa kufanya kama  walivyofanya mitume katika Injili kwa maana walikuwa ndani ya nyumba milango imefungwa. Walifanya hivyo kutokana na kuogopa, hata sisi tunayo hofu, tunayo aibu ya kufungua na kusema dhambi zetu.Lakini  Bwana anatupatia neema ya kutambua aibu, kuzitazama na si katika milango iliyofungwa, bali hata  kufanya ile hatua ya kwanza ya kukutana. Tunapohisi aibu, ni lazima kuwa na shukrani, kwa maana ni kuonesha kuwa hatukubaliani na mabaya, hivyo ni hatua nzuri. Aibu ni mwaliko wa siri ya roho ambayo inahitaji Bwana ili kushinda ubaya. Janga kubwa ni lile la kutokuwa na hofu kabisa anasisitiza Baba Mtakatifu na hofu ya kuhisi aibu ili kuweza kundokana na aibu hiyo kuelekea katika msamaha! 

Kuna mlango uliofungwa mbele ya msamaha wa Bwana, hasa ule wa kukata tamaa. Walifanya uzoefu mitume wa Yesu ambao wakati wa pasaka walitaka yote yarudi kama ilivyokuwa mwanzo. walikuwa pale Yerusalemu , wakemata tamaa; walifikiri kurasa za Yesu zimemalizika na kufungwa mara baada ya kukaa  nao kwa muda mrefu, lakini hakuna kilichobadilika. Baba Mtakatifu anaongeza kusema, hata sisi tunaweza kufikiria: mimi ni mkristo wa muda mrefu, lakini sibadiliki kit una ninatenda dhambi zilezile. Kukata tamaa maana yake ni kukataa huruma. Lakini Bwana bado anatoa mwaliko: uamini kuwa huruma yangu ni kubwa kuliko dhambi zako. Iwapo wewe si mwepesi wa kuomba huruma, omba huruma na utaona vizuri. Halikadhalika anayetambua sakramenti ya kitubio hawezi kusema kuwa yote yanabaki kama mwanzo kwa maana kila  msamaha unasafisha, unatia moyo ili kuhisi kuwa tunapendwa zaidi. Wakati tunapendwa na kuanguka tena  tunahisi uchungu zaidi ya kwanza, lakini uchungu ho ni wa faima maana unatuwezesa taratibu kuacha dhambi na kugundu nguvu ya maisha na kupokea msamaha wa Mungu wa kuendelea mbele na msamaha huo huo.

Baada ya aibu na kukata tamaa, Baba Mtakatifu anaongeza kusema kuwa nina  mlango mwingine zaidi uliofungwa yaani ni dhambui zetu. Kwa maana iwapo  hatutaki kufungua mlango  wote ukabaki nusu,  Mungu hawezi kamwe kupanda  kwa nguvu kuingia .Yeye kama Injili inavyofundisha anapenda kuingia katika mlango uliofungwa, hasa mahali ambapo umewekwa vizingiti vya kutokuweza kuingia. Na ndipo Mungu hutenda maajabu sehemu hiyo. Yeye hatoi  uamuzi wa kukaa nasi mbali kama vile sisi tnavyotaka kuwa mbali naye. Lakini tukiungama,ndiyo muujiza  mkubwa unatoke maana ni kugundua ukaribu wake nawa makutano. Pale mungu aliyejeruhiwa kwa ajili ya upendo wetu na kuyafanya makovu yetu sawa na ya kwake yaliyo matukufu anaonekana;hivyo Mungu ni huruma na anatenda maajabu katika udhaifu wetu. Hapo kuna mabadiliko , maana udhaifu wangu unafafanan na makovu yake matakatifu. Kwasababu yeye mwenye huruma anatenda maajabu katika udhaifu wetu. Kama Thoma tuombe  neema ya kutambua Mungu,ili tupate msamaha wake na furaha na kupata huruma yake na matumaini.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!
All the contents on this site are copyrighted ©.