2018-04-07 16:20:00

Papa:Jumuiya ya Emanueli iwe na msingi wa kutafakari fumbo la Kristo !


“Ninayo furaha  ya kukutana nanyi katika fursa ya mkutano wenu wa mwaka ambao unafanyika kwa mara nyingine Roma. Hija hii ni ishara kamili ya kushiriki katika Jumuiya ya Emanueli na umoja wa Kanisa zima Katoliki. Ni fursa hata kwangu kuwashukuru kwa ajili ya uaminifu wenu, hata ule upendo wa kaharifa wa mtume Petro na ninawasifu kwa  jitihada zenu za kimisionari  na ambapo kwa sasa karibu  mpo katika mabara yote, ninawata moyo kuendelea katika wakati ujao”.
 
Ni maneno ya hotuba ya Papa Francisko aliyoanza nayo wakati alipokutana na Jumuiya wa Emmanuali kutoka nchini Ufaransa , katika ukumbi wa Clementina Mjini Vatican.  Jumuiya ya Emmanuel ilianzishwa huko na   kikundi cha Maombi ya uhuisho wa roho Mtakatifu Katoliki, iliyoanzishwa  mwaka 1972  huko Paris Ufaransa na Pierre Goursat na Martine Laffitte-Catta, mwaka 1976 wakawa na katiba yao. Shughuli ya wanachama wa Jumuiya hii wanayo shauku ya kuishi tasaufi ya kuabudu , upendo na kuinjilisha hali halisi ya Emanuel yaani Mungu pamoja nasi katika maisha ya kila siku.

Papa Francisko akiendelea na hotuba yake anasema, uendelevu wao unajikita  hata katika utambuzi wa Chama cha walei wa Jumuiya ya Emanueli ambapo tarehe 15 Agosti 2017 , wametambuliwa kutokana na fursa na sababu za kuwa na  idadi kubwa ya miito ya kipadre ambayo karama ya Emanueli inatoa na kwa ajili ya matunda ya Uinjilishaji. Lakini mbali na kisiwa cha mapre wa jumuiya nyingine, walei au watawa wanao waombea juu ya kujulikana, Papa kinyume chake anasema, wao wanapaswa kuwa hai katika umoja kati ya maisha yote, mahali ambapo wao wanafanya uzoefu karibu miaka 40, katika kutafakari aina mbalimbali za miito, Na kuwaalika hata jumuiya yao  iwe na uhusiano daima wa nguvu katika hali halisi ya utajiri wa Parokia mahali ambapo wanaishi na kushirikishana vema katika matendo ya kichungaji ya Kanisa mahalia ( Evangelii gaudium, 29).

Karama ya Jumuiya ya Emanueli  imeandikwa jina: Emanueli, Mungu pamoja nasi ni muhimu katika kutafakari fumbo la aliyefanyika mwili kwa namna ya pekee katika kuabudu Ekaristi, kwani wanachota uhai wa safari ya kimisionari wa kutangaza Habari Njema kwa wote ambao Yesu amewaita rafiki zake. Papa anawatia moyo waendelee kugundua  hali halisi ya  ya Kristo kwa kwa watu wote katika muda wao na mahali popote watakapotumwa; waone huruma ya Mungu ambayo imewapenda hadi akatifa na  kukaa ndani mwao. Huruma ya Bwana daima ipo karibu na watu wake na inataka  ipendekezwe kwa shauku mpya kwa njia ya matendo ya kichungaji kwa njia  mpya ili iweze kugusa mioyo ya watu na kuweka muhuri na hatimaye wao waweze kupata njia ya kurudi kwa Baba( Misercordiae Vultus, 15). Roho hiyo inaweza kuwapo mahali popote jumuiya ilipo na kuonesha huruma ya Baba kwa namna ya pekee kwa maskini wa kukithiri, katika moyo na mwili na kuponyesha majeraha kwa faraja ya Injili, mshikamano na umakini.

Papa anaendelea, tangu mwanzo  Jumuiya ya Emanueli, imetambua kujieleza hali halisi ya kutangaza Habari njema kwa namna hai na furaha. Anawashauri wabaki katika mzizi wa Kristo hasa kwa  maisha ya undani na kuamini Roho Mtakatifu ambaye anakuja kusaidia udhaifu na kuponya kila kitu kinacholeta udhaifu huo katika  shughuli za kimisionari; awaimarishe ndani ya mioyo yao, shauku ya kutangaza Injili kwa furaha kwa wale wasio ijua au walio potea; wawe msari wa mbele katika Kanisa linalotoka nje, na ikiwa ndiyo shauku ya juu ya matashi ya Papa. Kanisa linawategemea , kwa uaminifu wa Neno, katika uwajibikaji wa huduma na katika ushuhuda wa maisha yanayobadilishwa na  Roho Mtakatifu (hotuba ya Papa Mkesha wa Pentekoste , 3 Juni 2017).

Pamoja nao anashukuru kwa hatua walitopiga kwa nia ya msukumo wa Roho Mtakatif ambayo daima anawasindikiza katika safari na wanawatakiwa wabaki daima katika usikivu wake kwasababu hakuna uhuru ulio mkubwa zaidi wa kuacha kuongozwa na Roho na ambaye anasaidia kuanga na kupeleka mahali ambapo anataka .Amewakabidhi kwa maobezi ya Bikira Maria na kumwomba ili waogoze njia za ona kuwalinda juhudi zao. Amewabariki na kuwaomba wasali kwa ajili yake.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!
All the contents on this site are copyrighted ©.