2018-04-07 16:00:00

Papa na Vijana wa Brescia Italia:Jikane binafsi na kuvua utu wa zamani!


Wasema kuwa mahali walipo vijana kuna kelele, lakini hapa kuna ukimya….(Wote makofi na vifijo…) Ninawashukuru kwa makaribisho yenu na kumshukuru Askofu kwa utangulizi wa hotuba yake na wote walio wasindikiza katika hija hii. Ni utangulizi wa meneno ya  Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi  tarehe 7 Aprili 2018 alipokutana na vijana 3,000  kutoka Jimbo Katoliki  la Brescia nchini Italia  kwenye  Ukumbi wa Mwenyeheri Paulo VI.

Akiendelea na hotuba yake, anasema alivyoshangazwa na maeno ya kijana aliyetajwa katika hotuba ya Askofu wao na maneno ambayo tayari mwenyewe alikuwa anayafahamu kwanza . Swali hilo lilikuwa linauliza “lakini maaskofu wanaamini kwamba vijana wanaweza kubadili Kanisa”? Baadaye, Papa alitaka kujua kama kijana huyo alikuwa miongoni mwao, japokuwa  kwa bahati mbaya hakuwapo. Lakini kwa upande wake  amesema kuwa anaweza kumjibu na wote hao kwamba, swali hilo liko moyoni mwake na ndiyo maana Sinodi ijayo ya maaskofu ijayo inawatazama Vijana, imani na Mang’amuzi ya Miito. Papa anaongeza kusema kuwa,  hata hivyo wao tayari wako katika maandalizi na yeye pia anaweza kushuhudia kuwa wanafanya hivyo maana wao wanaonesha hivyo katika  shughuli wanazoendelea kufanya  katika Jimbo lao. 

Halikadhalika akigusia juu ya usikivu anasema kwamba usikivu wa  kweli una maana ya kuwa na uwezekano wa kubadili kitu, kutembea pamoja na kushirikishana ndoto kama alivyosema yule kijana. Pamoja na hayo  ametaka naye kuuliza swali, iwapo swali la kijana lilikuwa ni kutaka kujua kama maaskofu wako tayari kuwasikiliza. Je vijana na wako tayari kusikiliza Yesu na kubadili kitu katika maisha yao? Swali hilo amewachia ili wajiulize ndani ya mioyo yao.  Lakini anaongeza kusema kwamba, anafikiri  wako tayari iwapo wamekuwa tayari kufika na kukutana mahali hapo, japokuwa hawezi kujua uhakika wao ndani yao binafsi. Ni kazi ya kila mmoja kujitafakari katika moyo, iwapo wako tayari kufanya hatua na kuota kama Yesu au wanayo hofu ya kwamba ndoto hizo zinaweza kuharibiwa mipango yao.

Papa anaendelea, Je ndoto ya Yesu ilikuwa ni ipi? Ilikuwa ile ya Injili inayoitwa Ufalme wa Mungu. Ufalme wa Mungu maana yake ni  upendo na Mungu na upendo kati yetu  ambao unatengeneza  familia kubwa  ya ndugu kaka na dada na Mungu kama Baba ambaye anapenda watoto wake na huwa na furaha kubwa kwa yule anayepotea lakini na kurudi nyumbani.  Na hiyo ndiyo ndoto ya Yesu. Papa ameuliza swali tena kama wako tayari kufanya hivyo na kubadilika ili wakumbatiwe na ndoto hiyo (vijana wamejibu ndiyo….) na kuongeza kusema, ili kuweza kukumbatiwa na ndoto hiyo, ni lazima kujikana binafsi,lakini haina maana ya kujidharau kwa kile ambacho Mungu alikuzawadia kama vile maisha, mwili na mahusiano. Badala yake, Mungu nataka umfuase na kujikana biafsi, kwa maana kila mmoja ndani ya maisha yake anayo kile kiitwacho katika Biblia, “mtu wa zamani. Yaani ubinafsi usio fuata mantiki ya Mungu, au mantiki ya upendo, badala yake ni kufuata mantiki tofauti ya ubinafsi na kufanya matakwa binafsi ambayo mara nyingi ni kama vile kujivunika  kitambaa bandia machoni, utafikiri una sura ya wema na kumbe umeficha ubinafsi!

Ili  kuondokana na utumwa huo wa ndani, katika kupendelea utajiri na tamaa za ubinafsi, Papa anasema inahitaji hata ushirikiano wetu , yaani wa kuomba Msamaha kwa Yesu, kuweza kuwa na moyo kama wa kwake. Mwambie Yesu nisamehe, nipe moyo kama wako,wa unyenyekevu na uliojaa upendo. Kwa maana Yesu alikuwa hivyo na moyo mzuri na alipenda anatthibitisha Baba Mtakatifu kwa vijana hawa! Papa Francisko anaendelea kueleza vijana kwamba, anayesali hivyo, Yesu anamshangaza, kama vile  furaha mpya ya kutaka kusoma Injili, au kuhisi kupenda kuudhuria Misa, jambo ambalo kwa vijana siyo kawaida yao, au kuhisi upendo wake kwa watu wanaoteseka,wagonjwa, waliobaguliwa na hata ujasiri wa kwenda kunyume na mambo ya sasa ya kuhukumu wengine.

Ili kuweza kuonesha hayo kwa dhati anasema, wapo watakatifu kama Mtakatifu Francisko wa Azizi, ambaye alijikana ubifsi wake, alikuwa amejazwa na ndoto za ulimwengu huu na baadaye akakumbatiwa na busu la ndoto za Yesu. Hata Mwenye heri Papa Paulo VI ambaye ametajwa na Askofu wao Pierantonio Tremolada katika hotuba yake na ambaye atatangazwa hivi karibuni Mtakatifu. Giovanni Montini, ambaye ni  Papa Paulo VI, Papa ambaye alikuwa ni kijana kutoka katika ardhi yao.Anahitimisha hotuba yake akiwaomba vijana wafanya mazoezi nyumbani. Kugundua jinsi gani Giovanni Battista Montini yaani (Mwenyeheri Papa Paulo VI) alikuwa wakati wa ujana wake ; alivyoishi katika familia yake; akiwa mwanafunzi na katika kikundi cha katekisimu na ndoto zake zilikuwa zipi. Amewahimiza wafanya hivyo!

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News

 
All the contents on this site are copyrighted ©.