2018-04-07 17:17:00

Papa anawashauri Chama cha Mapadre wa Prado kuongea juu ya Yesu Kristo!


Tarehe 7 Aprili 2018  Papa Francisko amekutana na Jumuiya ya familia ya mapadre wa Prado kutoka Ufaransa, katika Ukumbi wa mkutano mjini Vatican Papa Francisko anasema: Hata nyakati zetu,zinatambua umaskini wake ambao ni wa zamani na mpya kwa mfano wa mwanzilishi wao Padre Chevrier! Kwa maana hiyo  Papa aliekendela na hotuba yake, anawatia moyo ili waweze kwenda mbele zaidi kujikita katika matendo yao ya kichungaji kwa mujibu wa karama ya Shirika lao, pia anathibitisha kuwa  karama yao ina mgusa kwa namna ya pekee yeye binafsi , kwani  ndiyo moyo wa mabadiliko ya kimisionari ambayo Kanisa zima linaalikwa kutafuata; “upo muungano wa kina kati ya uinjilishaji na uhamasishaji wa kibinadamu ambao lazima uweze kueleweka na kuendelezwa katika matendo ya uinjilishaji”. Evangelii gaudium, 178).

Katika tukio la kutangazwa  Mwenye Heri Padre Chevrier Mwaka 1986 huko Lion Ufaransa, Mtakatifu Yohane Paulo II alikuwa amewapatia mapendekezo mbalimbali na wao wanafahamu vizuri ili kuweza kuwa na  nguvu katika utume wao, kwa njia hiyo, hata Papa anarudia kusisitiza mapendekezo hayo kwa kuchukua mojawapo, ya yale aliyo semwa.

Mtakatifu Yohane Paulo II aliwaomba kwamba wao waongee juu ya Yesu Kristo , kwa nguvu zile zile  na imani ya Padre Chevrer (…) kwani, Maskini wanayo haki ya kutangaziwa habari ya Yesu Kristo. Wanayo haki ya Injili na kupata  Injili kamili. (hotuba ya Mt. Yohane PauloII katika Tasisi ya Prado 7 Oktoba 1986). Papa Francisko anaongeza kusema, ni wazi kwamba  maskini wengi  wako tayari kujifungulia imani; wao wanahitaji Mungu, wana ukosefu wa umakini wa kiroho ambao wakati mwingine unaunda hali halisi ya ubaguzi, hivyo upendeleo wa maskini unapaswa kupewa kipaumbele zaidi na kutafsiriwa katika matendo ya dhati ya dini (Evengelii Gaudium, 200). 

Papa Francisko amerudia kuwaalika ili waweze kutazama  daima sura ya mwanzilishi wao na kutafakari maisha yake; wamwombe bila kuchoka. Uzoefu wa kiroho aliokuwa kuwa nao,kwani alijazwa upendo kwa maskini, uelewa na kushirikishana na mateso yao,  wakati huo huo  kwa kutafakari jinsi gani  Kristo ajivua kila kitu na kujifanya mmoja kama sisi!  Padre Chevrier alikuwa kama chem chem hai  ya kitume na ndiyo iwe safari yao ya kimisionari. Roho Mtakatifu awaangazie katika njia zao alizowaita watembee na  awape nguvu mbele ya changamoto na matatizo. Amekadhi wanachama hao  kwa maombezi ya Mwenye Heri Antoine Chevrer na kwa kusali kwa Mama Maria ili awaweke chini ya ulinzi wake wa umama na kuwabariki kwa baraka ya kitume.

Na Sr Angela Rwezaula.

Vatican News!

 
All the contents on this site are copyrighted ©.