2018-04-07 16:20:00

Papa akutana na Bi Henryane de Chaponay, mwanzilishi wa CEDAL


“Ninayo furaha ya kukutana nanyi asubuhi hii kuwasalimia na kuwashukuru kwa juhudi za huduma ya amani, utetezi wa haki za binadamu, ulinzi wa mazingira nyumba yetu na kusaidia kukua kwa jamii ya kibinadamu na kindugu”. Ni maneno yake Baba Mtakatifu aliyo anza nayo wakati alipokutana na  mjini Vatican na Bi Henryane de Chaponay, mwanzilishi wa Kituo cha mafunzo ya  maendeleo ya Amerika ya Kusini (CEDAL) .

Anatoa shukurani kwa  Bi Henryane de Chaponay kwa kujikita katika utume huo  na kama Mwanzilishi wa Kituo cha Mafunzo ya Maendeleo Amerika ya Kusini,pia kwa shughuli ya ubunifu wake ambao anasema umeonesha matunda kwa njia ya mazungumzo ya kibinadamu  kama vile mikutano ambayo ndiyo sura msingi wa kisiasa juu ya binadamu katika ujenzi wa uzalendo ambao unatunza nyumba ya pamoja.

Ni muhimu kutoa chachu na kuamsha sanaa ya kuishi pamoja kwa urahisi, kwa wema na undugu, kama vile  ilivyo kuelimisha utamaduni wa kuheshimu na makutano ambayo ni  nyenzo mbili msingi zenye uwezo wa kujenga wakati endelevu wa mawazo yaliyo ya juu ya binadamu.

Waraka wa sifa kwa Bwana  (Laudato Si ), ujumbe mbalimbali, kuitisha Sinodi ijayo ya Maaskofu wa Amazon, Papa anaongeza kusema, ni matashi yake kwamba historia ya binadamu inaweze kugeuka kuwa maua yanayo chanua uhuru, ukuaji, wokovu na upendo (Laudato si’, 79), kwa maana hiyo Papa ameonesha utambuzi wa ukarimu na jitihada zao katika shughuli hiyo. Anawaombea na kuwabariki kwa moyo wote!

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!

 
All the contents on this site are copyrighted ©.