2018-04-07 13:33:00

Askofu mkuu Paul F. Russell ateuliwa kuwa Balozi nchini Azerbaigian


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Paul Fitzpatrick Russell kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Azerbaigian na ataendelea kuwa Balozi wa Vatican nchini Uturuki na Turkmenistan. Askofu mkuu Paul Fitzpatrick Russell alizaliwa tarehe 2 Mei 1959 huko Greenfield, nchini Marekani. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapewa Daraja takatifu ya Upadre hapo tarehe 20 Juni 1987. Tarehe 19 Mei 2016 akateuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Balozi wa Vatican nchini Uturuki na Turkmenistan na hivyo kumpandisha hadhi na kuwa ni Askofu mkuu na hatimaye, kuwekwa wakfu hapo tarehe 3 Juni 2016. Baba Mtakatifu Francisko amemwongongezea majukumu na sasa atakuwa pia ni Balozi wa Vatican nchini Azerbaigian.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Vatican News.
All the contents on this site are copyrighted ©.