2018-04-06 10:42:00

Ujumbe wa Papa kwa washiriki wa Wiki ya 47 ya Taasisi za Maisha ya kitawa


Baba Mtakatifu Francisko ametuma ujumbe kwa njia ya video kwa washiriki wa Mkutano wa wiki ya kitaifa nchini Hispania kwa ajili ya mashirika ya kitawa. Katika ujumbe huo aliomtumia Padre Carlos Martínez Oliveras, Mkurugenzi wa Taasisi ya Taalimungu ya Maisha ya kitawa huko Madrid na kwa zaidi ya washiriki 700 katika wiki ya 47 ya kitaifa  ya Taasisi za maisha ya kitawa, iliyofunguliwa mchana Alhamisi, tarehe 5 Aprili 2018 Papa Francisko anasema: wasiwasi wangu mkubwa ni kwamba vijana wetu wanapoteza mizizi. Nina hofu hiyo! Labda kazi iliyopo leo hii ni kuandaa hatua za safari, ili waweze kuona tangazo  la Nabii Yoeli aliyetabiri kuwa: “wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono”, (J2,28).

Katika ujumbe huo Papa anaendelea kutafakari kwa kina kutazama hata juu ya ukosefu wa miito, japokuwa anasisitiza kwamba, hawawezi kusimama tu na kuendelea kulalamika, kwa kusikiliza muziki wa kichichini ambao unajutia sifa na utukufu uliopita, wakati Bwana bado anaendelea kusema: Tazama mbele ni kitu gani unaweza kutenda. Lakini pamoja na hayo, Papa anawapa onyo ili wasije kugeuka watu wa kulazimisha uongofu. Na kinyume chake anasema: ni lazima kutafuta mtindo wa kufungua njia mpya ili Bwana aweze kuita miito. Zaidi ya hayo pia anasisitiza kuwa:  haisadii kufanya kama wafanyavyo kampeni za uchaguzi, hata kampeni za aina nyingine za kibiashara, kwasababu wito wa Bwana haungiliani na  mitindo ya matangazo ya  kibiashara  (marketing). Wito ni jambo jingine tofauti, kwa maana hiyo anawataka wawe wajasiri na kwenda mbele!

Akiwatazama vijana kwa karibu Papa Francisko amegusia juu ya tafsiriya  Kijerumani ya kitabu cha mwisho cha mwandishi, Zygmunt Bauman (ambacho tayari hata kwa lugha ya kiitaliano kwa jina la kitabu: “wamezaliwa maji”, lakini tafsiri ya kijerumani: Die Entwurzelten maana yake: “Isiyo na mizizi”. Papa akitafakari juu yake anasema: “ tupo katika kipindi cha kurudi kutafuta mizizi tena. Lakini hata hivyo tupo hata katika kipindi cha kuweza kuwafanya wote waote  ndoto wanaume na wanawake, ili baadaye waweza kurithisha vijana uwezo wa kutoa unabii. Leo hii na zaidi, ni lazima vijana wawe na mazungumzo na wazee. Kwa maana ya mazungumzo kati ya babu na wajukuu zao ni mazungumzo ya kizazi hata kizazi kwa ngazi ya juu. Bado upo wakati ambao usipotezwe wakati huo. Kutokana na hilo, Papa anashauri kutafuta njia za kusikiliza mahangaiko ya vijana, hata ya wazee. Wote wawekwe pamoja na ndipo  kila kitu kitakwenda vizuri anabainisha. Na kwa upande wa idadi ya miito, Papa amehitimisha akisema hayo ni mapenzi ya Bwana, la muhimu ni kufanya kile anacho agiza kwanza yaani kusali na kutoa ushuhuda!

Katika wiki ya 47 ya kitaifa kwa ajili ya Taasisi za maisha ya kitawa, mkutano huo umeanza tarehe 5 na utamalizika 8 Aprili 2108 unaofanyika katika Chama cha Mwenye heri Paulo VI (Fundación Pablo VI) katika mji Madrid Uhispania. Unaongozwa na mada: “Ninawaita wale ninaowapenda. Vijana,mang’amuzi na maisha ya kitawa”. Lengo kuu la kufanyika mkutano huo limeandaliwa na Taasisi ya Taalimungu Madrid, katika mtazamio wa Sinodo ijayo ya Maaskofu itakayojikita kutafakari, vijana, imani na mang’amuzi ya miito. 

Na kati ya viongozi wakuu wa dini wanao udhuria wiki hiyo ni Kardinali Osoro Sierra askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Madrid na Óscar Rodríguez Maradiaga, Askofu Mkuu wa Honduras, ambaye ni Mkuu wa Baraza la Makardinali Washauri wa Papa. Ni kiungo cha makardinali 9 kilichoanzishwa na Baba Mtakatifu Francisko terehe 28 Septemba 2013, kwa lengo la kumsaidia Baba Mtakatifu katika Utawala wa  Kanisa zima la Ulimwengu na kufanya marekebisho ya rasmi ya Katiba ya Kitume Vatican.  Pia Askofu Mkuu José Rodríguez Carballo, ambaye ni  katibu mkuu wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Mashirika ya kitawa na Taasisi za maisha ya kitume pamoja na frateli Alois wa  Taizé Mkuu wa Jumuiya ya Kiekumene ya Taize nchini Ufaransa.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!
All the contents on this site are copyrighted ©.