2018-04-06 16:00:00

Nia za Maombi ya Papa kwa nwezi Aprili:Tuombee wenye masuala ya kiuchumi


Kama kawaida ya kila mwezi, Baba Mtakatifu  Francisko kutoa ujumbe kwa njia ya Video, hata kwa  mwezi Aprili 2018, nia ya maombi yake ya kitume imewaendea wahusika wote katika  masuala ya kiuchumi.

Kwa maana hiyo, katika ujumbe wa mwezi  wa nne kwa njia ya Video, Papa Francisko anasema kwamba, uchumi hauwezi kutegemea kuongezeka kwa ushuru na kupunguza masoko ya ajira, yanayosababisha kuunda aina nyingi za ubaguzi mpya. Ni lazima kufuata njia ya wafanya kazi, wanasiasa, watafiti na wadau wote wa kijamii ili wawe mstari wa mbele kama binadamu na kufanya kila liwezekanalo katika kuhakikisha kwamba zinapatikana  fursa za ajira yenye hadhi!

Akihitimisha maombi yake kwa njia ya video, Papa  anawaalika watu  wote kupaza sauti zao kwa pamoja, ili wahusika wa mawazo ya ubunifu na wanao jikita katika  masuala ya kiuchumi, wawe na ujasiri wa kukataa uchumi wa kupendelea na kubagua na kwa njia hiyo  waweze kutambua namna ya  kufungua njia mpya.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!

 

 
All the contents on this site are copyrighted ©.