2018-04-05 17:00:00

Wosia wa kitume: Furahini na kushangilia kuzinduliwa, 9 Aprili 2018


Ofisi ya habari ya Vatican imetoa taarifa kwamba, Jumatatu 9 Aprili 2018 saa sita na robo, katika Ofisi ya Habari Vatican utafanyika mkutano wa kuwasilisha Wosia wa Kitume wa Papa Francisko “Furahini na kushangilia, (Gaudete et exsultate), unaohusu Wito wa Utakatifu katika  dunia ya leo.
Watakao toa neno wakati wa uwasilishaji wa Wosia  wa Kitume wa Baba Mtakatifu Francisko, atakuwa ni Askofu Mkuu Angelo di Donatis, Makamu Askofu Jimbo kuu la Roma, Gianni Valente mwandishi wa habari na Paola Bignardi wa Chama cha kitume cha  Vijana Katoliki 

Kuhusiana na suala la wito wa Utakatifa katika dunia, ikumbukwe nkwamba  Baba Mtakatifu Francisko amekuwa akikumbusha mara nyingi ya kuwa "watakatifu siyo mashujaa wa kufikirika tu bali ni watu wenye furaha" ! Na hivyo  Wosia huu wa (Gaudete et exsultate), Furahini na kushangilia utakuwa ni Wosia  wa kitume wa tatu kutiwa saini na Papa Francisko mara baada ya Wosia  wa Kitume wa Amoris Laetitia, unao husu Furaha ya upendo ndani ya familia, ambao ulitolewa tarehe 19 Machi 2016 na Furaha ya Injili  (Evangelii gaudium) unaohusu kutangaza Injili katika ulimwengu wa sasa, ambao ulitolewa mnamo tarehe 24 Novemba 2013. Wakati huo inafuata nyaraka mbili kuhusu:Waraka wa Kitume "Utunzaji wa Mazingira (Laudato Si) uliotolewa tarehe 24 Mei 2015 na Waraka wa Kitume  "Mwanga wa Waamini ( Lumen Fidei)  uliotolewa mnamo tarehe 29 Juni 2013.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News

 
All the contents on this site are copyrighted ©.