2018-04-05 16:06:00

Papa amekutana na Rais wa Jamhuri ya nchi ya Armenia Bwana Sargsyan


Tarehe 5 Aprili 2018 Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Rais wa Jamhuri ya nchi ya Armenia Bwana, Serzh Sargsyan, ambaye baadaye amekutana na Katibu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin, akisindikizwa Askofu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican.

Katika mazungumzo yao na salam, wameonesha uhusiano mwema uliopo kati ya nchi hizi mbili, Vatican na Armenia. Wamezungumzia  juu ya sanamu ya Mtakatifu Gregori wa Narek Mwalimu wa Kanisa , ambayo imezinduliwa tarehe 5 Aprili katika Bustan za Vatican ili kuhamasisha kwa nguvu zaidi  za mahusiano ambayo pia ni kati ya Kanisa la kitume nchini Armenia na Kanisa Katoliki.

Halikadhalika,mazungumzo pia wamegusia mantiki za kisiasa inayohusu kanda na kutakiana mema ya kuweza kupata mwafaka katika hali halisi ya migogoro. Vilevile mada nyingine za kisiasa zimegusiwa kwa upande wa kimataifa, na zile zinazohusu  wakristo na madhehebu magomadogo, hasa katika nchi zenye vita.

Kuhusiana na maadhimisho ya uzinduzi wa sanamu ya Mtakatifu Gregori wa Narek iliyfanyika, taarifa kamili ni kwamba  imedumu kwa dakika 15 hivi  katika Bustani za Vatican. Ameyathibitisha hayo mwanahabari Pool aliyechaguliwa kufuatilia tukio hilo. Kwa njia hiyo athibitisha kuwa: Mbele ya sanamu, waliweka jukwaa kwa ajili ya viongozi wakuu ikiwa na maana: Papa, Karekin II na Aram I, ambao walikuwa  wamekutana nao dakika chache kabla ya maadhimisho mafupi hayo,Patriaki Katoliki wa Cilicia,Bedros XX, na Makardinali Koch na Sandri. Aidha viti vingine vya wakuu mbele ikiwa cha  Rais wa nchi ya Armenia Serzh Sargsyan na Karidinali Giuseppe Bertello Mkuu Tawala wa mji wa Vatican.  Nyuma yao alikuwa, ni  Monsinyo Georg Gaenswein, Mwenyekiti wa  nyumba ya Papa na Askofu Marini Mwalimu wa maadhimisho ya Liturujia za Papa.

Wakati wa maadhimisho Baba Mtakatifu amesali kwa lugha ya kiitaliano, wakati Aram kwa lugha ya kingereza na Karen lugha ya kiarmenia. Baada ya ishara ya msalaba, limefuatia somo la Injili kutoka Mtakatifu Yohane na baadhi ya tafakari ya Mtakatifu Gregori wa Narek, na mwisho kulikuwa na maombi, lakini mara baada ya kusomwa Injili walifunua rasmi  Sanamu ya Mtakatifu Gregori wa Narek. Baada ya kumalizia na kufunga maadhimisho hayo, Baba Mtakatifu ameweza kusimama dakika chache kuzungumza  na mchonga wa sanamu hiyo. 

Hata hivyo Papa pia amewapokea na kuzungumza na Patriaki Karekin II e Aram I: Mara baada ya Papa Kukutana na kuzungumza na Rais wa nchi hiyo , amekutana Patriaki Karekin II Mkuuwa warmenia wote. Ambapo mkutano ulikuwa wa faraga akiwa na mtafisiri mmoja tu. Wakati huo baada ya mazungumzo yao, Patriaki Karekin amemzawadia Papa Francisko kitabu cha Monasteri ya Narek na akamwambia Papa: “Monasteri hii haipo tena, kwa maana imeharibiwa nchini Uturuki”. Na Papa amemzawadia Karekin na baadaye Aram msalaba wa jiwe ukiwa unawakilisha Kanisa la Sistina uliochongwa juu yake. Zaidi pia amewapatia  vitabu vya vya Waraka wa Injili ya furaha (Evangelii gaudium), Amoris Laetitia na Laudato Si. 

Baada ya kumaliza mazungumzo na Karekin amekwenda katika chumba cha vitabu kwa faragha na Papa Aram I , Catholicos wa Kanisa la Kitume la Armenia huko Cilicia, mkutano ulikuwa ni mfupi kutokana na muda kuwatupa mkono. Papa Aram amemtakia hali kwa lugha ya kingereza na Papa Francisko akajibu ni nzuri, aidha meuliza juu ya afya yake, lakini naye akajibu kuwa ni nzuri sana.VilevilePapa ameongeza kusema, “ leo ni siku kubwa kwa ajili ya Armenia”.  Baadaye Papa Arm I amemzawadia hata Papa msalaba wa dhahabu, ambao  ni ishara ya watu wa Armenia amesema. Naye Papa ameubusi , kama vile alivyofanya Aram I wakati alipopewa zawadi kutoka kwa Papa.

Sr Angela Rwezaula
Vatican News
All the contents on this site are copyrighted ©.