2018-04-04 16:08:00

Papa amemteua Askofu wa Jimbo la Ilorin Nigeria, Paul A. Olawoore


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu wa Jimbo la Ilorin nchini Nigeria, mteule Padre Paul Adegboyega Olawoore wa Jimbo la Oyo, ambaye wakati wa uteuzi walikuwa ni Vika katika Mahakama ya Kanisa na Paroko wa Parokia ya Mama yetu wa Lourdes, Ogbomoso na dekano wa jimbo la Oyo. Askofu Mteule Paul Adegboyega Olawoore alizaliwa tarehe 30 Novemba 1961 Ikuri, katika Jimbo la Oyo.  Mafunzo ya falsafa na taalimungu katika Seminari  watakatifu Petro na Paulo huko Bodiga , Ibadan. Alipata daraja Takatifu ya Upadre Tarehe 3 Oktoba 1992 katika jimbo la Oyo.

Baada ya kupadrishwa ameshika nyadhifa mbalimbali kama vile1992–1993: kuhudumia Parokia ya Mtakatifu Mariahuko Ilesa;1993–1994: Kuhudumia Parokia ya Mtakatifu Petro na Paulo huko Ile-Ife;1993–2000: Katibu wa Askofu Julius Adelakun, Jimboni Oyo; 1996 – 2000: Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Bernardine, huko Oyo; 2000 – 2001: Paroko wa Mtakatifu Maria Magdalene, huko Tede; 2001 – 2003:Mafunzo kwa ajili ya sheria katika Chuo Kikuu cha Kipapa, Urbaniana Roma; 2003- 2011, Mkurugenzi wa Taasisi ya Mtakatifu Francis; Tangu 2003:alikuwa ni mwana sheria  vika mkuu wa mahakama Katoliki ya Jimbo Oyo; 2005–2011:  Dekano wa Jimbo la Oyo; tangu  2006:Mkurugenzi wa Tume ya Familia Jimboni na tangu  2011:Paroko wa Parokia ya Mama Yetu wa Lourdes  Ogbomoso, na Mkurugenzi wa Mafunzo ya Lugha katika  Shule katoliki ya Ogbomoso.

Sr Angela Rwezaula

Vatican Niews!

 

 
All the contents on this site are copyrighted ©.