2018-04-03 16:48:00

Mt. Yohane Paulo II, bado ni mfano wa kuigwa kwa watu wengi!


“Mtakatifu Yohane Paulo II hakosi kuigwa mfano , kuongoza  na kutupatia ujasiri”. Hayo ni maneno kwa mujibu wa  Kardinali Stanisław Dziwisz,tarehe 2, Aprili 2018  katika Madhabahu ya  Mtakatifu Yohane Paulo II mjini Krakow, wakati wa kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 13 tangu kifo chake (Karol Wojtyla),kilichotokea tarehe 2 Aprili 2005 mjini Vatican saa 3.37 masaa ya Ulaya. Kardinali Dziwisz ambaye ni Askofu Mkuu wa Jimbo la Krakow na ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Karol Wojtyła, amewauliza swali juu ya kitu gani leo hii wanaweza kusoma  katika kitabu cha maisha ya Yohane Paulo II ambaye aliweza kukifunga tarehe 2 Aprili 2005 , lakini kitabu hicho kubaki wazi kwa Kanisa na ulimwengu?

Akianza kufafanua,h ata hivyo amefikiria maisha yake na kwa kujibu swali hilo  Kardinali Dziwisz amesisitiza jinsi gani kwa upande wake Mungu alikuwa ndiyo kiini cha maisha hasa kama msingi mkuu na jiwe msingi pia mtazamo wake katika uso wa Yesu Kristo.  Akifafanua juu ya kitabu cha maisha ya Mtakatifu Yohane Paulo II anasema, inawezekana kukisoma kwa njia ya  kukabiliana na binadamu. Kwa kila binadamu ambaye amekombolewa kwa damu ya Mkombozi.  Tabia ya maisha yake yalikuwa ni tabia ya huduma na umakini, kuwa mfano wa hai kwa waamini. Papa Yohane Paulo II alikuwa anaamini kwamba binadamu ni njia ya Kanisa na zaidi alikuwa anatatia moyo kwa Kanisa ili kuweza kuhudumia binadamu huyo; kwa kuhamasisha  juu ya utunzaji wa kila maisha kuanzia kutungwa kwa mimba na kulinda; aliwalitia moyo wachungaji wa masuala ya vijana na familia, kusaidia wagonjwa na watu wasio jiweza ikiwa pia wazee.

Askofu Mkuu pia amebainisha zaidi katika kutambua kusoma kitabu cha maisha cha Yohane Paulo II, ya kwamba lazima kuwa na mtazamo wa upendo kwa Kanisa. Upendo kwa Kanisa hauna maana ya wazo tu la kufikirika, bali ni Kanisa ambalo linaundwa na watu wadhaifu na wadhambi; watu ambao wako katika njia ya wongofu na ambao wanarudi katika njia zilizoelekezwa na Injili. Yohane Paulo II kwa hekima yake aliongoza jumuiya kubwa ya Kanisa kwa lugha zake, ikijieleza kwa imani katika mantiki za utamaduni na utamadunisho tofauti. Katika moyo wake wa kichungaji kulikuwa na nafasi yak ila mmoja. Yohane Paulo II  alianzisha katika Kanisa Milenia ya Tatu kwa imani ya kristo na kuwatia moyo wote ili kutazama zaidi uso wa Yesu, aliye mmoja peke yake  na mwokozi wa ulimwengu; ambaye anawaalika katazama makuu ya imani, matumaini na chachu ili kuweza kugeuka upendo katika dunia iliyochanganyikiwa! 

Kwa kutazama mantiki ya jumuiya ya kimatifa, Kardinali amesema Kitabu cha maisha cha Yohane Paulo II kinaweza kusomeka kwa maana ya uwajibikaji wa dunia. Hii ina maana ya kwamba aliweza kuona wema badala ya ubaya katika dunia, si kwamba hakuona ubinafsi, mivutano na migogoro, la hasha  , havikupmta pembeni lakini. Alikuwa akijaribu kutafuta zaidi mazungumzo kwa wote, hasa hawalio na madataka , wanaowajibika kuanzia viongozi wa kidini na ambapo waongozwe na sababu za kweli. Alipokea viongozi wakubwa madhehebu duniani na kuwaalika wasali kwa ajili ya amani. Si rahisi pia  kusahau mchango mkubwa wa Papa Yohane Paulo II wa  kukumboa watu wa Ulaya ya Kati na Mashariki chini ya utawala wa udikteta.

Kardinali amehitimisha kwa kushukuru Bwana kwa zawadi ya Mtakatifu na  Mchungaji Yohane Paulo II, ambaye aliweza kuwa zawadi kwa  Kanisa na kwa ajili ya ulimwengu mzima , pia zawadi ya kila mmoja. Na kwa kusoma kitabu cha maisha ya Mtakatifu Yohane Paulo II, kila mmoja aweze kuiga na kuwa na shauku ya kujifanya zawadi kwa ajili ya wengine. Na Kristo aliyefufuka azidishe nguvu za kutangaza kwa furaha Injili kwa wote ambo wanakutana nao katika safari ya Maisha.

TUKUMBUKE HAYA:

Mtakatifu Yohane Paulo II alifariki tarehe 2 Aprili 2005 saa 3.37 za Usiku masaa ya Ulaya. Kwa miaka 26 ya utawala wake alifanya ziara za kitume 102 kimataifa na 142 nchini Italia.  Aliweza kutoa hotuba na mahubiri  3,000, aliandika Wosia 14wa kitume  na nyaraka za kitume 14, Katiba 14 na Barua za kutume 42.  Mtakatifu Yohane Paulo II kabla ya kuchaguliwa kuwa Papa, kwa miaka 20 amekuwa katika Baraza la Maaskofu Katoliki wa Poland , mwanzo alikuwa askofu Msaidizi wa Jimbo la Krakow  (1958-1964), baadaye Askofu Mkuu wa Krakow (1964-1978). Mwaka 1967 aliteuliwa kuwa Kardinali. Wakati wa huduma ya kichungaji nchini Poland aliweza kushika nyadhifa mbalimbali kama vile, kuwa Mwenyekiti wa Braza la Maaskofu Katoliki Poland (1969-1978). 

Na Sr. Angela Rwezaula 
Vatican News
All the contents on this site are copyrighted ©.