2018-04-03 15:38:00

Katika Bustani za Vatican itabarikiwa sanamu ya Mt. Gregori wa Narek!


Tarehe 5 Aprili 2018 katika Bustani za Vatican, Baba Mtakatifu Francisko ataongoza sherehe na kubariki Sanamu ya Mtakatifu Gregori wa Narek iliyowekwa katika bustani za  mji wa Vatican. Sherehe hizo zitaudhuriwa na Kiongozi wa Kanisa Katoliki katika  nchi ya Armenia, Krikor Bedros XX, pia Rais wa nchi hiyo, Serzh Sargsyan, aidha Patriaki wa kiorthodox KAREKIN II na waarmeni katika Makao ya Vatican huko Etchmiadzin, na Patriaki ARAM I. Sanamu hiyo imechongwa na David Erevanci wa nchi ya Armenia ambayo ilitengenezwa kwa mujibu wa Rais wa Jamhuri ya nchi ya Armenia, Bwana Serzh Sargsyan, sanamu hiyo alizwadiwa Papa Francisko wakati wa ziara yake ya kitume nchini humo mnamo Juni 2016.

Ilikuwa tarehe 12 Aprili 2015 katika fursa ya Misa iliyo adhimishwa na Papa Francisko katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, kwa kukumbukumbu ya milioni moja na nusu ya wafia dini wa nchi ya Armenia, Mtakatifu Gregori wa Narek alitangazwa kwa hadhi ya kuwa Mwalimu wa Kanisa ulimwenguni. Tukio hilo lilitoa fursa ya pekee na  ilikuwa ni moja ya roho ya kiekumene kati ya makanisa mawili, ambapo kwa mara ya kwanza walikuwa wameunganika viongozi wa makanisa ya ya Kiorothodox ya Kiarmenia pamoja na Papa wa Roma.

Kwa upande wa sanamu ina urefu wa mita mbili, na iliwakilisha Mtakatifu Gregori akiwa anatazama juu mbinguni, kama ishara ya kuwakilisha pia mtindo wa  makanisa ya nchi ya Armenia pamoja na ti wa mkomamanga likiwa ni ishara ya watu wa nchi ya Armenia. Hata hivyo wataweza kutengeza pia sanamu ya pili inayofanana kama hiyo ya  Mtakatifu Gregori wa Narek ili mwishoni mwa mwaka huu  2018 iweze kusimikwa katika bustani ya Echmiadzin nchini Armenia.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!
All the contents on this site are copyrighted ©.