2018-04-02 16:56:00

Tarehe 2 Aprili 2005, Mtakatifu Yohane Paulo II aliitwa na Mungu!


Tarehe 2 Aprili 2005 Mtakatifu Yohane Paulo II aliaga dunia. Aliwaachia simanzi kubwa waamini wengi na lakini pia shukrani kubwa kwa ajili ya Papa huyo Wojtyła ambaye alipendwa na watu wengi duniani hadi kuweza kufika kwa wingi mjini Vatican ili kutoa salam zao mwisho. Ilikuwa ni saa 3.27 za usiku masaa ya Ulaya, tarehe 2 Aprili 2005,  kwa maana hiyo ni miaka 13 iliyopita, Mtakatafu Yohane Paulo II aliaga dunia!. Kwa masaa machache maelfu na maelfu ya waamni walikusanyika katika viwanja vya Mtakatifu Petro wakisali  Rosari. Na Milioni 7 ya mahujaji walifika Roma kwa ajili ya maombolezo na maziko ya Papa  Karol Wojtyła!

Uchungu mkubwa pamoja na shukrani kubwa bado vinakumbukwa katika  siku ile kwa waamini walio wengi , lakini hata pia imani ya kina kwa wale waliomsalimia kwa mara ya kwanza alipochaguliwa tarehe 16 Oktoba 1978 na kusikia sauti yake akiwambia kuwa makardinali wamemchagua kutoka mbali.

Siku alipoaga dunia, aliyetoa tangaza la kifo chake wakati ule, alikuwa ni Kardinali Leonardi Sandri,wakati ule alikuwa ni Katibu wa Vatican na kwa sasa ni Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki.  Siku zilizofuata,msululu mkubwa wa watu kutoka duniani kote waliweza kufika  ili kutoa heshima ya mwisho katika geneza la Papa Yohane Paulo II ambaye kabla ya kutimia  miaka 10alitangazwa  kuwa Mtakatifu, mnamo tarehe 27 April 2014.

Itakumbukwa Misa ya  maziko iliadhimishwa tarehe 8 Aprili 2005 na Kardinali Joseph  Ratzinger, aliyekuwa Dekano wa Makardinali wakati ule. Lakini baada ya siku chache akachaguliwa yeye mwenyewe kuwa Papa kwa kuchagua jina la Benedikto XVI. Na kwa njia hiyo Tarehe 2 Aprili 2018 ni siku ya kumbukumbu ya kifo cha Mtakatifu Yohane Paulo II, tumwombe atuombee ili tupate neemana kuweza  kuiga mfano wake wa kupenda mateso, vijana , familia na ushuhuda wa kweli katika Kristo Yesu.

Na  Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!

 








All the contents on this site are copyrighted ©.