2018-04-02 15:33:00

Papa Francisko anawaombea wote hasa waliotekwa nyara ili warudi makwao!


Ili kutosahau yale ambayo walikuwa wakisema wakristo wa kwanza:“ Bwana amefufuka kweli kweli.  Nasi tutamke mara moja zaidi: Bwana amefufuka Kweli kweli ”. Asante. Ni maneno ya kwanza ya Papa Francisko aliyotamka mara baada ya tafakari neno la Mungu  siku ya  Jumatatu ya Pasaka tarehe 2 Aprili 2018, wakati kutoa salam zake mara baada ya sala malkia wa Mbingu kwa mahujaji wote toka pande za dunia waliofika katika viwanja vya Mtakatifu Patro kuungana na sala hiyo muhimu ya Kanisa.

Akiendelea anasema; katika kipindi hiki cha Pasaka anapenda  kutoa  salamu za upendo kwa wote, familia na makundi ya parokia, vyama na mahujaji wengine binafsi waliotoka Italia na sehemu mbalimbali za dunia. Kwa kila mmoja anamtakia mema ili aweze kusheherekee kwa utulivu wa siku hizi nane kuu za Pasaka , ambapo kipindi kinelendeza na tabia hiyo ya furaha ya ufufuko wa Kristo. Wapokee kila fursa kwa ajili ya kushuhudia amani ya Nwana Mfufuka, zaidi kwa watu ambao ni wadhaifu na wasio kuwa na bahati. 

Kufuatia na suala la wadhaifu, Papa Francisko amepata fursa ya kukumbuka na kuwakikishia maombi yake kwa Mungu,watu wote wenye matatizo ya (autism). Papa Francisko anawaomba pia wasali kwa ajili ya zawadi ya amani duniani kote na  hasa kwa ajili ya watu wote wanateseka kwasababu ya migogoro iliyoko sasa. Amerudia pia  kutoa wito ili watu wote waliotekwa nyara bila hatia na ukosefu wa huru waweze kuachiwa na kurudi majumbani kwao. Amemalizia akiwatakia matashi mema ya Jumatatu ya Malaika na kuowaomba wamkumbuke katika sala zao.

Je Autism ni nini? Ni ugonjwa wa watu kukosa uhusiano na wengine katika ulimwengu, mtu kuishi nje ya kinachojikeza karibu yake, bali kuwa na ulimwengu wake. Na hivyo ni ugonjwa utokanao na ukosefu wa maendeleo ya ujenzi wa mahusiano ya nje ya  kijamii na upendo, matatizo ya ukosefu wa kuzungumza,au  kurudia rudia maneno na michezo hiyo hiyo;ugumu wa kutembea akiwa mtoto, hata wakati mwingine kutumia nguvu na kupiga kelele kwa nguvu. Dalili hizi zinajitokeza awali katika utoto na kuendelea. Na kwa njia hiyo kila tarehe 2 Aprili ya kila nwaka ni Siku  ya dunia ya kuwakumbuka watu wote wanaoteseka na ugonjwa huo, kwa kingereza  unaitwa ( Autism).

Na Sr Angela Rwezaula

Vatican News

 
All the contents on this site are copyrighted ©.