2018-03-30 16:46:00

Maneno ya Papa Francisko kuhusu jehanamu na huruma inayoleta wovu!


Wakati tunapojiandaa kwa siku hizi tatu Kuu kabla ya Sikukuu ya Pasaka, mwandishi wa habari wa Radio Vatican amejaribu kutafuta  tafakari ya Papa Francisko kuhusiana suala la Jehanamu hasa kujikita katika tafakari za Baba Mtakatifu Francisko kwa miaka hii tangu aanze utume wake kwa mada ya  “Maneno ya Papa Francisko kuhusu jehanamu: huruma inayooka: lakini kitu gani?" Papa akianza kuelezea maana ya Pasaka: Pasaka ni Sikukuu muhimu ya imani yetu kwasababu ni Pasaka ya wokovu; sikukuu ya upendo wa Mungu kwa ajili yetu. (Haya ni baadhi ya maneno ambayo Papa Francisko ameeleza katika Katekesi yake ya Jumatano tarehe 28 Machi 2018,ikiwa ni  katekesi iliyojikita kutafakari siku tatu Kuu  kabla ya Pasaka. na kuongeza kuuliza je wokovu wa kitu gani?

Kifo, hukumu, jehanamu na peponi: Moja ya ibada ya misa ya tarehe 22 Novemba 2016 katika Kanisa la Mtakatifu Marta Mjini Vatican, Papa alithibitisha kuwa dunia haitaki kufikiria siku za mwisho. Je kuna nini mara baada ya maisha haya? Yeye binafsi alikumbuka wakati alipokuwa mtoto anakwenda katekisimu ya kwamba waliwafundishwa mambo manne kuhusu kifo, hukumu, jehanamu na peponi. Akaongeza na kusisitiza  kuwa, haya  mambo yanaweza kumwogopesha mtu lakini ni ukweli. Iwapo wewe huchunguzi mwoyo wako, ili Bwana apate kuwa nawe  karibu na ukaendelea ukaishi mbali na Bwana daima, na ndipo hapo labda kuna hatari  ya kuendelea kuwa mbali na umilele wa Bwana!

Jehahamu siyo  chumba cha adhabu: Halikadhalika katika misa nyingine ya tarehe 25 Novemba 2016,  katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican Papa alirudia tena kuthibitisha kuwa “Jehanamu siyo chumba cha adhabu, bali ni mahali pa kuwa mbali daima na Mungu ambaye anatupatia  furaha, ni mahali pa kuwa mbali na Mungu anayetupenda sana! Huruma ya Mungu inatuokoa na uaharibifu wa milele; kama ilivyojitokeza kwa mhalifu juu ya msalaba, ambaye kwa dakika za mwisho wa maisha yake aliweza kumkabidhi Yesu na kumwambia amkumbuke wakati atakapoingia katika ufalme wake na Yesu alisikika akitamka “Nakuambia kwa hakika leo utakuwa nami peponi”.

Shetani ni jehanamu: Papa Francisko akigusia juu ya jehanamu ni shetani anasema : “hakuna anayekupeleka jehanamu  kwasababu unakwenda wewe mwenyewe na unachagua kuwapo kule. Jehanamu ni kutaka kwenda mbali na Mungu, kwasababu ya kukataa upendo wake. Na  shetani ni jehanamu kwasababu yeye alipendelea hivyo na ndiye mojawapo tuliye na uhakika kwamba ni jehanamu”. (Hayo aliyatamka wakati wa ziara yake ya kitume katika parokia moja ya Roma ya Mtakatifu Maria Mama wa Mwokozi wakati wa kukutana na watoto na vijana tarehe 8Machi 2015).

Na hukumu ya mwisho Papa anathibitisha kuwa: “mwisho wa maisha yetu wote tutahukumiwa”, lakini hukumu yetu ya mwisho itahusiana  juu ya pendo, kama Yesu mwenyewe asemavyo: “kwa maana nilikuwa na njaa nanyi mkanipa chakula”. Bwana anatupatia mara nyingi fursa za uongofu na kuingia katika mlango wa wokovu. Papa anathibitisha hilo: “Bwana hachoki kutusamehe na kutusubiri hadi mwisho pamoja na dhambi zetu tulizo nazo! Na hiyo ndiyo huruma yake. Licha ya hayo yote lakini sisi tunao uhuru wa kukubali au  kukataa, lakini kukataa maana yake ni ufisadi; kwa maana ni mwenye dhambi ambaye hataki kuungama na ambaye anakataa upendo wa Mungu”. (Aliyasema Papa Francisko wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana tarehe  21 Agosti 2016)

Wokovu wa milele: Akitafakari juu ya Wolovu wa Milele: Papa anauliza: Iwapo Mungu ni mwema na anatupenda , kwanini wakati mwingine tunafunga milango? Na katika maisha yetu siyo mchezo katika video au tamthiliya; maisha yetu ni ya dhati  na lenye  lengo la  muhimu la kufikia  yaani wokovu wa milele. (Ni uthibitisho wa Papa wakati wa tafakari ya Malaika wa Bwana tarehe  21Agosti 2016).

Bwana ni mwema: Papa Francisko anaonesha  suluhisha kuhusu hofu zetu tulizo nazo kwamba, iwapo kila mmoja ni mwaminifu kwa Bwana, wakati atakapokuja tutaweza kusema kama  Mtakatifu Francisko wa Azizi aliyeita kwamba “njoo  dada kifo”. Hakuna haja ya kuogopa!. Na hata siku ya hukumu tutamwona Bwana na kuweza kusema naye: Bwana ninazo dhambi nyingi, lakini nimetaka kuwa mwaminifu, Baba Mtakatiu anaogeza kusema: kwa kuwa Bwana ni mwema, hatutakuwa na hofu. (Haya aliyasema wakati wa misa katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatiican tarehe 22 Novemba2016).

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News”








All the contents on this site are copyrighted ©.