2018-03-09 15:50:00

Tarehe 12-13.3.2018:Mkutano juu ya haki msingi ya elimu na mafundisho!


Kuanzia tarehe 12-13 Machi 2018 katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Santa Croce, utafanyika mkutano wa Kitengo cha Sheria za Kanisa unao uhusu haki msingi ya elimu na mafundisho. Katika mkutano huo ni mada nyingi zitaguswa ambazo zimechaguliwa na  kitengo cha Sheria ya Kanisa kwa kukusudia juu ya mada ya Haki ya Elimu na Mafundisho. Pamoja na hayo taarifa inasema kuwa mada hizo ni: Elimu kama haki msingi ya binadamu na kitovu kinachojitegemea cha mafundisho ambayo yanalinda sheria Ulaya, mikakati ya fedha za shule msingi katika mataifa ya Ulaya, elimu ya wazalendo kama  jibu linalo wezekana katika utamaduni wa watu wengi, nafasi ya elimu ya wazazi, elimu ya nyumbani na changamoto zinazojitokeza kuhusu jinsia.

Lengo la mkutano huo ni kutaka kujikita kwa kina kutazama Haki ya Kaninsa wakati wa kueleza mafundisho katoliki na thamani ya binadamu inayosimamia juu ya sheria asili kwa njia ya msingi na mwelekeo wa shule yoyote ya maadili na yenye uwezo wa kuelezea. Kutokana na hiyo kutakuwapo na nfasi msingi kwa walimu wa Kanisa katika elimu na wenye taaluma ya kutosha kuchambua uhusiano kati ya haki sheria na Kanisa, kwa mtazamo wa haki msingi ya mafundisho hata utafiti ambao unawatazama waamini katika mantiki ya elimu ya sayansi ya Kanisa.

Mkutano huo utafunguliwa na Katibu wa Baraza la Elimu Katoliki Askofu Angelo Vincenzo Zani, wengine kati yao ni Jorge Otaduy (Universidad de Navarra), Alfred Fernández (Mkurugenzi wa  Oidel, Geneva), Vincenzo Turchi (Chuo Kikuu Salento Italia), Paolo Cavana (Lumsa), Emmanuel Tawil (Chuo Kikuu cha  Paris, II Panthéon-Assas), Alessandro Ferrari (Chuo Kikuu cha mafunzo ya Insubria), Paolo Asolan (Chuo Kikuu cha Kipapa Laterano ) na maprofesa wa Chuo Kikuu cha Kipapa Santa Croce Roma ,Stefan Mückl, Jean-Pierre Schouppe na José Tomás Martín de Agar. Aidha na wataalam wengine wengi  wa taaluma ya sheria  kutoka mataifa mbalimbali.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.