2018-03-05 14:49:00

Kitabu cha Kard.W.Kasper juu ya Ujumbe wa Amoris laetitia.Majadala kindugu!


Tarehe 4 Machi 2018 Kardinali Walter Kasper amefikisha miaka 85. Ni Mwenyekiti mstaafu wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya kuhamasisha umoja wa Wakristo na mtaalimungu maarufu kimataifa  kutoka Ujerumani.Tarehe 5 Machi  2018 akiwa na Askofu Mkuu Vincenzo mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Maisha, amewakilisha kitabu chake cha mwisho chenye kichwa cha habari “Ujumbe wa Amoris Laetitia ( Furaha ya upendo ndani ya Familia) “Majadiliano kidugu”.Kitabu ambacho kitapatikana katika maduka ya vitabu.

Kabla ya kuwasilisha kitabu hicho, Kardinali Walter Kasper amezungumza na Vatican News, kuhusiana na majadiliano ambayo yametokea kwenye Waraka wa Kitume wa Baba Mtakatifu Francisko  na matunda ya Amoris Laetitia, yaani furaha ya upendo ndani ya familia.  Katika sura za kwanza za kitabu chake amesisitiza juu ya furaha ya Upendo ndani ya familia kwamba, siyo mafundisho mapya, bali ni kurudia na kuendeleza kwa upya ule utamaduni, kwa sababu utamaduni siyo kama  Ziwa la maji yaliyo tuwama, bali ni ziwa  linalo bubujika maji yake katika mto na kwa maana hiyo  ni kitu hai kabisa. Na kwa njia hiyo ni kusema kuwa  Kanisa ni chomba hai ambacho kinapaswa daima kuwelewesha  zaidi na kutoa thamani yake ya utumaduni Katoliki wa hali ya sasa. Na hiyo ndiyo maana yake ya  kurudia hata usemi wa Papa Yohane wa XXIII!

Hali kadhalika katika kichwa cha habari sehemu ya pili imeandikwa “majadiliano kindugu”, Kardinali Kasper ameandika kuwa ni lazima kutokuwa na hofu ya kujadiliana lakini akiongeza kusema kuwa, hakuna nafasi ya kuhukumu wapinzani  kwa maana hiyo , kardianli  anataka hawali ya yote kueleza kuwa majadiliano katika Kanisa ni muhimu;japokuwa  ni lazima kutokuwa na hofu.  Anafafanua zaidi  kwamba,  kuna majadiliano ambayo ni makali na yenye nguvu ambayo yanashambulia wapinzani. Kwa kawaida upinzani ni tabia ambayo inapinga mafundisho yanatolewa. Lakini pamoja na hayo  Mafundisho juu ya kutengua hayawezi kuweka katika masuala ya Baba Myakatifu! Na hivyo kabla ya kunena lolote kuwa ni upinzani, ni lazima kujiuliza nini maana yake na uthibitisho huo. Zaidi Kardinali Kasper anathibitisha, ni lazima kutambua kuwa kama ni mkatoliki hawezi akawa tofauti au kutoa ushauri na malekezo tofauti.

Hata hivyo katika kuzungumza juu ya upinzani na mjadala  uliojitokeza katika kipengele cha 351 cha Furaha ya upendo (Amoris Laetitia), kinachohusu upokeaji wa sakrameti ya komunio kwa walio na talaka ya ndoa na kuolewa tena, katika kitabu hicho, Kardinali anathibitisha kuwa, kipengele hiki ni lazima kusomwa katika mwanga wa Waraka wa Mtaguso wa Trento uliokuwa unahusu Ekaristi. Hiyo ni kwasababu Mtaguso wa Trento unathibitisha kuwa, iwapo kesi ambayo siyo dhambi kubwa, lakini ya kawaida, Ekaristi takatifu ina uwezo wa kuondoa dhambi hiyo. 

Dhambi ni neno lenye ugumu wake kwa ujumla lakini pia  siyo sheria peke yake ya kitu, bali hata inahitaji umakini na dhamiri ya mtu, vilevile ni lazima kutazama undani wake kwa kina kwa njia ya  Sakramenti ya kitubio, kama ipo kweli dhambi kubwa au dhambi ndogo ya kawaida na hata labda hakuna chochote. Kama ni dhambi ya kawaida, mtu anaweza kuondolewa na kukubaliwa apokee sakramenti ya Ekaristi. Hii inakwenda sambamba tayari na mafundisho ya Mtakatifu Papa Yohane Paulo II na kwa maana hiyo, Baba Mtakatifu Francisko alichokifanya katika Waraka wa Amoris Laetita ni  kuendeleza  njia hiyo ambayo ilikuwa tayari imefunguliwa na mapapa waliotangulia. Kwa maana hiyo Kardinali Kasper anathibitisha kuwa haoni sababu ya kusema kuwa huo ni upinzani.

Msaada mkubwa wa Waraka wa Furaha ya upendo ndani familia ambao unaotolewa kwa familia  ya leo, ili kuweza kutambua vema na kuufanya kuishi waraka huo katika  matendo yao ya  maisha ya kila siku kwa wanandoa kwa mujibu wa Kardinali anasema: anatambaua baadhi ya Parokia mjini Roma ambao wanaunganika kwa pamoja ambao ni  wanandoa na wanaotarajia ndoa kuandaa ndoa yao.  Wanasoma baadhi ya vipengele vya Waraka huo na kutafakari kwa kina. Lugha ya waraka huo ni wazi kwa kila mkristo kuilewa. Ni lugha ambayo siyo ya hali ya juu  katika utaliimungu bali ni  lugha nyepesi ya  kutambuliwa na waamini rahisi na wenye mapenzi mema . watu wa Mungu walio wengi wanayo furaha na kuusoma ujumbe kwa sababu unatoa uwanja mpana katika uhuru  na kutafakari mambo muhimu ya ujumbe huo  wa kikristo na ujumbe rahisi, aidha wako pamoja upende wa Baba Mtakatifu Francisko!

Kardinali Kasper vilevile anamalizia akielezea juu ya umuhimu wa huruma ya Mungu ambayo tangu Baba Mtakatifu Franciko  aliposali sala ya kwanza ya  malaika katika viwnja vya Mtakatifu Petro  wa Bwana  alitaja kitabu chake wakisome ambacho kinaeleza juu ya huruma hasa kutazama huruma katika familia. Kardinali anathibitisha kuwa leo hii tunaishi kipindi cha vurugu katika ulimwengu. Watu wengi wamepata majeraha. Hata katika ndoa kuna majeraha mengi. Watu wengi wanahitaji huruma ili kuelewa na kutambuliwa na Kanisa katika nyakati hizi ngumu ambazo tunaishi. Na kwa maana hiyo huruma ndiyo jibu katika ishara za nyakati zetu!

 Sr Angela Rwezaula
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.