2018-03-02 14:42:00

Pd.Cantalamessa:Tafakari ya pili ya Kwaresima,Upendo hauna fitina!


Tafakari ya  pili ya mahubiri  ya Kipindi cha Kwaresima yanayotolewa na Padre Raniero Cantalamessa kwa Mwaka 2018 mjini Vatican, tarehe 2 Machi  yameongozwa na mada ya  upendo hauna fitina, akitafakari juu ya upendo kikristo tangu enzi zile hadi sasa. Katika mada hiyo amefafanua katika vipengele vinne: kuhusu kisima cha utakatifu kikristo; upendo wa dhati; upendo kwa wale walio nje ya jumuiya na upendo wa ndani ya jumuiya kwa mujibu wa barua za Mtakatifu Paulo.

1. Katika kisima cha utakatifu kikristo:
Padre Cantalamessa akijaribu kufafanua juu ya kisima cha  utakatifu kikristo anasema ulimwengu  unaalikwa katika utakatifu.Mtaguso Vatican  II a unatoa maelezo muhimu juu ya  nini maana ya utakatifu hasa wa njia ya maelekezo kutoka "Mwanga wa Mataifa ( Lumen gentium): Bwana Yesu, mwalimu na mfano wa sura ya Mungu kwa kila ukamilifu wote na kila mmoja ya wafuasi wake  na hali zozote alitangaziwa utakatifu wa maisha ambayo yeye mweyewe ni kiongozi wa ukamilifu na  kwa maana hiyo mwe wakamilifu kama alivyo Baba yangu wa mbinguni (Mt 5,48). 
Alituma Roho Mtakatifu kwa wote  na ili kuwatingisha waweza kupenda Mungu kwa moyo wote, roho yote, akili na nguvu zote. (taz Mk 12,30), na kupendana kama Kristo walivyo wapenda (Yh13,34; 15,12).Wafuasi wa Yesu wanaalikwa na Mungu si kwa ajili ya sifa ya matendo yao, bali kwa sifa na ishara zake na neema ambayo ni ya haki katika Kristo Bwana wetu. Kutokana na hiyo  ubatizo katika imani wote wamekuwa kweli wana wa Mungu na kushiriki asili yeke ya kimungu na hivyo kuwa kweli watakatifu. Kwa msada wa Mungu lazima kuwa wakamilifu katika maisha yao ya utakatifu walio upokea (LG 40). 

Kwa ufupi wa hayo yote  “ utakatifu ni ukamilifu wa muungano na Kristo (LV,50. ) na hivyo maono haya yanatafakari  kwa wasiwasi mkuu wa Mtaguso  wa Vatican II, ili kuweza kurudi katika kisima cha Biblia na maandiko ya mababa wa Kanisa kwa lengo la kushinda hata mapambano ndani ya uwanja wa shule zilizokuwa zimetokea karne hizo. Hiyo ni kutaka kuwa na utambizi wa maono mapya ya utakatifu ambao ynawezesha  Kanisa kutenda,hasa wakati wa kutangaza neno, Katekesi na mafundisho ya kiroho kwa makanditati wa kikuhani na maisha ya kitawa ; ikiwa ndiyo maana ya maono ya kitaalimungu ambayo pia hufanyika katika mchakato wa Baraza la Kipapa la kuwatangaza watakatifu.

Ufupi wa Biblia unakamilika na kuwa zaidi utakatifu kwa msingi wa kutangaza Neno jema ambapo Mtakatifu Paulo katika barua yake kwa warumi sura ya (12 na 14). Mwanzo  Mtakatifu anayo maono yanayotazama  hatua za safari ya utakatifu kwa waamini na lengo lake. “Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.  Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu” (Rm 12,1-2).

2. Upendo wa dhati:
Padre Cantalamesaa akielezea kipengele juu ya upendo wa dhati anasema, upendo wa kikristo si kusema ni moja ya fadhila tu  bali ni aina  kati ya fadhila zote ambazo zinategemea sheria na manabii  (Mt 22, 40; Rm 13,10) .Kati ya matunda ya Roho ambayo Mtume Paulo kwa Wagalatia 5,22) anataja,  ya kwanza ni upendo ; “ tunda la Roho ni upendo, furaha , amani…” hivyo inakwenda sambamba na fadhila nyingine ambazo zinapatikana katika Barua ya Mtakatifu Paulo kwa Warumi sura nzima ya 12, akifafanua  na kutoa ushauri juu ya upendo. “Pendo na lisiwe na unafiki lichukieni lililo ovu, mkiambatana na lililo jema”. (Rm 12,9…. )

Ili kutambua roho ya ushauri huo, ambao Mtakatifu Paulo anatualika katika upendo,ni lazima kuanzia na neno la kwanza  “Pendo lisiwe na unafiki“. Si moja ya ushauri tu, bali ndiyo mama wa fadhila zote na ndiyo siri ilipo ya upendo. Upendo wa kweli kwa mkristo ndiyo asili ya msukumo wa kupenda kwa dhati na ambayo inajirudia katika vipengele vingine vya barua nyingine  (2 Kor 6, 6 e in 1 Pt 1, 22). Upendo anaotaka ni ule unaonekana kwa njia zote za maneno na matendo na pia ule wa ndani ambao unajikita katika roho na mwili. Hali halisi ya upendo inaendelea kujieleza zaidi katika  mahitaji ya watakatifu “mkifuata ukarimu; katika kukaribisha wageni mkijitahidi.(1Kor 13) kwa kuonesha kuwa wema kwa wengine unakuja hawali ya yote kabla ya mwengine.

Upendo wa ndani na nje vyo vinaenda sambamba kama inavyojeleza katika Neno la Yesu mwenyewe katika  Injili ya  Matayo sura ya 25  akisema: yote mliyo fanya kwa wale wadogo…. ,  Yakobo 2,16, na mtu wa kwenu akawaambia, Enendeni zenu kwa amani, mkaote moto na kushiba, lakini asiwape mahitaji ya mwili, yafaa nini? …..  (1Yh 3,18)  Watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, bali kwa tendo na kweli. Kutokana na mifano hiyo ni  kabisa kuona kuwa maelezo yote hayo yanasukuma katika upendo  wa matendo  kwa utambuzi wa Mtakatifu Paulo alivyokuwa mstari wa mbele kwa maskini wa Yerusalem anathibitisha Padre Cantalamessa!

3.Upendo kwa ndugu walio nje:

Baada ya kueleza njinsi gani ya kufanya upendo wa kweli kikristo, mtume katika kuendelea  lazima ajioneshe katika hali halisi ya maisha ya jumuiya. Aina mbili ambazo Mtakatifu Paulo anasisisiza ni ile  ya kutazama kwa kina mahusiano ya nje ya jumuiya yaani wale ambao wako nje; pili mahusiano ya ndani yaani wale wanaoishi ndani ya jumuia yenyewe. Mtakatatifu Paulo kwa njia hiyo anathibitisha kwa njia ya maandiko kuwa:“Furahini pamoja nao wafurahio; lieni pamoja nao waliao.  Mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi. Msinie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge. Msiwe watu wa kujivunia akili.  Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote.  Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote. Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana.  Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake.  Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema”. (Rom 12, 14 - 21).

Katika barua hiyo inajionesha jinsi gani maadili ya Injili ni asili ya kweli na kuonesha uaminifu wake endelevu. Jumuiya ya wakristo Roma ni mwili  na kiungo kwa namna kinavyokea habari njema hiyo. Upo utambuzi pia wa vishawishi ambavyo viliwakabilia haa ya kufungia binafsi wakiendeleza mira na desturi za urithi wa wachache waliokombolewa kutoka katika dunia iyopotea. Na hizsia hiyo pia iliwatazama watu wa kihistoria wa jumuiya ya Esen ya Qumran anathibitisha Padre Cantalamessa.

Kwa ushauri wa Mtakatifu Paulo unaweza kutoa ushuhuda wa matumaini yaliyomo ndani mwake  kwa upole na heshima na  kama anavyosistiza Mtakatifu Petro katika barua yake: Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu. Nanyi mwe na dhamiri njema, ili katika neno lile mnalosingiziwa, watahayarishwe wale wautukanao mwenendo wenu mwema katika Kristo. (1 Pt 3, 15-16). Padre Cantalamessa anaongeza: Hiyo inahitaji kutambua mtindo wa moyo ili kujikita mbele ya binadamu ambaye kwa ujumla anamkataa Kristo na kuishi katika giza badala ya mwanga  kama Injili ya Mtakatifu Yohane isemavyo: Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu” (cf. Gv 3,19). Katika tabia za namna hiyo ndipo upendo wa kina na uchungu wa kiroho unakufanya kuwapenda na kuteseka kwa ajili yao na kubeba mzigo wao  mbele ya Mungu kama Yesu alivyobeba mizigo yetu na kuipeleka mbele ya Baba yake wa Mbinguni!

4. Upendo wa ndani
Padre Cantalamessa akifafanua sehemu hiyo ya upendo wa ndani anasema, sehemu ya ya pili  ya zoezi la upendo linatazama mahusiano ya ndani ya jumuiya: Kwa dhati inahusiana na jinsi gani ya kukabiliana na migongano iliyopo ndani ya jumuiya . Katika nafasi hiyo , Mtakatifu Paulo anatoa barua yake ya ushauri  katika sura nzima ya 14. Hii ni kutaka kuonesha wazi  mitafaruko iliyokuwa imetokea katika jumuiya  ya wakristo wa Roma, ambapo Mtume Paulo alikuwa akiwaita wadhaifu,  wenye nguvu na wale wale wanajipendeza wenyewe: “Basi imetupasa sisi tulio na nguvu kuuchukua udhaifu wao wasio na nguvu, wala haitupasi kujipendeza wenyewe”. (Rom 15,1).

Wa kwanza walikuwa wale ambao walikuwa wanahisi ndani ya dhamiri zao kutazamwa na sheria zilizokuwa zimerithiwa na sheria za hawali hasa za wapagani; kwa mfano kutokula nyama ,wakidhani kuwa  labda ilikuwa  imechinjwa wa ajili ya kutoa sadaka za miungu pia  walikuwa wakitofautisha  siku moja  na nyingine! Wa pili ni wenye nguvu:  hawa walikuwa wanatumia  jina la uhuru wa Injili yaani ambao hawakuwa wanashikilia mwiko wowote uwe wa chakula au kutofautisha siku yoyote. Kwa njia hiyo itimisho Mtakatifu Paulo anasema “Kwa hiyo mkaribishane ninyi kwa ninyi, kama naye Kristo alivyotukaribisha, ili Mungu atukuzwe. Kwa maana nasema, ya kwamba Kristo amefanyika mhudumu wa agano la kutahiriwa kwa ajili ya kweli ya Mungu, kusudi azithibitishe ahadi walizopewa baba zetu;  tena ili Mataifa wamtukuze Mungu kwa ajili ya rehema zake; kama ilivyoandikwa, Kwa hiyo nitakushukuru kati ya Mataifa, Nami nitaliimbia jina lako. Na tena anena, Furahini,Mataifa,pamoja na watu wake.  Na tena, Enyi Mataifa yote,msifuni Bwana; Enyi watu wote,mhimidini. Na tena Isaya anena, Litakuwako shina la Yese, Naye aondokeaye kuwatawala Mataifa; Ndiye Mataifa watakayemtumaini” (cf. Rom 15, 7-12).

Padre Cantalamessa kwa ujumla ametaka watambue kuwa walikuwa na tatizo juu ya  mahusiano kati ya waamini wanaotoka katika uyahudi na waamini wanaotoka katika mataifa. Kwa njia hiyo amemalizia akisema kuwa kama ilivyo kuwa migongano inatokea katika jumuiya mahalia au ulimwenguni kwa enzi zile, na hata sasa Mtakatifu Mtakatifu Paulo bado anaendela kutoa ushauri ule ule alio utoa kwa jumuiya ya waroma kwa nyakati zile kwamba: Kwa hiyo mkaribishane ninyi kwa ninyi, kama naye Kristo alivyotukaribisha, ili Mungu apate atukuzwe(Rom 15,7)!

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.