2018-03-02 16:27:00

Barua ya Papa kwa Mwandishi wa Kitabu juu ya mambo 10 kuhusu wanawake!


Baba Mtakatifu Francisko  ametuma barua kwa Maria Teresa Compte Grau mwandishi wa kitabu  chenye kichwa cha habari “ Diez cosas que el papa Francisco propone a las mujeres,” maana yake mambo kumi anayopendekezwa na Papa Francisko kwa wanawake) ambacho kitawakilishwa tarehe 7 Machi 2018 katika mji Mkuu wa Madrid, Hispania, katika kituo cha  Chama cha Mwenye heri Papa Paulo VI. Watakao toa neno juu ya kitabu hicho ni Mirian de las Mercedes Cortés Diéguez, Gombera wa Chuo Kikuu cha Kipapa cha Salamanca, Natalia Peiro Pérez, Katibu  Mkuu wa Caritas nchini Hispania, Clara Pardo Gil, Mwenyekiti wa  chama cha “mikono iliyoungana ( Manos Unidas), na  Mariña Riós, Mwenyekiti wa Baraza la Mashirika ya kitawa katika Baraza la Maaskofu Hispania  (Confer).

Katika barua ya Baba Mtakatifu anamshukuru  Maria Teresa  kwa kichwa cha habari, kitabu kinachotafakari juu ya mambo msingi anayotoa yeye mwenyewe binafsi kuhusu wanawake. Anahisi kuwa maneno yake ni tunda la uzoefu  na tafakari juu ya mada nyingi zinazojikita katika  mada hiyo na ambazo zinatoa  wito na utume wa wanawake.

Baba Mtakatifu lakini pia  anaonesha wasiwasi mkubwa  unao tokana na  baadhi ya kasumba hasi za wanaume  katika jamii hata zinazo endelea;  mahali ambapo vurugu dhidi ya wanawake inazidi, aidha jamii   kuwatendea vibaya, unyanyaswaji hata katika matangazo ya biashara katika lunginga na  kutumiwa katika viwanda. Wasiwasi pia ni juu Kanisa lenyewe  na kwamba ni nafasi ya huduma ambayo kila mkristo anaalikwa, japokuwa  wakati mwingine, Kanisa  linateleza kwa upande wa kesi zinazohusu wanawake; na hata nafasi  ya kuwa watumwa badala ya kutoaji wa huduma ya kweli.

Kwa kufuatilia mawazo ya watangulizi wake, Baba Mtakatifu anathibitisha kwamba: anaamini kuwa upo ulazima wa kuunda na kutafuta maadili ya binadamu kwa upya  ambayo inungana na maendeleo mapya ya sayansi, hata katika unyeti wa sasa wa utamaduni ili kuweza kujikita kwa kina zaidi, si kwa ajili ya utambulisho wa wanawake tu, bali hata ule wa wanaume ili huduma iweze kuwa bora na kibinadamu kwa pamoja. Lakini  ili kufikia mwelekeo huo upo ulazima wa kujiandaa katika ubinadamu mpya na daima wa kubadilika anathibitisha Baba Mtakatifu! Ni matarajio yake kuwa katika kitabu hicho kinaweza kuwa na uhusiano hasa kwa mantiki hiyo.

Ni wazi katika kitabu cha tafakari yake anaongeza Baba Mtakatifu, hakusahau Maria, Mbarikiwa kuliko wanawake wote, na anaamini kwa mfano wa kuwa mwanamke, Maria anaweza kuonekana kwa namna ya pekee, ambayo yeye binafsi anapendelea kuita mtindo wa Maria, kwa kufuata Waraka wake wa kitume  wa Injili ya Furaha  Evangelii Gaudium (n. 288). Mtindo ambao unawaalika ulazima wa kumtazama Mama ambaye anapenda kwa upole na ukarimu. Waume na wanawake wa Kanisa wasipoteze mtanzamo huo kwa maana ni muhimu anashauri Baba Mtakatifu!

Katika mambo kumi yanaweza kuwasaidia wale ambao watasoma  na Bwana aweze kuwajaza mara mia na  kutembea daima kwa  moyo wa kina, wakiwa na utambuzi wa utume mkubwa wa kimisonari na utume wa mwanamke. Bwana ambariki  na Bikira Maria Mtakatifu amlinde. Bwana amsaidia katika shughuli ya utafiti na ualimu, akisaidia watu wengine kugundua uso wa Yesu ambaye anapenda waume na wanawake bila ubaguzi na zaidi maskini wadhaifu wa kukithiri. Asisahau kusali wa ajili yake.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!

 








All the contents on this site are copyrighted ©.