2018-03-01 16:58:00

Kanisa Kuu la Kaburi Takatifu Yerusalem,limefunguliwa tena kwa mahujaji!


Tarehe 28  Februari 2018 saa 4.00 masaa ya nchi za Mashariki imefunguliwa kwa upya Kanisa Kuu la Kaburi Tatifu katika  nchi Takatifu, iliyokuwa imefungwa kwa umma hivi karibuni. Uamuzi huo ulichukuliwa na wawakilishi wa jumuiya Katoliki ya Waorthodox na Warmenia, mara baada ya Waziri Mkuu wa Israeli Bwana Benjamini Betanyahu, kufanya mkataba na Meya wa Yerusalem, Nir Barkat , aliyetangaza kusitisha kuomba ushuru wa manispaa, katika shughuli zinazoendeshwa na dini. 

Hizo ni shughuli zinazohusiana moja kwa moja na jumuiya za dini ambazo ziliongozwa   na tume na kikao na waziri wa shirikisho la Kanda, Tzachi Hanegbi. Jumapili iliyopita walikuwa wametazama masuala yanayohusiana na sheria ambayo inayotazama ardhi binafsi zilizo uzwa na Jumuiya za dini  kwa watu binafsi mara baada ya 2010.

Msimamizi wa nchi Takatifu Padre Fracesco Patton, Patriaki wa Kiorthodox Teofilo III na wa Kiarmenia, Nourhan Manougian walitangaza kwa pamoja kuonesha kuwa wao kama viongozi wa  Makanisa wanayosimamia Kaburi Takatifu na maeneo yote mbalimbali matakatifu ya Yerusalem, wanashukuru Mungu kutangazwa jioni ya ya tarehe 27 Februari, Waziri Mkuu Netanyahu juu ya suala hilo na kuoenesha shukrani za pekee kwa wale wote walifanya kazi bila kuchoka ili kuweza uwepo wa ukristo Yerusalem undelee na kutetea kila hali ya maisha yake.

Baada ya tamko la waziri Mkuu, viongozi hao wanasubiri kukabiliana na waziri Hanegbi na wote ambao wanapenda Yesusalem ili kuhakikisha mji wao mtakatifu unaendelea kuwa changamoto ya uwepo wa ukristo  na kubaki sehemu ambayo dini tatu zinazo fanana zinaweza kuishi na kutarajia pamoja. Kwa njia hiyo Kanisa Kuu la Kaburi Takatifu mahali ambapo Bwana wetu alisulibiwa , akafa na kukufua pamefunguliwa kwa ajili ya mahujaji wote tarehe 28 Februari 2018 saa 4.00 asubuhi masaa ya nchi za Mashariki.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News

 








All the contents on this site are copyrighted ©.