2018-02-28 15:50:00

Papa amesalimia waamini katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro!


Baba Mtakatifu amewasalimia hata waamini waliokuwa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, amewashukuru kwa uvumilivu wao ambao wameweza kusubiri hadi mwisho. Bwana abariki uvumilivu wao na anaamini kuwa ilikuwa vema wawe ndani humo kuliko kuwa nje katika baridi. 

Na Katika salam zake za mwisho mara baada ya katekesi yake, amerudia kukumbuka nchi za Mashariki ambazo wanaendelea kuteseka na vita. Amesisitiza kuwa ni lazima kusali kwa ajili ya ndugu na kaka wanaoteseka wakati wa kusalimia waamini katika lugha ya kiarabu. Hata hivyo ikumbukwe kuwa siku ya Jumapili 25 Februari wakati wa kumaliza sala ya Malaika wa Bwana, alikuwa amerudia kutoa wito huo huo kutokana na mashambulizi ambayo yamesababisha vifo vya maelfu ya watu wa Siria katika mji wa Ghouta.

 Sr. Angela Rwezaula 

Vatican News!

 








All the contents on this site are copyrighted ©.