2018-02-27 13:33:00

Mons.Vigano':Ameadhimisha misa kwa wafungwa wa Magereza ya Rebibbia Roma!


Kwa ajili ya rafiki zenu, kuwasikiliza na kuwapa ushirikiano wa makutano kwa anayeteska zaidi katika hali ya kubaguliwa. Na hivyo wapende familia zenu na watoto wenu. Hata kwa machozi katika macho yenu na mioyo iliyo jaa uchungu, salini nao na kuwashukuru kwa ukaribu wao ambao unawasaidia kushinda uchungu wa upweke.

Ni wito wa Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Mawasiliano Monsinyo Edoardo Vigano' alio utoa  katika nyumba ya wafungwa huko Rebibbia Jumapili 25 Februari 2018, asubuhi wakati wa kudhimisha ibada ya misa. Misa hiyo imeandaliwa na Padre Nicola Cavallo msimamizi wa Kanisa la magereza la wafungwa, na kushiriki  misa hiyo hata mkurugenzi wa kitengo cha Taalimungu ya kichungaji ya Sekretarieti ya Mawasiliano Bi, Nataša Govekar na mwana Biblia wa Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregorian Roma, Profesa  Rosalba Manes, anayejitolea kwa wafungwa katika Magereza ya Rebibbia.

Akiendelea na mahubiri yake Monsinyo Vigano amekumbuka mawazo ya Papa Francisko anayo rudi mara kwa mara katika ujumbe wake hata hivi wa kuwa karibu na wafungwa. Ujumbe wa mwisho wa Papa Francisko wakati wa sala ya Malaika wa Bwana aliwatumia salam  wafungwa wote katika magereza na kuwatia moyo kila mmoja ili waishi kipindi cha kwaresima kama fursa ya ya kujiuindia moyo safi chini ya mtazamo wa huruma ya Bwana, kwa maana yeye hachoki kamwe kusamehe.

Somo la kwanza linaelezea uzoefu wa Ibrahimu ambaye labda wamesikia historia yake mara nyingi. Ibrahimu alikuwa na mtoto wa pekee Isaka, aliyemzaa wakati wa uzee wake. Ni mtoto wa pekee wa ahadi ambayo alikuwa ndiye alete ukombozi kwa watu wengine. 
Lakini Siku moja Ibrahim akapokea amri kutoka kwa Mungu ili amtoa sadaka mtoto wake . Ni mzazi yupi anaweza kueleza jambo hili la kiajabu, kuomba atolewa sadaka mtoto wa pekee?

Lakini cha kushangaza, Ibarahimu pamoja na kuumizwa  moyo wake, anakubali moja kwa moja kuanza maandalizi ya  kwenda mahali alipo elekezwa. Aliandaa altare na kuweka kuni, akamfunga mwanaye na kuchukia kisu tayari kumchinja. Ibrahimu anaamini Mungu kwa kina hadi kufikia hatua ya kumchinja mwanae, tegemeo lake endelevu na  ahadi katika ardhi .

Imani hiyo pia zaidi inaoneka katika upendo wa Mung kwa Binadamu ambau sasa anaoesha wazi kuwa hapendi kifo chake bali maisha tu.Kwa njia hiyo utii wa Ibrahimu unakuwa kisima cha baraka hadi leo hii. Na kwa maana hiyo Monsinyo Vigano anathibitisha kuwa hata majaribu makubwa ya kutisha tunao uhakika kuwa haku lolote linaweza kututenganisha  uwahikia kuwa hayawezi kutengenisha na upendo wa Mungu. La muhimu ni kuamini kabisa Mungu na kuwa na shauku naye ambaye alimfufua mwanae mpendwa Yesu Kristo.

Katika Injili ya siku, inawataka waamini wote kutambua ya kuwa tuna mahitaji ya kupanda mlima wa mageuzi ili kupokea mwanga wa Mungu kwasababu uso wake uweze kuangaza hata nyuso zetu.  Hiyo inaweza kupitia katika sala, ishara ndogo ndogo za kuwakaribisha wengine , msamaha na huruma, kutenda haki , kuishi kindugu , urafiki wa dhati. Haya yote ni matendo ya kukutana na Bwana si kama wazo la kufikirika  au kama mapendekezo yasiyo na msimamom ni jambo la dhati la kukutana na mt una maisha kamili katika Kristo. Kipindi cha kwaresima anamalizia  ni  nafasi yetu, hata machozi na moyo uliojaa uchangu, wa kusali na kumshukuru mungu kwa ukaribu ambao unaweza kushinda uchungu na upweke.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.