2018-02-27 14:07:00

Hotuba ya Kard.Pietro Parolin katika kuwakumbuka wakristo wanaoteswa!


Tarehe 24 Februari 2018  Gofu la Colosseo mjini Roma liliangazwa kwa rangi nyekundu , rangi ya damu ya wafia dini, ili kuwakumbuka wakristo waliobaguliwa na kuteswa duniani wakitetea imani yao. Kuwasha mwanga huo wa rangi nyekundu ulienda sambamba na  Kanisa la Mtakatifu Paulo huko Mosulna Kanisa Kuu la Kimaroniti la Mtakatifu Elia huko Aleppo. Waandaji wa  mkesha wa kumbukumbu  hii ni Shirika la Kipapa la  Kanisa hitaji ambapo kati ya viongozi wengi waliodhuria ni pamoja na Kardinali Petro Parolin Katibu wa Vatican.  Akitoa hotuba yake Kardinali, amewashukuru Shirika la  Kipapa la Kanisa hitaji kwa ajili ya uwakilishaji na kunzisha tukio hili pia fursa aliyopewa.

Amewasalimia washiriki wote, kwa namna ya pekee wote waliounganikwa kwa pamoja kwa njia ya mawasiliano  huko Aleppo na  Mosul kwa afla hiyo ya kuwakumbuka wafia dini. Anawatumia  salam za upendo mkubwa pia kwa wote ambao katika nchi za Mashariki na ulimwengu mzima wanajaribiwa na mateso kiroho na kimwili, wakati huo wakiendelea kusali kwasababu ya  matukio ya vurugu na ghasia za kila aina na kwamba wakati mwingine kilio hicho kinabaki katika  ukimya na sintofahamu .

Aleppo na Mosul, ni maeneo mawili  ya ishara ya uchungu mkubwa uliotokana na itikadi kali za chuki na sera za kisiasa ya uchumi , jioni ya siku hiyo Kardinali anasema, wameweza kufanya ishara nyingine kubwa kwa ajili ya wakristo na dunia nzima yaani yaani  katika magofu ya Colosseo. Mwaka 2000 katika kumbukumbu hiyo,magofu hayo yalichaguliwa na  Mtakatifu Yohane Paulo II kwa ajili ya kufanya kumbukumbu ya kiekumene kwa mashahidi wa imani wa karne ya XX. Ushuhuda wa umwagaji damu wa wakati ule bado unaendelea hadi leo hii. 

Baba Mtakatifu Francisko hachoki kamwe kusema mara nyingi kuwa leo hii Kanisa ni Kanisa la Mashaidi. Leo hii ni kukumbuka wakristo walioteswa  bila kusahau wafia wa madhehebu mengine katika dunia ya kiekumene wanaendelea kuteseka kwasababu ya tunda la chuki kipofu, na wanatesaka na matukio ya ukiukwaji wa uhuru wao msingi ,kati ya huo ni uhuru wa dini. Ndugu zetu kaka na dada ni waathirika wa kwanza dhidi ya mantiki isiyo tambua nafasi ya mwingine, yenye utofauti na kutaka kuondoa nafasi yake. Kuheshimu uhuru wa dini si jambo jengine zaidi ya utambuzi wa hadhi ya kila binadamu.
 Tarehe 23 Februari kwa mwaliko wa Papa Francisko wamesali na kufungu, kumwomba Mungu zawadi ya amani na hasa katika nchi ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo, Sudan ya Kusini na Siria. Ni kwa njia ya kumrudia Mungu , kisima cha hadhi ya kila kiumbe , tunaweza kuwa wasanii wa amani na kushona mahusiano ya pamoja yaliyochanika , ilikuweza kushi katika jamii iliyochanika kwa chuki na ghasia. Kardinali Parolin anaongeza; leo hii ni uwakilisha ishara hii kwa ajili ya kusaidia na kuwa karibu . 

Ishara na opicha amabzo zipi , sinawakiloshwa mbele ya macho yetu ili ziweze kugusa dhamiri na kufuta ule utofauti  kwa kugeuka kuwa wawajibikaji . Leo hii zaidi ya kale wakristo wangi duniani wanaishi na uchgun wa kweli katika mateso kwa ajili ya kutete imani yao, wanalipa kwa njia ya kushuhudia Kristo, ujumbe wake wa upendo na msamaha. Kwa njia hiyo sala zetu na msada wetu , mshakamano na kutiwa moyo viwandee wao . Kwa njia yao leo hii ni kurifaia upya wajibu wetu kiroho na zana ili kuwahakikishaia kuwa kilanjia inawezakana kupitia ili kuhamasiaha amani , usalama na wakati mzuri endelevua wakati huo huo walie ambao wanajikitia katika kukimbilia wenye mahitahiji ya kibadamu, shukrani za dhati ziwaendee.

Akimalizia, Kardinali Pietro Parolin anasema kwa pamja katika mshikamo wao , na kuwasiaida ndiigu katika matumani na nguvu ya ukomozi wa Bwana . 
Shughuli hiyo haifanyi kazi kwa mantiki ya dunia bali ya Mungu ambayo kwa upendo wa unyenyekevu anaasha kila mmoja awe huru na yupo tyari kujitoa kwa kila hali yoyote kuchukua msalaba ili kusaidia, kukumbaitia na kuokoa. Ndiyo ushuhuda wa Yesu ambao kama mbegu dogo intoa matunda (taz. Yh , 12, 24); na kufanya kazi kwa uvumilivu kama wa mbegu ya aladari (taz. Mk 4, 30-32) ambayo kupandwa katika shamba la ulimwengu na kuona na kuwa na matawi yake ambayo yanatoa kivuli kwa wale wanaotafuta na kuwatuliza na amani ambayo ni upendo tu anaoweza kuutoa.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.