2018-02-24 10:40:00

Ireland:Wanafamilia wanaalikwa kuandaa vema Siku ya IX ya Familia Duniani 2018


Baba Mtakatifu Francisko amechagua mji wa Dublin kukaribisha Mkutano mkuu wa Siku ya IX ya Familia Duniani utakao anza tarehe 21-26 Augosti 2018 ukiongozwa na  kauli mbiu "Injili ya Familia: furaha ya ulimwengu”.  Mkutano huo hufanyika kila baada ya miaka mitatu, ambapo mkutano huo mkubwa wa kimataifa hukusanya familia nyingi pamoja kutoka dunia nzima ili kuadhimisha, kusali na kutafakari kiini na umuhimu wa ndoa na familia kama jiwe la pembeni la kuishi kwetu, la jamii yetu na  Kanisa letu. Haya ni maelezo ya Askofu Buckley, wa Jimbo la Cork na Ross nchini Ireland wakati wa ibada ya misa kuipokea picha ya Mkutano Mkuu wa Familia nchini Ireland, jioni ya tarehe 22 Februari 2018.

Askofu anasema  kwamba, wanaikaribisha picha hiyo katika jimbo lao kwa furaha kubwa! . Paia yeye binafsi alipata kuibariki katika madhabahu ya Kitaifa ya  Mama Maria wa  Knock mwezi Agosti 2017, kwa ushiriki wa familia nyingi  kutoka Cork na Ross, maaskofu, mapadre na wanamini kutoka majimbo 26 ya Kisiwa cha Ireland mahali amabapo tangu wakti huo, imeanza kuzungukia kisiwa hicho hadi siku ya maadhimisho hayo.

Anathibitha zaidi kwamba, ni bahati ya pekee kwa nchi ya  Iraland kuchaguliwa na Papa Francisko kuukaribisha Mkutano wa dunia wa Familia mwezi Agosti. Zawadi hiyo inawafikia kutokana na kwamba Baba Mtakatifu anatambua mzizmi mkuu wa utamaduni wa maisha yao ya familia na utume wa kuwafikia wengine kwa Imani. Ni Imani yake Papa Francisko atafika ili kuweza kushirikishana nao tukio hilo na kuwapa moyo ili wajite kwa upya kutambua zaidi juu ya umuhimu wa familia.

Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili alikuwa wa kwanza kufungua Sinodi ya kwanza ya Familia, hivyo wa kwanza kuanzisha tukio hili wakati wa utume wake ambapo hata kuandika waraka wake juu ya maisha ya familia akisema: “Maisha ya binadamu yanapitia njia ya familia. Familia ni msingi wa utakatifu. Watoto kamwa hawatacha ukweli wa familia, wanaweza kuacha nyumba, kuacha mji hata nchi yao lakini hawewezi kamwe kuiacha familia zao. Shule zetu zinaweza kuwa na walimu wanaoofundisha watoto wetu vizuri, lakini sehemu kubwa ya kuishi maisha yao daima ni katika familia zao, yaani wazazi, babu ba bibi zao. Maisha yetu yanajengwa juu ya uhusiano tulio nao na familia zetu, kwa kutupatia msaada na kujenga juu ya furaha ya upendo”.

Katika kukuza hilo ni kuanzia na wosia wa Furaha ya upendo, ambayo imepata nafasi kubwa ya kuendelea kugundua na kupokea utajiri wa nyaraka za kipapa kwa miaka ya hivi karibuni. Hiyo pia inaangazia  mwaka 2016,ambapo  Papa Francisko alitoa wosia mzuri wa kusoma na kutafakari kwa kina uitwao Amoris Laetitia  yaani Furaha ya Upendo ndani ya Familia, mwendelezo huo unaopaswa kugunduliwa kwa kina kuupokea utajiri wake na  kuwa kiongozi katika shughuli zote za kichungaji.

Tangu kutolewa kwake Askofu anathibitisha kuwa  bado unaendelea kufanyiwa utafiti zaidi kupitia majimbo yote na kwa namana ya pekee katika kipindi cha mwaka mzima wakati wa kuandaa  mkutano Mkuu wa dunia wa familia 2018. Makanisa yote kwa njia ya familia wanaalikwa  kuhamasisha umuhimu wa ndoa za kikristo anathbitisha Askofu.

Kanisa ni mfano wa ndoa katika mahusiano na mme na mke kama kioo cha uhusiano wa Kristo na Kanisa lake.  Kila familia ni Kanisa la nyumbani, pia ni shule ya sala; na wazazi wanaombwa kuwasaidia watoto wao nyumbani. Katika Kanisa la Ireland ni lenye utamaduni wa familia zinazosali ndani ya nyumba zao; ndiyo msimamo mkuu ulio saidia wakati mateso ya wakristo na kipindi kigumu. Sala zinaunganisha familia na kila mmoja anafahamu hilo kwamba familia inayosali pamoja na kuishi pamoja inaishi kwa upendo.

Katika kipindi hili cha kwaresima kwa namna ya pekee katika somo la Isaya na masomo mengine yanaalika kusali kama watu wa Agano la kale waliochaguliwa na Mungu. ”Nisikilizeni, ninyi mnaoifuatia haki;ninyi mnaomtafuta Bwana; uangalieni mwamba ule ambao mlitolewa kwa kuchongwa, na tundu la shimo ambalo mlitolewa kwa kuchimbuliwa  (taz Isaya 51,1). Kutokana na maneno hayo wote wanaalikwa kutoka waliko lakini bila kusahau tamaduni walizorithi  kuziendeleza zaidi katika sala ya familia na maisha yao.

Mkutano Mkuu wa familia dunia uanaowadia anasema Askofu kuwa, wote wanaalikwa  kwa nguvu zote  katika sala kwa upya ndani ya familia. Mkutano huo utaudhuriwa na familia nyingi kutoka katika dunia. Akitoa mfano anasema  , kwa namna ya pekee Jimbo Kuu la Los Angles ambalo ni jimbo kubwa nchini Marekani  na ambalo  Askofu wake msaidizi David O’Connell ni mzaliwa wa Glanmire, Co Cork Ireland , katika jimbo hilo ataongoza ndege iliyo jaa mahujaji kufika Ireland  kwa ajili ya tukio maalum la maadhimisho hayo  mwezi Augosti 2018.

Sr Angela Rwezaula 

Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.