2018-02-22 14:37:00

Tume mpya ya Shirikisho la Kianglikani itafanya mkutano karibuni huko Cairo


Wajumbe wa Tume mpya wa Shirikisho la waanglikani (New Anglican Inter Faith Commission, Aifc) watakutana siku zijazo mjini Kairo Misri kwa ajili ya mkutano wao wa kwanza. Tume hiyo imechaguliwa kwa matashi ya Baraza kuu la ushauri la Kiangiliakani wakati wa mkutano huko Lusaka Zambia mwaka 2016 na kutangazwa tena wakati wa mkutano  wa wakuu wa Muungano huo, uliofanyika huko Canterbury Uingereza Oktoba mwaka jana. Lengo kuu  la Tume mpya  ni kutaka kuleta utambuzi zaidi kati ya makundi tofauti ya imani na kujaribu kukuza  imani, mahali ambapo bado kunatawaliwa na mawzo ya ujinga na vikwazo. Atakayeongoza tafakari ya mkutano wa Tume  mpya ya Aifc ni  Josiah Idowu-Fearon mtaalimungu na mtaalam wa mahusiano kati ya wakristo na waislam itakayokuwa, pia  wajumbe kutoka Afrika ya Kaskazini na Mashariki kwa mujibu wa habari za mtandao wa kiangliakani  anglicannews.org  watashiriki.

Askofu Mkuu Justin Welby wa Canterbury nchini Uingereza,  akifafanua juu ya mkutano huo, anafurahishwa hawali ya yote kuundwa kwa tume hiyo. Anawakaribisha kwa shauku kubwa kuanza kazi hiyo akisisitiza juu ya umuhimu Tume ya kidini kwa ajili ya wakati endelevu. Katika ujumbe kwa njia ya video kwa tume  mpya (Aifc), Askofu Mkuu wa Canterbury anaeleza kuwa, dunia inatafuta kupembua na kutambua kati ya  viongozi wa kidini, ule uwezo wa kutokuwa na utofauti, bila chuki. Hiyo ni kutokana na kwamba: kwa bahati mbaya uwezo wa kuishi bila utofauti na  kuishi bila chuki katika dunia hii utafikiri ni ndoto maana ni hali inayozidi kupungua siku hadi siku. Kwa njia hiyo Askofu Welby kwa   wajumbe wa tume mpya anasema, wanapaswa kutafuta mtindo na mfano  mpya ambao mara nyingi Yesu Kristo anapenda kuutumia na kuongea  kwa  upendo, utokao juu ya msalaba, katika ufufuko; unaonekana wakati wa kupaa kwake mbinguni na hata katika kutoa zawadi ya Roho Mtakatifu.

Shughuli za tume mpya ni kuleta uwezo  wa kutoa ushuhuda kikristo katika ulimwengu wa dini nyingi katika  kanda za Umoja wa kiangilikani. Aifha anakumbusha Askofu Mkuu Welby kuwa, Tume hiyo imepolewa kwa shauku kubwa na viongozi wengine wa kikristo, akiwemo hata patriaki Tawadros II wa Kanisa la Kiorthodox  ambaye pia ataweza kukutana na wajumbe wa tume hiyo wakati wa mkutano wao mjini Cairo. Pamoja na hayo wajumbe wa tume hiyo watakutana hata na Imam mkuu wa  Al-Azhar.

Naye Askofu Mouneer anasema, shughuli muhimu kwa wafuasi wa imani nyingine za dini imekuwa sasa ni muhimu na hasa kujikita kwa juhudi zoote katika kazi kwa pamoja kwa ajili ya wema wa wote ili kuweza kuwa na maelewano pamoka na kusaidiana na mwingine kama watu ambao wameombwa kwa mfano na sura ya  Mungu na kupendwa na Yeye!

Sr Angela Rwezaula
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.