2018-02-22 16:02:00

Toleo la tatu la Mahubiri ya Papa Francisko katika Misa za asubuhi kutolewa!


Katika duka la vitabu kwa sasa kinapatikana kitabu kimoja  chenye kichwa  cha habari “Papa Francesco: Unyenyekevu na mshangao”. Ni toleo la tatu la kitabu cha Mkusanyiko wa mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko kuanzia mwaka 2015 hadi Juni 2017. Huo ni mkusanyiko wa mahubiri karibia laki mbili katika toleo la tatu linalojikita mahubiri ya Baba Mtakatifu katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican kila asubuhi. 

Wakati wa kuwasilisha kitabu hicho kwa vyombo vya habari Kardinali Ginfranco Ravasi ambaye ni Askofu Mkuu Katoliki wa Italia amesema, kitabu hicho ni fursa ya pekee ya kukusanya na kutambua asili na maono ya muhubiri mkuu.

Katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican, Baba Mtakatifu alianzisha namna mpya ya kuanza na kushi asubuhi kwa misa. Uasili wake unapatikana katika mahubiri yake ambayo anatoa bila bila kuandika au kuwa na uhusiano wowote na karatasi  yaani kwa lugha nyepesi na wazi. Ni kwa mujibu wa utangulizi wa kitabu hicho Kardinali Ravasi anaandika pia kuwa “ Papa Francisko katika mahubiri yake anapenda jambo muhimu ni kuzungumza wazi na  rahisi, bila kutumia sentensi zisizoeleweka na ngumu.

Toleo la tatu la mahuburi ambayo yameweza kuwandikwa vizuri na waandishi wa Vatican News ni fursa ya kupokea kwa njia ya maandiko matakatifu  asili na maono ya mhubiri mkuu ambaye anatoa ufungua wa uongofu wa moyo  kwa njia ya Neno la Mungu ili kuweza kupatana naye. Aidha katika utangulizi Kardinali Gianfranco anaandika kuwa, nyakati zinabadilika na sisi wakristo tunapaswa kubadilika kila wakati. Lakini mabadilimo hayo lazima kuwa na tabia ya mimamo katika  imani kwa Yesu Kristo. Kuwa  kitede katika ukweli wa Injili, lakini pia tabia zetu lazima zibadilike kila wakati kwa mujibu wa ishara za nyakati, maana sisi sote tuko huru.

Sote tu uhuru kwasababu ya zawadi ya uhuru tuliyoipta kutoka kwa Yesu na kazi yetu kubwa ni ile ya kutazama kwa kina kitu gani kinatokea ndani ya maisha yetu na kufanya mang’amuzi ya hisia na mawazo yetu; halikadhalika nini kinatoke nje yetu na kufanya mang’amuzi ya ishara za nyakati. Yote hayo ni kwa njia ya ukimya, tafakari na maombi anamalizia Kardinali Ravasi.

Ikumbukwe kuwa Kardinali Gianfranco Ravasi ni mwana biblia wa Italia, mtaalimungu na mwenye utaalam wa masomo ya kiyahudi. Tangu 2007 ni Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya utamaduni na mjumbe wa Tume ya Kipapa kwa ajili ya Sanaa Takatifu, pia mjumbe wa Baraza la kuandaa mafunzo na nyaraka za Kipapa.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.