2018-02-22 15:42:00

Maaskofu Katoliki Marekani kuhamasisha siku ya DACA,tarehe 26 Februari 2018!


Maaskofu wa Marekani wametoa wito kwa ajili ya siku ya  terehe 26 Februari 2018 kuwa, ni Siku maalum Kitaifa Katoliki kwa ajili ya kuhamasisha harakati ya kulinda mpango wa Dreamers (DACA),unao husu  kuwalinda vijana wahamiaji walio ingia Marekani wakiwa wadogo kwa njia zisizo halali wakiwa na wazazi wao kuishi nchini humo. Na kwasasa wako katika hatari ya kurudishwa nchi zao za asili.

Mpango  wa DACA ulianzishwa na aliyekuwa Rais wa Marekani Barack Obama miaka mitano iliyopita ili kuwalinda vijana hao dhidi ya kurejeshwa makwao na kuruhusiwa kusoma na kufanya kazi Marekani. Hata hivyo Obama ambaye aliahidi kutoingilia masuala ya kisiasa baada ya kustaafu alitoa taarifa akiushutumu uamuzi huo wa Trump kwa kuutaja usio sahihi, na ambao siyo wa kibinadamu wa kutaka kuwaadhibu wasio na hatia.

Kwa upande wa Maaskofu wa Marekani wanawaalika waamini wote wa nchi na wabunge waliochaguliwa kutetea  mpango wa dreamers ili kuhakikishia wanapata njia mwafaka ya vijana hao wanapata uzalenda katika nchi hiyo. Habari kutoka Baraza la Maskofu wanawakumbusha wakatoli kuwa, imani yao inawasukuma kuwasindikiza zaidi wahitahiji, kati yao ni ndugu wote kaka na dada wahamiaji, kwa njia hiyo lazima kuonesha mshikamano, ushirikiano kwa namna ya pekee  hasa wakati huu kuunana pamoja kwa dhati.

Tangu kutolewa taarifa hiyo Maaskofu wengi wamekuwa wakishutumua na kutoa wito wa dharura ili kuweza kuwatetea vijana hao. Hata hivyo siku zinazidi kupita  bila mwafaka wakati huo wasiwasi ni mkubwa kwa namna ya pekee ya vijana milioni 1,8 wa mpango  wa DACA ambao wanaweza kupoteza ulinzi huo  kufikia tarehe 5 Machi 2018 kama alivyokuwa amehaidi Rais Trump.

Pamoja na hayo tangu mwanzo wa mwezi Februari , maaskofu wengine wengi, na mashirika ya kidini yanaendelea kuongeza juhudi na kutoa  sauti zao kwa bunge , hata maoni ya umma kwa ajili ya kuendeleza mpango huo wa DACA. Pia Chuo  Kikuu cha Notre Dama huko Indianapolis kimethibitisha kuendelea kuwasaidia vijana wa Dreamers  katika kujiandikisha masomo yao na maisha yao.

Sr Angela Rwezaula
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.