2018-02-20 14:15:00

Ziara ya Askofu Mkuu Richard Gallagher nchini Azerbaijan 9-12 Februari


Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican, alianza ziara kuanzia tarehe 9-12 Februari 2018 huko Baku katika Jamhuri ya  nchi ya Azerbaijan, kuitikia mwaliko wa Waziri wa Biashara ya nchi za nje Bw. Elmar Mammadyarov na Balozi Kitume wa Vatican nchini  Azerbaijan,Vladimír Fekete, (S.D.B) aliyechaguliwa na Baba Mtakatifu Francisko hivi karibuni.Askofu mkuu Gallagher alisindikizana na Monsinyo Tymon Tytus Chmielecki kutoka katika Ofisi ya Katibu wa Vatican na Monsinyo Mihăiţă Blaj muhusika wa shughuli za mahusiano katika Ubalozi wa Vatican nchini Azerbaijan. Ametoa daraja ya uaskofu kwa Balozi mpya wa Vatican nchini Azerbaijan na kukutana na jumuiya ndogo ya waamini wa Kanisa Katoliki; kufanya mikutano mbalimbali na viongozi wa Serikali na wale wa kidini.

Mara baada ya kufika uwanja wa ndege tarehe 9 Februari Askofu Mkuu Gallagher aliadhimisha Misa Takatifu katika kituo cha wasalesiani wa Don Bosco cha Mtakatifu Maria mkingiwa wa dhambi ya Asili. Hapa pia alipata fursa ya kukutana ndugu  na jamaa wa Askofu mkuu mteule Fekete waliofika kwa ajili ya maadhimisho ya kumweka wakfu askofu mteule. Badaye alifanya matembezi mafupi huko Alley mahali alipozikwa Baba wa Taifa hilo, Heydar Aliyev na mke wake Zafira, hata kuona mnara wa makubusho  ya mashujaa wa kupigania huru. Uwakilishi wa Vatican ulipokelewa na Bwana  Ilham Aliyev, Rais wa Jumhuri ya Azerbaijan katika Ikulu. Mkutano wao walishiriki pia Balozi wa Azerbaijan aliyeko Vatican  Bwana Rahman Maustafayev.

Mkutano huo wameonesha uhusiano mwema uliopo kati ya nchi hizi mbili na utashi wa kuedeleza juhudi hizi kutokana na ziara ya Baba Mtakatifu Francisko ya tarehe 2 Oktoba 2016, hata katika baadhi ya kuanzisha mambo kadhaa ya kiutamaduni. Hata hivyo rais wa nchi hiyo  ametoa shukrani kubwa kutokana na kumteua na hatimaye, kumweka wakfu Monsinyo  Fekete kuwa Askofu mkuu. Rais alisema kuwa, hiyo ni ishara inayoonesha umakini wa Baba Mtakatifu Francisko kwa nchi yao na kuwatia moyo jumuiya ndogo ya waamini wa Kanisa Katoliki. Viongozi hawa wamejikita katika masuala yanayohusu mipango ya kitaifa kwa ajili ya kuhamasisha mazungumzo ya utamaduni na majadiliano ya kidini katika roho ya umoja, heshima kati ya dini.  Na mwisho wamebadilishana  mawazo juu ya hali hali ya kisiasa katika kanda yao na dunia kwa namna ya pekee umakini wa nchi za kiislam na  kutaka kuongeza juhudi ya kuwa na mahusiano ya umoja wa nchi za Ulaya.

Siku iliyofuata Askofu Mkuu Gallagher alikwenda katika ofisi ya Sheik Allahshukur Pashazade, Mwenyekiti wa Baraza la masuala ya  Caucaso kukutana na wajumbe wa baraza hilo na viongozi wakuu wa madhehebu yaliyopo nchini humo. Mkutano huo uliudhuriwa na  Askofu Mkuu Aleksander Ishein wa Baku- Azerbaijan   na wa Kanisa la Kiorthodox Urusi, kkuu wa Jumuia ya wayahudi  Milikh Yevdayev, na Balozi wa kitume Askofu Mkuu Fekete.

Kiini cha azungumzo yao kati ya mengi ni juu uvumilivu wa dini katika nchi ambazo zinapendelea kukutana viongozi mara nyingi na kuchangia kudumisha undugu kati yao na kuhamasisha haya namna ya kuishi kwa umoja, amani na mshikamano kati ya jumuiya za kidini. Baada ya mkutano rasmi washiriki wote walikwenda kula chakula cha pamoja kilichotolea na Sheiki kwa heshimaya Askofu Mkuu Gallagher.

Mchana Askofu mkuu alitembelea kituo kikubwa cha Heydar Aliyev cha makumbusho, humo amejifunza historia ya kizamani na ya sasa ya nchi ya Azerbaigian. Jioni alipata chakula cha usiku na baadhi ya Mabalozi wanaojulikana huko Baku. Tarehe 11 Februari alikutana na jumuiya katoliki na kuadhimisha Misa ya kumweka wakfu Askofu mteule Fekete, katika Kanisa la Mtakatifu Maria Mkingiwa dhambi ya Asili huko Baku, iliyoudhuriwa na Askofu Mkuu wa Kiorthodox Aleksander na baadhi ya mabalozi, Tbilisi, Slovakia, Austria na Roma, wakiwemo mapadre wangi, watawa na waamini. Baada ya maadhimisho hayo Askofu Mkuu alisalimiana na jumuiya na wageni wakati wa chakula cha mchana. Baada ya mapumziko kidogo alikwenda kutembelea wazee na maskini kwenye kituo cha Watawa wa Shirika la Wamisionar wa Upendo. Baada ya kuwasalimia wote alipata kusali masifu ya jioni na kukutana na watawa ambao wamesimulia historia ya shirika lao katika mji wa Baku.

Tarehe 12 alikwenda katika Tume ya Taifa ambayo inahusiana na maswala ya watawa. Alikutana na Mwenyekiti wa Tume hiyo Bwana Mubariz Gurbanli, ambaye aliwakilisha hali halisi ya watawa katika nchi hiyo na kusisitiza juu ya kuwa na haja ya kuendeleza mizizi ya kale ya ukristo. Katika mazungumzo yao kwa kirefu ameeleza hata maendeleo yaliyofanyika tayai kwa miaka 20 mara baada ya kipindi cha kuishi ukomunisti . kwa maana walikuwa wakizuia kuwapo sehemu zoztoza za kufanyia mikuano ya ibada na kichungaji.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.