2018-02-19 11:31:00

Maandalizi kabla ya Sinodi ya Vijana 19-23 Machi 2018 yatimua vumbi!


Katika Mkutano kabla ya Sinodi ya Maaskofu uliandaliwa kuanzia tarehe  19-23 Machi  2018 Mjini Roma, utakaribisha vijana 300 kutoka duniani kote na wengine milioni moja walialikwa kuchangia mapendekezo yao kutokana na maswali na ushuhuda wao kwa njia ya mitandao ya kijamii. Baba Mtakatifu Franciko atafungua Mkutano huo akijibu maswali ya vijana 5 kutoka kila bara.

Ni tarehe 19 mwezi Machi ambayo  ni siku ya kukumbuka  ya kuanza kwa kazi ya kitume  kama kharifa wa mtume Petro, ambapo pia itakuwa ni fursa ya Baba Mtakatifu Francisko kufungua kazi ya mkutano huo kwa vijana 300 kutoka duniani kote ambao watakuwa Roma hadi tarehe 24 machi, katika Taasisi ya Maria Mater Ecclesiae. Lengo kuu ni kujadili mada ya Sinodi ya Maaskofu inayohusu Vijana, imani na mang’amuzi ya miito itakayofanyika mwezi oktoba mwaka huu.

Ikumbukwe kuwa pamoja na vijana ambao wataudhuria mkutano huo, si kutoka katika mabaraza ya maaskofu Katoliki duniani kote tu, bali hata vijana wawakilishi kutoka katika  makanisa mengine ya kikristo, na yasiyo ya kikristo, hata wengine wanaoishi katika hali maalum kama vile kutoka magereza na wengine kutoka katika  vituo vya uponyanji hususani madawa ya kulevya.

Hata hivyo katika mkutano huo pia watakuwa watu wengine wasio amini, baadhi ya wazazi na viongozi wa vijana, mapadre, wahudumu wa kichungaji vijana ambao wanaishi karibu na vijana ili kuweza kuwasikiliza vema hali wanazoishi dani ya maisha yao. Kwa ushiriki wa watu wazima pia utasadisa vijana waweze kuzungumza wazi  na watu wazima .

Licha ya Mkutano huo tangu Baba Matakatifu alipotoa a tamko la mapendekezo ya siku ya vijana , mikutano mingi  yenye kuwa na mwelekeo wa maandalizi hayo imeweza kufanyika sehemu nyingi kwa mfano hata kwa ushiriki wa Kardinali Lorenzo Baldisseri Katibu Mkuu wa Sinodi ya Maaskofu, mwezi machi 2017 huko Barcellona, ambapo  ulifanyika mkutano wa vijana ulio andaliwa na Baraza la Maaskofu wa Ulaya; Mazungumzo ya Vijana wa Afrika Katika mkutano uliofanyika huko  wa Afrika Dakar mwezi Januari 2018 na waliokuwa mstari wa mbele ni wakatoliki na waislam. 

Halikadhalika suala la sinodi linazungumza kila wiki  katika makutano ya kiekumene huko Taize Ufaransa; katika mkesha wa sala ulioandaliwa na Jumuiya ya Shalom katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu Roma tarehe 17 Feberuari 2018 saa 3.30 za usiku masaa ya Ulaya;Sinodi ndogo iliyoandaliwa huko Lourdes; sinodi ndogo iliyoandaliwa na majimbo ya Afrika ya Kusini mjini Durban na mikutano meingine!

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.