2018-02-13 16:19:00

Misa ya Papa Francisko Katika kanisa la Mt Marta na Patriaki wa Antiokia!


Asubuhi ya tarehe 13 Februari 2018,kama kawaida ya Baba Mtakatifu Francisko ameadhimisha misa katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican, lakini hakuhubiri, bali ametoa maneno machache  kuelezea maana ya maadhimiso ya misa ya siku hiyo! Walio udhuria misa na Papa Francisko, alikuwa ni Patriaki wa Kanisa la Antiokia wa Kigiriki-Melkiti Youssef Absi na Ujumbe wake wote. Mwisho wa Misa hiyo,Patriakia amemshukuru Baba Mtakatifu Francisko kwa lugha ya kifaransa na wote kwa pamoja wametoa baraka kwa wote!

Maneno ya Baba Mtakatifu wakati wa utangulizi wa misa amesema, “katika misa hii niko pamoja na ndugu Patriaki Youssef ambaye  anafanya umoja wa kitume: Yeye ni baba wa Kanisa, na Kanisa moja la kizamani, amekuja kumkumbatia Petro na kusema “mimi ninaungana na  Petro”.

Hiyo ndiyo maana ya maadhimisho ya leo: mkono wa Baba wa Kanisa na Petro. Kanisa moja na tajiri, likiwa na taalimungu ndani ya Taalimungu Katoliki, yenye liturujia ya kushangaza na watu, ambpo pia muda huu, sehemu kubwa wa watu hao wamesulibiwa kama Yesu.”

Baba Mtakatifu ameendelea kusema kuwa kuwa, misa hiyo itolewa sadaka kwa ajili ya watu ambao wanateseka, kwa ajili ya wakristo wanaotaseka wa nchi za mashariki na ambao wanatoa maisha, wanatoa na kuacha mali zao kwasababu wamefukuzwa". Na mwisho Baba Mtakatifu amesema, "Misa hiyo pia itolewa  sadaka kwa ajili ya utume wa ndugu patriaki Youssef".

Na mara baada ya misa Takatifu, Patriaki amemshukuru Baba Mtakatifu  Francisko kwa ajili ya misa nzuri ya umoja kwa jina la Sinodi  ya Kanisa la Kigiriki- Melkiti Katoliki. Yeye binafsi ameguswa sana na upendo wake kindugu, ishara za kindugu na mshikamano ambao ameunesha katika Kanisa lao, wakati wa kutolea sadaka Misa hiyo.

Ametoa ahadi kuendelea kuamsha nyoyo zao na nyoyo za wote, makleri na waamini pia watakumbuka daima tukio hili la kihistoria , kipindi ambacho ni vigumu kueleza jinsi kilivyo kizuri, yaani undugu na umoja ambao unawaunganisha wote kama wafuasi wa Kristo.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News

 

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.