2018-02-03 15:56:00

Askofu Mkuu Brislin: Upo umuhimu wa kufanya kazi pamoja katika nchi!


Katika hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Baraza la Maaskofu wa Afrika ya Kusini SACBC)  tarehe 24 Januari 2018, Askofu Mkuu Stephen Brislin wa Jimbo Kuu la Cape town na mwenyekiti wa  Baraza hilo amezungumzia juu ya mada ya mpango wa Kichungaji kwa ajili ya Kanisa la kanda hiyo na kushutumu vikali juu mzunguko mbalimbali ya sera za kisiasa na kitaifa zinahujumu watu wake. Wakati huo  anakubali matatizo ya wakati huu, kuwahimiza wajumbe wa Baraza hilo na waamini wote wa Kanisa katoliki  kubaki kidete  na matumaini, na kufanya kazi kwa ajili ya nchi wanayoitaka wote; hiyo ni pamoja na kuhusisha kukabiliana na matatizo ya ubaguzi na mgawanyo usio sawa wa maliz za asili katika uchumi wan chi.

Aidha amesema wanayo fursa kubwa ya kuishi utume wao, kwa mtazamo wa mwanga wa miaka 200 tangu kuanza rasmi imani ya Kanisa Katoliki nchini Afrika ya Kusini na anasistiza kuwa imekuwa tukio muhimu sana na  sifa na shukrani kwa Mungu. Anakubali kuwa maadhimisho makubwa ya  Kanisa lililoanzishwa na Mungu linaundwa na wanadamu wadhaifu. Kwa maana hiyo anasikitishwa na kipindi ambacho kanisa limekuwa kimya. Lakini hayo, anaongeza ni sehemu ya mapungufu ya ukoloni na ubaguzi wa rangi.Anatambua wazi kwamna watu wengi wameumizwa na Kanisa katika suala hili na katika masuala mengine. Lakini kwa yote hayo kwa unyenyekevu anaomba msamaha hasa kwa upande wa wa matukio ya unyanyasaji wa watoto kijinsia, matukio ambayo pia yamefanyika katika Kanisa la Afrika ya Kusini anasema leo hii wanataka kukiri na kuondokana na uovu huo na kuwalinda watoto kwa dhati.

Akishukuru kwa dhati kwa miaka 200 iliyopita ya uinjilishaji katika nchi yao; amebainisha shukrani ziwaelelee wota wanajiotlea na wao, kwa uamnifu na kwa utume walio kabidhiwa kusimamia watu na kuwa waaminifu katika utume huo.Utume huo ni kutangaza Kristo katika ulimwengu, kuhubiri na kuwaleta watu ili wakutane na Kristo mwokozi wa ulimwengu.  Anelezea juu ya  mageuzi ya mkutano wao ya kwamba, urekebishaji wa mkutano huo umezingatia kanuni ambayo kila ngazi inapaswa itende  katika huduma ya uinjilishaji na miundo hiyo ya mkutano ina maana ya kuwa katika utumishi wa majimbo na sio njia nyingine! Hata hivyo, mawazo haya mapya kabisa amesema, yamesababisha uundaji  mpya wa mpangilio mzuri wa Mpango wa kichungaji katika  maono ya Uinjilishaji kwa Jumuhiya zinazohudumia Mungu,binadamu na viumbe vyote!

Akifafanua zaidi: mpango huo unahusiana na vipengele nane ambavyo ni : Uinjilishaji; mafunzo kwa walei; uwezeshaji;  maisha ya utume wa mapadre na mashemasi; Ndoa na Familia; Vijana; Haki na Amani na kutokutumia nguvu; Uponyaji na Upatanisho;  na mwisho huduma ya kulinda na kutunza mazingira. Katika vingele hivyo 8 Askofu Brislin amevifafanua kwa kirefu; hatimaye, amemaliza akielezea juu ya ushirikiano mbalimbali aliofanya kama mwenyekiti wa SACBC, hata kazi ambayo bado inahitajika kutekelezwa  hasa masuala yanayohusu biashara haramu ya kibinadamu, wahamiaji na wakimbizi!  Na hiyo ni kutokana na ripoti ya Kanisa la Afrika Kusini (SACC) na kwamba jitihada zinaendelea hasa za  kupambana na rushwa, pamoja na kazi katika sekta mbalimbali kama vile madini, ili  madini yaweze kuwa haki ya kiuchumi wa nchi.  

Aidha akieleza matumaini na hofu yake ya sasa katika nchi yao, amewahimiza waamini wote kuwa pamoja, kama Wakatoliki wa nchi hiyo, kuungana katika imani yao kwa Yesu Kristo, kuendeleza mila na desturi zao walizochota za ukatoliki wakati wa maadhimisho ya ukatoliki wa miaka 200 iliyopita katika nchi yao.  Ni kuendelea kuamini, kutangaza na kumtukuza Mungu, katika matarajio ya ufufuko na kukutana na Bwana wetu Yesu Kristo mkombozi wa dunia siku moja.

Naye Kardinali Wilfrid Napier, askofu mkuu wa Durban, akizungumza juu ya mpango wa wakichungaji, amesema  wakati umefika kwa mkutano wa kuanzisha kamati ya kuangalia masuala makubwa yanayowakabili Afrika Kusini. Amehimiza  mkutano wa kuanzisha timu ya kuandaa fursa za nafasi kwenye masuala muhimu kama uchumi, ubaguzi wa rangi na hali ya kisiasa. Anasisitiza kuwa mpango mpya wa wachungaji utazingatia masuala yanayowakabili nchi. 

Sr Angela Rwezaula
Vatican News

 








All the contents on this site are copyrighted ©.