2018-02-02 14:00:00

Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Baraza la Maaskofu India kuanza 2-9 Februari


Mimi niko pamoja nanyi hadi miisho ya dunia .Tunaungana katika utofauti kwa ajili ya utumea wa huruma na ushuhuda,ni kauli mbiu iliyochaguliwa na Mkutano Mkuu wa mwaka wa Baraza la Maaskofu Katoliki wa India ambao wamekusanyika kuanzia tarehe 2 hadi 9 Februari 2018, huko Bangalore India. 
Mada katika sehemu ya kwanza inasismamia juu ya Yesu kuhakikisha usindikizaji wake kwa Kanisa kilia wakati na hata mahali popote. Ndiyo chanchu ya nguvu na ujasiri katika huduma ya utume wao na kushuhudia Injili kwa binadamu. Ni maelezo ya Askofu Theodore Mascarenhas Katibu Mkuu wa Barza la Maaskofu kwa vyombo vya habari katoliki vya habari. Barza la Maaskofu India lina majukumu ya kichugaji kwa zaidi ya waamini zaidi ya milioni 20 nchini India.

Mkutano Mkuu umewadia kipindi ambacho Kanisa Katoliki la India linakabiliana na changamoto kubwa hasa katika kuhudumia na kutoa ushuhuda wa Injili. Kanisa ni kubwa na mwamasishaji wa umoja katika utofauti. Lakini Makundi na vyama ambavyo vina hamasisha utamaduni wa utaifa na udini wanazidi kusikika sana. Mauaji bila hata hukumu ya sheria kwa wimbi la watu chini ya kivuli cha ulaghai au kuchinja ng’ombe au utumiaji wa nyama ya ng’ombe,umekuza hofu kubwa hasa, kati ya Wakristo na Waislam nchini India. Kuuawa kwa waandishi wa habari wanaopinga, wimbi la mashambulizi ni ishara za kuleta wasiwasi katika jamii ambayo kiutamaduni ni ya amani. Askofu Mascarenhas anathibitisha kuwa, vurugu zilizojipenyeza kwa jina la utaifa, linawapa wasiwasi mkubwa.

Katibu Mkuu anatbitisha kusema kuwa msaada wa viongozi wa serikali kwa namna ya pekee wa Waziro wa Utalii Bw,Alphonse Kananatham na wabunge wamechangia kuweka hali chini ya ulinzi. Wakati huo huo wakristo pamoja na hayo bado wana wasiwasi wa mauaji ya  kutumia sumu ambayo uameenea katika jumuiya ya wahindi,na kwa njia hiyo katika Mkutano Mkuu, Maaskofu watajadili jinsi gani Kanisa linaweza kuwa chumvi, mwanga na chachu, ili watu wote wenye mapenzi mema waweze kuungana kwa pamoja ili kuendeleza maadili ya kikatiba na kukuza taifa la amani na upatanisho. Maaskofu aidha watajadili jinsi gani Kanisa linavyoweza kuendelea kushuhudia upendo wa Yesu Kriato na kutumika taifa.

Zaidi ya hayo  kanisa pia litafana tafakari juu ya utafiti wa njia mpya za ushirikiano na serikali kwa nhaza ya mikoa, na viuo vya mipango ya maendeleo na kuendeleza taifa kwa namana ya pekee kwa watu wa kabila la Delit, makabila na watu waliosukumwa pembezoni. Ufunguzi wa  Mkutano Mkuu umeanza na maadhimisho ya Ekaristi takatifu ikiongozwa na Balozi wa Vatican nchini India Askofu Mkuu Giambattista Diquattro, wakati Kardinali Charles Bo, askofu Mkuu wa Yangon, atakuwa mgeni rasmi. Mwisho wa mkutano huo watamchagua Mwenyekiti na wasadizi wake wawili kuongoza miaka miwili. 

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News.








All the contents on this site are copyrighted ©.