2018-02-02 14:30:00

Hali ngumu na kipeo cha uchumi na kisiasa yaikumba nchi ya Chad!


Watu wa nchi ya Chad  wanaishi kipindi kigumu,ni kutokana na kuanguka kwa  bei ya mafuta ya petroli na kuchangia kipeo kigumu  cha uchumi wa nchi. Mameya wa manispaa  zote wako wanaitisha maandamano bila kikomo ili kupinga usimamizi wa fedha za serikali, ambapo pia wameamnua kukata hata mishahara ya wafanyakazi nchini humo.Viongozia wa jamii wanapinga tendo la makato ya mishahara, na kutoa  wito ili serikali iache  vitendo vya ukandamizaji, wakizuia kila aina ya mipango ya maandamano ya amani. Hivi karibuni Askari walitumia mabomu ya machozi kusambaratisha wanafunzi na mamia ya watu kutiwa mbaroni katika mji mkuu N’Djamena wakati wa maandamano yao.

Katika kipindi hiki cha mivutano ya kijamii na kisiasa, Kanisa mahalia, linawaalika watu na Taasisi husika kujikita kila mmoja katika nafasi yake aliyo nayo, lakini kwa mwelekeo wa mema kwa uwote na jitihada  ili  kuondokana na kipeo cha uchumi, bila kuangukia katika vurugu, ghasia na kukata tamaa. Hayo ni maelezo katika vyombo vya habari katoliki na Padre Mmisionari  wa kijesuiti Padre Franco Martellozzo, ambaye anaishi nchini Chad zaidi ya miaka 50.

Katika taarifa yake, anasema kuwa, kwa hakika kwa saa ni kipindi kigumu kwa ngazi ya kijamii na watu wengi wamewekwa katika mjaribu. Viwanda mbalimbali vya umma na maofisi yamesimama, kama vile shule na mahospitali. Kila kitu kimesimama. Mishahara inalipwa imechelewa, wakati huo imekatwa makato makubwa. Tendo la kukata mishahara ,limesababisha maandamano makubwa hasa kwa upande wa mashule. Tatizo hili linawatazama hasa wafanyakazi mahofisini mijini na mashule , lakini si wakulima na wafugaji, kwasababu hata kama kuna  tatizo la mabadilko ya hali ya hewa ambayo yanaathiri mavuno na ufugaji , wakulima wamezoea.

Hata hivyo nchi ya Chad iko kati ya nchi za kanda ya jangwa la sahara, mahali ambapo kwa miaka ya karibuni imekosa msimamo mkubwa kwani: Mashariki ya Chad kuna kipeo cha Sudan,Kusini ni kipeo cha Jamhuri ya Afrika ya Kati na Mashariki ni ile ya Camerun mahali ambapo mivutano kati ya imaya mbili za lugha ya kingereza na kifaransa inazidi, wakati watu wadhaifu na wenye mahitaji wanazidi kuteseka na ambao kila siku wanatamani wema wa pamoja na msaada kutoka kwa Shirika la wajesuit ( Magis) wa Italia.

Sr Angela Rwezaula
Vatican News

 








All the contents on this site are copyrighted ©.