2018-01-28 15:30:00

Papa anawaombea waathirika wa shambulio la kigaidi huko Kabul Afghanstan!


Mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana, Baba Mtakatifu ametoa ujumbe wa masikitiko yake kutokana na mashambulizi ya kigaidi mji mkuu Kabul nchini Afghanstan yalitokea Jumamosi tarehe 27 Januari na kusababisha vifo zaidi ya watu 100  na idadi kubwa ya majeruhi.  Amekumbusha hata hivyo kwamba, mapema karibuni pia huko Kabul lilitokea tena shambulio katika nyumba ya kulala. Je hadi lini watu wa Afghanstani wataendelea kuvumilia matendo haya dhidi ya kibinadamu?.  Anawaombea waathirika wote na familia zao, hata wale wanaondelea kufanya kazi kwa ajili ya ujenzi wa amani.

Kadhalika amekumbuka Siku ya maadhimisho ya Ugonjwa wa Ukoma Duniani mwaka 2018 inayoadhimshwa kila mwaka ifikapo tarehe 28 Januari. Baba Mtakatifu ansema, ugonjwa huu kwa bahati mbaya bado unaendelea kushambulia hasa kwa watu wasiokuwa na vitu na maskini sana. Kwa njia hiyo anawaombe ndugu kaka na dada hao, na kuonesha ukaribu na mshukamani, pia kuwaombea wale wote wanaojikita kusaidia ili waweze watu hao wapate  kurudi katika jamii.

Amewasalimu wahujaji wote, familia, parokia vyama na wote mahujaji kutoka nje na ndani ya nchi ya Italia. Kwa namna ya pekee amewakaribisha vijana wa Chama cha Vijana wakatoliki kutoka Jimbo Kuu la Roma.  Anawashukuru kwa shughuli yao ya "msafara wa amani" waliyoanzisha wakiwa na viongozi wao, mapadre wazazi na wahudumu wengi.  Amewahimiza wasichoke kuendelea kuwa chombo cha amani na furaha kati ya vijana wenzao.

Pia amewaruhusu vijana wawakilishi wawili wasome ujumbe wao, uliombatana na ishara ya kurusha mapuzo juu. Lakini Baba Mtakatifu aliongeza kusema: “Je mnaona hayo mapuzo ? Tunaposali vibaya na maisha yetu yasipoendana na maisha ya Yesu, maombi yetu hayawezi kufika, ni lazima kuhitaji msaada wa kusukuma illi maombi hayo  yaweze kwenda juu. Kwa maana hiyo anashauri ya kuwa,"mnapohisi kuwa sala zenu hazisikilizwi, basi tafuteni kusaidiwa na mtu yoyote”.

Sr Angela Rwezaula
Vatican News

 








All the contents on this site are copyrighted ©.