2018-01-27 16:13:00

Hotuba ya Papa kwa Wawakilishi wa Chama cha Msalaba Mwekundu Italia!


Maneno ya Mwenyekiti wenu yamenipa fursa ya kufikiria kuanzishwa kwa Chama chenu; katika matarajio yanayowasaidia na katika upeo wa huduma mnayokabiliana nayo. Ni maneno ya utangulizi wa hotuba ya  Baba Mtakatifu aliyo anza nayo wakati alipokutana na chama cha Msalaba Mwekundu nchini Italia asubuhi ya tarehe 27 januari 2018 katika ukumbi wa Mwenye heri Paulo VI Vatican. Baba Mtakatifu akiendelea kufafanua juu ya chama chao anasema, Chama cha Msalaba Mwekundi kinajikiti katika shughuli yao nchi yote ya Italia na katika ulimwengu mzima kwa huduma yao isyo na kifani yenye thamani kuanzia zana , roho na mchango wa kuweza kukuza ule utamaduni mpya wa kuwa wazi na mshikamano. 

Shughuli yao inatakiwa kupewa sifa na kutambuliwa kwa kiasi mkubwa na kila raia mzalendo kwasababu ya shughuli nyeti katika matukio mbalimbali ambapo wanakabiliana na ugumu na hatari nyingi za asili. Kwa mfano wa kesi za kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi na majanga mengine ya asili na kwamba, wao ni faraja  kwa  watu waliopatwa na majanga wakiwakilisha kwa dhati  ishara ya ukaribu wa watu. Pamoja na hayo, pia hata shughuli yao ya kuwasaidia wahamiaji wakati wa safari yao kakatisha baharina kuwapokea fukweni wale ambao wamevuka baharini , wakiwa na matarajio ya kukaribishwa na kushirikishwa.

Mikono yao wanayo nyosha kuwaokoa ni ishara kubwa ambayo inaweza kutafsiriwa  kama vile : Sikusaidii kwasababu ya muda huu na kukutoa katika bahari ukiwa salama, bali  ni kukuhakikishaia kuwa nitakuwa nawe na kuchukua jukumu ndani ya moyo wangu” anasema Baba Mtakatifu! Kwa njia hiyo uwepo wao karibu na wahamiaji, unawakilisha ishara ya kinabii na hivyo ni muhimu katika ulimwengu.  “Utume wa mtu wa kujitolea una uwezo wa kuinamia kila mtu katika hali yake ya  mahitaji na kutoa msaada kwa namna ya upendo mkuu, kwa maana inakumbusha  sura ya Kiinjili katika picha ya Msamaria Mwema (Tz Lk 10,25-35). Na katika neno moja Baba Mtakatifu anathibitisha, Yesu ambaye alikuwa tajiri, anajitoa katika mwanga wa thamani ya matendo na thamani ya msingi wa Katiba yao.

Kanuni ya kwanza msingi ambayo Katiba inahimiza ni ile ya ubinadamu ambao najikita kwa namna ya kzuia na kutoa faraja kwa kila mateso ya kibinadamu( Art 1.3). Ubinadamu unaooneshwa kwa watu wenye kujawa na mateso mengi ni sawa na ule uliomsukuma Msamaria mwema kuinami kwa yule mtu aliyekuwa chini ya ardhi  amejeruhiwa na maharamia. Yeye alishikwa na huruma hadi akawa karibu kwa maana, bila huruma si rahisi kukaribia, bali unakwenda mbali; na binadamu aliyejeruhiwa anabaki kitu kisichokuwa na sura. Mateso hayo yanafamfanya Baba Mtakatifu akumbushe na kuonesha mateso ambayo yamejaa katika dunia yetu, watoto, wazee na watu wengi wasiojulikana na ambao sura zao hazijulikani , zimejificha chini ya kivuli cha sintofahamu!

Hali hiyo inazuia kwa hakika kutotazama mwingine na kuizuia kutambua mateso. Utamaduni wa ubaguzi ni utamaduni usio kuwa na jina, usio kuwa na uhusino  hata sura. Utamaduni huo unaamua kuchagua baadhi na kuwabagua wengine. Lakini kuhimiza misingi ya kibinadamu, maana yake ni kuhamasisha tabia ile yanye kusimika mizizi katika thamani ya kila kiumbe pia ni mchakatoa unaochukua nafasi ya kwanza ya kuweka maisha ya kijamii katika kitovu na si katika uchumi bali kujali na kumsaidia mtu, si katika fedha bali ni katika binadamu ameongeza Baba Mtakatifu!

Msingi wa pili katika Kanuni yao ya Chama cha Msalaba Mwekundu  inahimiza uadilifu ambao si katika kujali mkuwa na upande wowote kama msingi wa tatu ambao chama hakisimami upande wowote iwe katika migogoro au  katika migogoro ya kisiasa, rangi au ya kidini. Kigezo hiki cha utekelezaji kinatofautiana sana na mwenendo ambao leo kwa bahati mbaya umeenea sana, wa  kutofautisha nani anayestahili hukudumiwa na kusaidiwa  kutoka kwa wale, ambao kinyume chake wanaitwa wasiyo stahili.

Hata hivyo Baba Mtakatitu ameongeza kusema kuwa  wao tayari wana siasa; Je ni chama gani cha kisiasa? utume wao ni siasa na kwamba hata Mwenyekiti wao ametamka kuwa wao ni chama cha kisiasa kwa ajili ya wenye mahitaji sana,na kwa njia hiyo anathibitisha baba Mtakatifu:wao ni chama cha kisiasa kwa ajili ya watu wenye kuhitaji msaada sana! 

Msamaria katika  Injili anaanza matendo yake bila ubaguzi: kwa maana hakujiuliza mara mbili juu ya mtu aliyekuwa amelala chini kabla ya kumsaidia, ili kujua anatokea wapi, anasadiki nini au aliyemjeruhi amefanya vibaya au  alikuwa nasababu. Msamaria mwema hafanyi uchunguzi wowote  wala kumhukumu au kutotoa msaada wake kwa kutokana kuzuiawa sheria za kimaadili au za kidini. Kwa urahisi alimfunga taratibu majeraha yake na kupeleka katika nyumba ya kulala, na kumsaidia mahitaji yake yote, ambaye katu hasingewza kuacha. Msamaria anaonesha matendo , analipa yeye mwenyewe, anapenda! Kwa maana hiyo anaongeza kusema kuwa hapo ni kusema kuwa ibilisi anaingia katika mifuko, kwa maana fadhila zinatoka mifukoni; maana analipa kumsaidia mwingine na  msamaria huyo anapenda. Nyuma yake inaonesha  sura ya Yesu mwenyewe anayemwinamia binadamu na wote ambao ametaka kuwaita ndugu, bila kubagua hata mmoja na kuwapa wokovu kwa kila binadamu.

“Chama cha Msalaba mwekundu nchini Italia kinashirikisha misingi ya kibinadamu, bila ubaguzi na kutokuwa na upande wowote wa chama na kushirikiana na Chama cha Kimataifa cha Msalaba Mwekundu pamoja na kile cha Mezzaluna Rossa, ambacho kinaunganisha  vyama vya kitaifa 190, kuunda mtandao mmoja wa kimataifa ambao ni muhimu kuandaa kwa ngaza ya ulimwengu msima msaada,kukuza uwelewa wa pamoja, urafiki na ushirikiano na amani ya kudumu kati ya watu (Tz Katiba 1,3).”
Maneno hayo Baba Mtakatifu anasema, ndiyo yawe  maana ya utume wao daima katika ujenzi wa uelewa wa pamoja, kudumisha shauku ya kimantiki ya kibindamu na jamii na juu ya hisia za kirafiki. Pia kuwa  chama kinachotazama wengine kwa miwani ya kirafiki  na si katika miwani yenye mashindano au migogoro na ili  kuweza kuwa wajenzi wa ulimwengu bora wa kuishi na wa kibinadamu.

Baba Mtakatifu amehitimisha kwa mawazo yake  yakimwendea kwa  wale ambao katika kutoa huduma yao na kusaidia wamepoteza maisha: Lakini anaongeza kusema, hawa  hawakuyapoteza bali wametoa maisha yao,kwa maana hiyo wao ni mashahidi wao. Yesu anasema, “hakuna upendo ulio mkuu wa kutoa maisha kwa ajili ya wengine”, na kwa maana hiyo hao ni  kati yao. Walobaki waige mfano, wanawasaidia nakuwalinda huko mbinguni.

Na kwa njia ya Roho mfufuka ambaye ni Roho ya upendo na amani asiadie katika njia hi ina kusaidia kuikamilisha. Na kwa wote amewapa Baraka ya Mungu na kwa namna ya pekee wale wote waliopoteza maisha wakati wa kutoa huduma yao na kwa ajili ya wapendwa wao.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.