2018-01-25 15:55:00

Ujumbe wa Papa Francisko katika Mkutano wa CEBs Katoliki nchini Brazil


Baba Mtakatifu Francisko, ametuma ujumbe wake katika Mkutano wa 14 wa mwaka  (CEBs) wa Jumuiya ndogo ndogo za kitume za Kanisa katoliki nchini Brazil, mkutano ulioanza  tarehe 23 na utamalizika tarehe 28 Januari 2018 ukiongozwa na Mada ya “Cebs na changamoto za ulimwengu wa vijijini”. Mkutano huo unafanyika katika jimbo Kuu la Londrin  na ambao utajikita katika masuala msingi matatu yanayohusu nchi ya  Brazil: nyumba, ajira na vijana!

Ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko uliotiwa saini na Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican unasema, jumuiya ndogo dogo katoliki ziwe chombo cha uinjilishaji na kuhamasisha utu wa binadamu. Anawatia moyo na baraka ili wapate kusaidia Kanisa la Brazil kwa kupeleka mbele changamoto ndani ya ulimwengu wa  vijiji na kutoa mwamko mpya wa uinjilishaji na kuwa na  uwezo wa kuzungumza na dunia ambayo inafanya Kanisa liwe jipya!

Halikadhalika katika ujumbe wa Baba Mtakatifu ulioandikwa kwa lugha ya kireno na kutangazwa katika mtandao wa Baraza la Maaskofu Brazil, Baba Mtakatifu anatumia  maneno kutoka kitabu cha Kutoka: “nimeona na kusikia kilio cha watu wangu na hivyo nimeshuka ili kuwakomboa” (Kut 3,7-8), anasisitiza kuwa, Mungu kamwe hawezi kuwa tofauti mbele ya mateso ya watu wake na kwamba, matendo ya Mungu daima ni ya wokovu, ambayo yanajieleza katika maisha binafsi na kutoa mwanga  wa Injili kwa njia ya matendo ya upendo na mshikamano.

Anawataka daima wawe na umoja katika hali zote za parokia na kuelekeza upeo wao katika Kanisa mahalia;  kwa kufanya hivyo wanaweze kukabiliana na changamoto zisizoelezeka hasa zile za ubaguzi kwa ndugu na kaka wanaoishi pembezoni. Mkutano huo unawajumusha watu karibia  3,000. Umezinduliwa Jumanne 23 Januari na maadhimisha na Ekaristi Takatifu iliyoongozwa na Askofu Mkuu Geremias Steinmetz,wa Jimbo Kuu katoliki la  Londrin.

Sr Angela Rwezaula
Vatican News

 








All the contents on this site are copyrighted ©.