2018-01-22 15:18:00

Rais wa Bolivia asikiliza maombi ya Maaskofu na raia wake!


Rais wa Bolivia, Evo Morales, kupitia mahojiano na Telesheni ya taifa  na pia kupitia tweet yake ametangaza kuwa, ataomba Bunge kufuta Kanuni mpya ya Sheria. Rais amesisitiza kuwa amefanya uamuzi huo kufuatia maandamano ya kupinga mswada huo, maandamano ambayo yamefanyika kwa miezi miwili mfululizo na sekta tofauti za jamii  huku wakidai “haki”ya kutofahamika na kuomba kufutwa kwa Mswada huo wa sheria.

Miongoni mwa wale waliokuwa wamekosoa Mswada huo mpya ya Sheria, ambao pia inaelezea uwezekano wa utoaji mimba katika hali mbalimbali, ikiwa ni pamoja na umaskini wa mama, Kanisa la Bolivia limekuwa mstari wa mbele. Baraza la Maaskofu nchini Bolivia mara kadhaa, wameomba kuondolewa kwa Kanuni hiyo ya sheria ili kuanza upya mazungumzo ya kweli na sekta mbalimbali za kijamii.

Hata hivyo mapendekezo ya Rais Morales yatawasilishwa  mapema wiki hii katika Bunge, wakati huo huo Kamati inayoratibu hali halisi zinazopinga kanuni za sheria mpya (Conade), wametangaza kuwa maandamano hayataacha mpaka uondoaji wa Kanuni ya sheria hiyo unaidhinishwa na Bunge!

Sr Angela Rwezaula
Vatican News

 








All the contents on this site are copyrighted ©.