2018-01-20 13:57:00

Msalaba wa Kiekumene kutoka Lund,umepelekwa jijini Geneva!


Tarehe 18 Januari 2018 Msalaba wa Lund umewekwa katika Kanisa dogo kwenye Kituo cha Kiekumene huko Geneva, kama ishara inayaooneka ya hatua ya mchakato wa mapatano iliyo  anzishwa na wakatoliki na waluteri. Kuweka msalaba huo katika Kanisa hicho umekuwa na maana kubwa na muhimu kufuatia ufunguzi wa tukio la Juma la Kuombea Umoja wa Wakristo, tarehe 18 Januari 2018 siku ambayo umesindikizwa na maadhimisho ya likiturujia ya kiekumene. Juma la Kuombea umoja wa wakristo kwa kawaida ni ya kila mwaka kuanzia tarehe 18 hadi 25 Januari 2018, siku amabyo inaangukia katika Siku kuu ya wongofu wa Mtakatifu Paulo Mtume wa watu. Kila mwaka siku hiyo inaongozwa na kauli mbiu, ambapo kwa mwaka huu, inaongozwa na msitari wa Neno la Mungu kutoka katika kitabu cha kutoka, “Mkono wako wa kuume Ee Mungu ni wenye nguvu na utukufu, (Kut 15,6).

Katika maadhimisho hayo wameshiriki Kardinali Kurt Koch  Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya kuhamasisha Umoja wa Wakristo, Katibu Mkuu wa Baraza la Makanisa Ulimwenguni (Wcc), Dr. Olav Fykse Tveit na Mchungaji Martin Junge Katibu Mkuu wa Shirikisho la Kiluteri Duniani (Flm) wakiwemo waamini kutoka makanisa mbalimbali ya kikristo. Habari kutoka katika mtandao wa Wcc zinasema kuwa, tafakari la Neno kwa niaba ya wote lilitolewa na Mchungaji wa Kuluteri Kaisamari Hintikka, muhusika wa mahausiano ya Kiekeumene kwa ajili ya Shirikisho la Kiluteri duniani pamoja na Kardinali Kurt Koch, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya kuhamasisha Umoja wa Wakristo.

Hili ni tukio muhimu na maana sana katika mchakato mzima wa safari ya kiekumene. Msalaba wa Lund ulitengenezwa kutokana na tukio la Maadhimisho ya ufunguzi wa kumbukumbu ya jubilei ya miaka 500 ya mageuzi ya Kiluteri iliyofanyika tarehe 31 Oktoba 2016, katika Kanisa Kuu la Lund nchini Sweden, mahali ambapo hata Baba Mtakatifu Francisko aliudhuria maadhimisho hayo ya ufunguzi wa Jibilei ya miaka 500. Ni tukio linalojulikana  kama jiwe milenia ya historia ya mahusiano kati ya wakatoliki na waluteri na vyama vyote vya kiekumene.

Akielezea juu ya kuweka msalaba huo wa Lund katika Kikanisa hicho mjini Geneva, Katibu Mkuu wa (Film , mchungaji  Kaisamari Hintikka amesema, ni ishara msingi ya kusifu na kushukuru  hatua ya tukio la kumbukumbu ya pamoja kati ya waluteri na wakatoliki huko Lund. Ni tendo muhimu na ishara ya matumaini na kushirikishana ili kuacha nyuma ya mabega yetu ile migogoro na mitafaruko iliyopita. Leo hii waluteri na wakatoliki wanaelekeza macho yao kwenye upeo wa safari ya pamoja.

Sr Angela Rwezaula
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.