2018-01-18 09:01:00

Juma la Kuombea Umoja wa Wakristo 18-25 Januari:Uekumene ni umisionari!


Katika kuelekea Juma la kuombea Umoja wa Wakristo kuanzia tarehe 18 hadi 25 Januari, Gazeti la Osservatore Romano limetoa tafakari kuhsua suala la uekumene  kwa mtazamo wa Kardinali Kurt Koch, ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya kukuza Umoja wa Kikristo akithibitisha kuwa uekumene ni kama utume. Mnamo mwezi Oktoba 2019, utakuwa ni mwezi maalumu wa kimisionari kwa mujibu wa matashi ya Baba Mtakatifu Francisko, “ ili hatimaye kuweza  kuamsha ufahamu zaidi wa utume wa watu (Misio ad gentes) na kujikita kwa upya katika mabadiliko ya maisha ya kimisionari na kichungaji kwa ujumla.”

Kaardinali Koch anaandika kuwa, uamuzi huo ulitangazwa kwa wote  katika ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko wakati wa tukio la kuzindua  maadhimisho ya miaka 100 tang  Waraka wa Kitume wa Papa Benedikto XV kwa jina “Maximum illud”, utangazwe, unaohusu  shughuli za kimisionari katika dunia. Baba Mtakatifu amekumbusha kwamba,inawezekana kutambua mwezi wa maalumu wa kimisionari hata kuanzia mwezi wa kimisionari wa Oktoba 2018. Hivyo suala  kama hili ni pamoja na kuchangia shughuli za tafakari msingi za  kimisionari na uwajibikaji wa kiekumene.

Kardinali Koch anaendelea na kuandika kuwa, mahusiano kati utume wa kimisionari na kiekumene umenza tangu hawali na umekuwa ndiyo hatua ya kwanza ya kimisionari. Maelekezo hayo msingi yanajieleza kwa dhati tangu mkutano wa kwanza wa dunia juu ya utume wa kimisionari; mkutano ulio fanyika Scotland katika mji wa Edinburgh mnamo mwaka 1910. Walioudhuria mkutano huo, walikuwa wanafahamu vizuri aibu iliyokuwa ipo katika makanisa na jumuiya za kikristo. Aibu iliyotokana na ushindani katika kazi zao za kimisionari, kwani  walikuwa wameharibu uaminifu wao katika kutangaza Injili ya Yesu Kristo, hasa katika mabara ya mbali. Aibu hiyo inatokana na kutangaza  katika tamaduni nyingine Injili, wakati huo huo wakiwa na ufahamu halisi wa migawanyiko na mitafaruko iliyokuwapo katika Kanisa la Ulaya.

Mitafaruko hiyo ilikuwa ni jambo la uchungu na ukosefu wa umoja kati ya wakristo waliokuwa wanawakilisha tayari vizingiti vikubwa katika utume wa kimisionari duniani. Kardinali Koch aidha anaandikia, ushuhuda wa kuaminika kwa njia ya matendo ya wokovu wa Yesu Kristo katika ulimwengu unawezekana tu iwapo Makanisa yanaweza kuponya majeraha ya migawanyiko katika imani na katika maisha.

Wakati wa mkutano huo huko Edinburgh; ni Askofu wa kimisionari wa Kiangiliakani Charles Brent, aliyeonesha jitihada za nguvu ili kushinda zile tofauti zinazohusiana na mafundisho ya imani na sheria za Makanisa ambazo zilikuwa zinaleta utofauti katika mchakato mzima wa kuelekea umoja kamili. Kwa kuzingatia utambuzi mkuu wa sasa uliopo kati ya utume na uekumene, ni wazi kwamba itakuwa rahisi kutambua zaidi ni  kwanini yapo maendeleo tangu mkutano huko Edinburgh  kwa njia ya vyama viwili ambavyo vimesindikiza hatua za mchakato wa  uekumene hadi nyakati zetu.

Kulianzishwa Chama cha kikristo cha kujikita katika matendo ambacho  kiliitwa “Maisha na Kazi” kilichoanzishwa mnamo mwaka 1914 huko  (Konstanz) nchini Ujerumani, kwa lengo la kukuza kwa nguvu mshikamano wa kiekumene katika kukabiliana na changamoto kubwa za jamii, kwani  nyakati hizo, kulikuwa na kazi kubwa inayohitajika ya ujenzi wa amani kati ya watu. Shughuli kubwa ya chama hicho ilikuwa ni kuchangia kutafuta suluhisho la matatizo ya kijamii na kuhamasisha wakristo wawe na nguvu za kisiasa na  umoja kwa nyakati hizo.Nguvu hizo ni kama vile zilitendeka, kwa mfano wa Chama cha Mataifa, kwa utambuzi kuwa dunia iliyokuwa tayari imejaa migawanyiko na migogoro na hivyo , wakristo na Makanisa wangeweza kujikita barabara katika ujenzi wa amani na umoja wa kiekumene.

Hata hivyo mwaka 1910 mzizi mwingine wa chama cha kiekumene ulianzishwa huko  Edinburgh, chama hicho kiliitwa “Imani na utaratibu wa sheria” ambacho kilijihusisha na suala la imani na utaratibu wa sheria ya Kanisa,ambapo mnamo mwaka 1948 kikawa Tume ya kujitegemea ndani ya Baraza la Kiekumene la Makanisa. Kwa njia hiyo baada ya Mkutano wa Edinburgh matokeo yake yameonesha wazi kuwa, matendo ya ushirikiano wa kiekumene ulipaswa kufanywa tu na Makanisa, ambayo hawali ya yote yalikuwa yanakubali matatizo na vyanzo vya migawanyiko ili kujikita katika mafundisho ya imani na juu ya uhusiano wa masuala ya kitaalimungu na utafiti wa umoja katika imani. 

Vyombo vitatu hivyo, vinawakilisha changamoto mbalimbali ndani ya hatua za mchakato wa kiekumene. Imani na utaratibu wa sheria (Faith and Order) inajihusisha na masuala ya kitaalimungu katika mahusiano na imani na mwisho kuhamasisha utafiti wa kuweza kufanya umoja unaonekane, umoja wa  kiliturujia, katiba ya Kanisa na utume wake. Maisha na Kazi (Life and Work inakabiliana na changamoto za kileo katika njia za uekumene kwa kuzingatia juu ya mshikamano kati ya Makanisa na  katika huduma duniani kote. Na Chama cha kimisionari kwa namna ya pekee ni katika kutoa ushuhuda  wa pamoja wa wakristo katika dunia na mbele ya dunia.

Utume na uekumene unahitaji kusaidiana kwa pamoja. Kanisa la kimisionari kwa dhati na asili yake  ni Kanisa la kiekumene ambalo linajihusisha na shughuli zote za kimisionari. Hata hivyo katika Mtaguso wa Pili wa Vatican , walitambua uwazi wake ile katiba ya kichungaji katika Kanisa la ulimwengu mamboleo kwa Waraka wa Gaudium et Spes, yaani mwanga wa mataifa. Mkutano wa mtaguso ulikuwa ulijipenyeza kwa kina katika matendo ya Kanisa, wakisisitiza kuwa Neno lake si kwa ajili ya watoto wa Kanisa na wale ambao wanatamka jina la Kristo bali ni kwa  watu wote. 

Kardinali Kurt Koch anamalizia ufafanuzi wake kwamba Uinjilishaji lazima uwe na ufunguo wa muziki wa kiekumene ili kwa njia ya sauti zake nzuri ziendane bila kutofautiana. Iwapo Juma la maombi kwa ajili ya umoja wa wakristo litasaidia kwa kina kutambua kile ambacho kilikuwa ndani ya moyo wa Yesu wakati wa sala yake na kutambua kwamba umisionari na uekumene ni vitu viwili kama mapacha, basi ndiyo utakuwa mchango mkubwa wa hatua ya  maandalizi ya mwezi wa maalumu wa kimisionari 2019.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.