2018-01-16 08:55:00

Kanisa la Marekani linashutumu kauli ya Trump dhidi ya binadamu!


Rais Trump ametumia neno lisilostahili dhidi ya Haiti na nchi za Afrika alipouliza swali la ni kwa nini Marekani iwapokee wahamiaji kutoka mataifa ya kimaskini kama Haiti na Afrika. Kufuatia na matamshi hayo makali ya Trump, maaskofu wa Marekani wanaonesha wasiwasi mkubwa, kutokana na usema huo mkali.

Wanaeleza hayo kupitia  kwa James Roger msemaji mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Marekani  kwamba, maneno Rais Trump wakati wa  mkutano tarehe  11 Januari 2018 aliyokuwa amehitisha wajumbe kujadili mkataba uliopendekezwa wenye nia ya kuwazuia wahamiaji kupeleka familia zao nchini humo, pia kutaka kugeuza mpango wa Green card kutumika tu kuwapa kinga maelfu kwa maelfu ya wahamiaji vijana dhidi ya kurudishwa nyumbani kwao si maneno ya kiungwana ni maneno ambayo kwa hakikia yanazuia haki na ulinzi wa kibinadamu.

Kila binadamu ni mfano na sura ya Mungu, hivyo tamko la kudharua taifa na watu wake ni ukiukwaji wa msingi ya kweli na ambayo imeonesha uchungu mkubwa.Ni lazima kuacha lugha kama hizo zisizi za kibinadamu dhidi na kaka na dada. Msemaji wa Baraza la Maaskofu anaendelea kuonesha hata suala la  majadala wa hivi karibuni kuhusu wahamiaji na hali halisi ya kuzuia kinga  ya muda mfupi ya vijana lakini nane katika mapano wa Daca.
Kufuatia maneno mabaya sana ,hata viongzoi mbalimbali wa Kanisa na serikali mbalimbali duniani, wameshutumu vikali juu ya tamko la Trump dhini ya Afrika na haiti, wanakiri kuwa, maneno hayo ni hatari sana na kuonesha bayana kile ambacho kilisubiriwa tayari kabla ya kuanza utawala wake. Maneno yake yanazidi  kuonesha ubaguzi wa rangi na kuongeza kukanyaga haki msingi za binadamu wakimbizi na wahamiaji.

Naye Kardinali Seán O’Malley wa Jimbo Kuu la Boston katika blog yake amesema kuwa, miaka mingi wamefika watu wengi Marekani kwa ajili ya kushirikiana maisha yao, utamaduni, imani , lakini roho ikuwa tofaut na lugha ambayo leo hii imetumika kutoka kwa kiongozi dhidi ya wahamiaji. Kwa maana hiyo lugha hiyo ni ngumu na ambayo haukubalikiwa, siyo ya makaribisho,hata ya heshima. Taasisi zio na  sauti mbalimbali zenye uwezo kuungana pamoja  kupinga upotofu wa tamko la namna hiyo katika ulimwengu.Ikiwa kiongozi wa ngazi ya juu na nchi huru anataka kuheshimiwa  basi hana budi kutoa heshima kwa watu wa mataifa mengine na kuheshimu tamaduni nyingine.

Hata hivyo hata katika  dunia ya watawa, wamegutuka sana kusikia Rais wa nchi anatumia lugha chafu na kukashifu watu wa Haiti , El Salvatdo na nchi za Afrika hasa , kwa uwepo wa watawa wengi na nyumba nyingi katika mataifa wakihudumia raia wengi . Msemaji Mkuu wa Watawa 2,900 wa Shirika la Huruma ameliambia shrika la habari kwamba, wanapokea wahamiaji na wakimbizi katika mashule, makanisa na taasisi mbalimbali za afya: hivyo kutokana na lugha aliyotumia Trump , si haki kutumika katika nchi hiyo kwa wazalendo wake. Na hakuna mtu anaweza kuelezea uongozi wa aina hiyo katika nchi huru ya Marekani.

Na baadhi ya raia wa Haiti wamemtaka kwamba Trump aombe radhi Afrika na Haiti. Hakuna  anayekubaliana  na maneno kama hayo kutoka kwa kiongozi kama huyo na hivyo, akiwemo mwanaharakati  wa Haiti kwa jina Rene Civil ambaye amemtaja Trump kuwa sawa na saratani duniani kote na kwa nchi yake, na mtu anayesababisha mgawanyiko miongoni mwa watu. Katika maneno yake amesema"Tunamtaka Donald Trump kuomba radhi kwa bara zima la Afrika na kwa Haiti, nchi ambayo damu ya watu wake ilitumika kupitia mababu walioikomboa Marekani kutoka utumwani.

Wademokrati wamemkosoa pia Trump kuhusu matamshi yake dhidi ya raia wa Haiti na Waafrika kwa kile walichosema kuwa yanaonesha anawapinga wahamiaji. Mbunge Luis Gutierrez wa Marekani amesema wanaweza kusema kuwa wanajua kwa asilimia 100 kuwa Rais Trump hawapendi watu kutoka baadhi ya nchi au watu wenye rangi fulani ya ngozi.

 Sr Angela Rwezaula 
Vatican News

 

 

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.