2018-01-16 14:00:00

Ask.Mkuu De Donatis:Siri ya uaskofu mwema ni ekalu,kushuhudia na kufuasa!


Tarehe 13 Januari 2018, Askofu Mkuu Angelo De Donatis, Makamu Askofu Jimbo kuu la Roma, amewasimika rasmi,Maaskofu wateule wawili katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane Laterano. Maaskofu wateule ni Padre Daniele Libanoi, padre wa Shirika ya Yesu na Padre Paolo Ricciardi, alikuwa padre wa Jimbo. Mapadre hao wawili waliteuliwa na Baba Matakatifu Francisko mnamo tarehe 23 Novemba 2017 kuwa maaskofu wawili wasaidizi wa Jimbo Kuu la Roma. Maadhimisho ya kuwaweka wakfu na Makamu wa Askofu Jimbo Kuu la Roma pia alikuwa pamoja na askofu  Gianrico Ruzza, Msaidizi wa Jimbo katika eneo la Roma ya Kati na Askofu Andrea Turazzi, Askofu wa Jimbo la Mtakatifu Marino-Montefeltro Roma. 

Askofu Mkuu Angelo De Donatis wakati wa mahubiri yake ametafakari kwa kina  mada ya siri ya kuwa askofu mwema, kwa kutumia ufunguo wa maneno matatu ambayo ni ekalu, ushuhuda na mfuasi. Akichambua juu ya ekalu, kwa kutumia  maneno ya Mtakatifu Paulo yasemayo “ miili yenu, ni ekalu la Roho Mtakatifu. Maneno ya Mtakatifu Paulo anabainisha kuwa ni mapinduzi kwa maana ni kuonesha kuwa sasa, Mungu wa majeshi haishi tena katika ekalu au katika mlima Sayuni; Yeye anaisha sasa katika  moyo wa kila mbatizwa. Kila ndugu tunayekutana naye ni fumbo. 

Zamani nje ya uwanja wa ekalu la Yerusalem, ulikuwa umetengwa sehemu mbili na  na ukuta. Ndani yake kuliandaliwa  nafasi ya madhabahu na sehemu nyingine ya wale ambao walikuwa hawakutahiriwa. Juu ya lango kuu la kupita katika kizingiti cha jiwe, palikuwapo na maandishi ya ilani kali kwamba, myahudi aliyekuwa akivuka hapo, alikuwa ni mhusika wa kifo chake binafsi. Tangazo hili lilikuwa likitaka kuonesha utakatifu wa dhabahu hilo. Kwa maana ni yule tu aliyekuwa na agano na Mungu angeweza  kudiriki kuingia na kuwa mbele yake.

Kama maaskofu wapya,  Askofu Mkuu De Donatis ameongeza kusema, wao wamekabidhiwa kama vile aina mbili za utume katika ndugu, kama ilivyokuwa zamani katika ekalu. Uwepo wa Bwana kwa namna ya pekee, utaonekana  kwa Askofu Mteule Daniele kukabidhiwa shughuli ya Makleri na  Askofu mteule Paulo kukabidhiwa wagonjwa. Kwa maana hiyo,wao katika utume watakutana kila mmoja mahangaiko,ambayo ni  kama vile wanakwenda kutafakari zaidi upeo wa ukuta wa wakati ule na kuona  mwanga katika mlima wa Sayuni. Maaskofu hao wanapaswa kuwa wasimamizi na walizni  na si mabwana; na kuwa na Roho ya utakatifu anayeishi ndani ya roho zao.

Aidha amebanisha kuwa, kile anachokieleza  si kwamba ni ushauri, bali ni ukweli wa uwepo halisi wa Bwana anayeishi katika nafsi ya wale watakaokutana nao. Kwa maana hiyo, Bwana  anaishi katika makuhani na mashemasi, kwa njia ya fadhila ya Sakramanti waliyopokea; anaishi katika ndugu wagonjwa katika nguvu ya wale anaoteseka na ambaye inaonesha utakatifu kwa ishara ya Msalaba wao. Amesisitiza kuwa ipo haja na huduma ya wagonjwa hao, kwa maana jumuiya bila kuwa na utume wao, ni kama chama tu, jumuiya isiyo kuwa na nafasi kwa ajili ya wagonjwa ni kama ramani tu ya hali halisi.

Ufunguo wa pili ni ushuhuda. Ili kuelezea neno hilo amesema, Yohane Mbatizaji alihamaki, “Tazameni! Huyu ndiye Mwanakondoo wa Mungu”.  Hakusema, “Tazama mimi”, bali alielekeza kwamba  “Tazameni”. Mwanakondoo ni kiini cha tangazo la unabii: uwepo wake unaonekana nyuma ya mwana wa Kristo. Katika Injili inaeleza wazi kuw, Yohane alikubali  hatua ya kuawasindikiza baadhi ya wafuasi bora katika shule ya Yesu. Yeye hakuwa bwana au kushikilia madaraka binafsi. Maana  yeye aliwasukuma na kuwahimiza  wafuasi kuelekea kwake Kristo, wala hakuwa na majivuno au wivu.

Matakatifu Yohane Mbatizaji katika sura ya mwanakondoo imejionesha katika Kitabu cha Kutoka sura ya 10; mahalia ambapo  wanaongea juu ya maandalizi ya Pasaka: Nyama ya mwanakondoo,ambayo wayahudi walikula wakati wa usiku wa kukumbia kutoka  Misri, ili wapate nguvu za kuvumilia safari ndefu; damu iliwahakikishia ulinzi dhidi Malaika mwangamizi. Akilinganisha na mwanakondoo wa Yesu Yohane Mbatizaji, anaungama kuwa hakuna yoyote zaidi ya Yesu  anaweza kutoa waamini  katika mti wa utumwa na uhuru wa wana wa Mungu.

Yesu anaimarisha waamini wake kwa njia ya nyama na kuwakomboa kwa damu yake. Anawalisha na kuwafanya wawe wapya, anawashibisha na kuwasamehe. Maisha ya shuhuda ambayoYohane Mbatizaji ameonesha ni kizingiti kikuuu ili kutambua kuwa Kristo ni utajiri wetu wa kutosha. Kwa njia hiyo hakuna yoyote hata viongozi wa Kanisa wanaweza kujifanya kuwa ndiyo waanzilishi wa mwanzo na mwisho wa uokovu wa  mtu.

Ni lazima kujifungua na kuwa mashuhuda bila upendeleo au kimbelembele. Ni lazima kuwa kiini cha ukristo na kuonesha  nini maana ya Mwanakondoo anayeondoa  dhambi za dunia. Maaskofu hao watakuwa maskini iwapo, kama viongozi wanatakuwa ni washabiki wa kufunika utupu au kufanya jumuiya ya kikristo kuwa kama  kiwanja cha kuonesha uwezo walionao. Kwa maana hiyo, Askofu Mkuu De Donatis, amewataka maaskofu wapya wasaidizi, kuendeleza unyenyekevu na upole ambao unafahamika kwa watu wengi ili waelekeze Mwalimu na kuwatia moyo watu waweze kuwa na matumaini katika Roho Mtakatifu.

Neno la tatu na mwisho kuhusu ufuasi. Yesu aliwajibu mitume wawili wa Yohane  walio muuliza unaishi wapi, na  kwamba, njooni na mtaona.  Amefafanua kuwa hili lilikuwa ni swali ambalo kawaida  wayahudi walikuwa wakiomba kwa mwalimu ili waweze kuelewa zaidi wakati wa darasa lao. Na Injili inaonesha kuwa siku hiyo wafuasi walibaki na Yesu siku nzima.

Je tunatambua nini maana  ya kubaki? Ni neno msingi katika Injili ya nne; kwa maana tunaona kuwa, Maria alibaki chini ya miguu ya msalaba; Yesu anawaita waamini wabaki katika Neno lake. Kwa maana hiyo neno kukaa au kubaki” ni mtindo wa kuonesha upendo wa kila mfuasi. Na kama tungeweza kutafsiri katika lugha rahisi, tunaweza kutumia neno la ”kutegemea”. Sisi tunasema kuamini Kristo labda tunataka hata kushirikiana naye, lakini utashi wa kutegemea yeye siyo jambo rahisi namna hiyo. Iwapo katika mwili wetu tunaweza kufanya uzoefu wa ukweli wa maneno yake asemayo, ” bila mimi hamwezi kufanya kitu” labda  mwishowe ndipo tunaweza kukubali juu ya neno hilo la kutegemea nguvu ya Roho Mtakatifu. Kwa maana nyingine kufanya uzoefu wa kutofanikiwa katika maisha au vizingiti binafsi, ndiyo siri ya kujifunza namna ya kubaki na Kristo.

Je mpaka lini tunasukumwa kufanya uzoefu wa upendo na Mwalimu? Ni kwa njia ya kusikiliza Injili isemayo “ Wewe  ni Simoni Mwana wa Yohane , kuanzia sasa utakuwa Kefa”. Yesu anabadili jina la Simoni na kumsaidia kufahamu jambo msingi. Kutegemea Yeye maana yake ni kujikabidhi kwake, hadi kukubali yeye afanye mapinduzi katika maisha yetu binafsi na historia yetu na kwamba,  hiyo ndiyo Shule ya maisha! amethibitisha Askofu Mkuu De Donatis.


Sr Angela Rwezaula 
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.